Nissan Dualis yawaka moto. Hizi gari zina shida gani?

Gear box ya hii gari wengi wanaua kwasababu ya hydraulic wanazoweka.. either wanaweka hydraulic isiyo sahihi(NS-2) au wnaweka hydraulic hafifu na sio kwenye level yake inaYotakiwa...lakini pia hzi gari zinatumia gear box ya belts isiyokua na gear za menomeno (yaan CVT transmission/continuous variable transmission), ambayo inafanya isiwe gearbox nzuri ya kuhandle too much power hasa kwa wale maniac/rough drivers wanaotaka ndani ya sekunde kafika speed 70, sasa watu wengi hawajui namna ya kuishi na transmission system (gearbox) hii ndo maana wanaziua..angalia hata Toyota zinazokuja na gearbox ya CVT mfano ist new,sienta,rumion, belta, ractis,vitz,premio/allion new, utakuta zipo na same problems why because of putting wrong transmission fluid....jaman always weka transmission fluid recommended na manufacturer pia avoid frequent changing ya transmission fluid... change at least after every 30,000km kama unamatumizi heavy ila kwa matumizi ya kawaida unaweza change kwa interval ya 50,000km... Tunza gari likutunze
 
Hilo gari lilikuwa used japan au brand new?
 
Ninavyotafuta pesa kwa shida hivi alafu ninunue gari iwake moto aisee ntapata ukichaa
Lipia comprehensive insurance with excess buyback ili usipate kichaa..with many insurance products there are many ways to transfer risks to somebody else ili pressure iwe ndogo (at least uweze ku restore position yako ya kurudish gari)
 
Mshaanza mafundi maiko.
Teknolojia muwezi mnaaishia Kubahatisha tu. Kuna fundi kakorofisha Alphad mpaka ijitambui nikiwasha inafungua vioo.
Kesho namdamkia tumalizane hajui uchungu wa kununua gari
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Fundi Chidi anakwambia ukibadili oil ya engine mara 3 ya 4 ndio unabadili oil ya gearbox tena. 😀

Ukiangalia kwa makini utagundua kuwa kila baada ya kilometre 10,000 unabadilisha transmission fluid. Ni ukichaa
 
Nataka niingie veta nkasome kozi ya umeme wa magari. Nataka nije niwapiku mafundi uchwara. Vp huko mtaan hii kozi ya umeme wa magari ina hela??
 
M nakumbuka siku moja tulienda pale sinza kwa wale jamaa wana deal na nissan dualis, wakaipima ikatoa fault kama 6 hv, tatu kwenye gearbox na 3 kwenye engine sensors.

Akasema gearbox inahitaji kubadilishwa transmission zen fault za kwenye Engine atafuta halafu atembelee kama siku mbili hv arudi wapime tena kama kuna falt itajirudia basi watabadili spea husika. Akabadili transmission siku ile baada ya wiki hv akanipigia simu akiniuliza ivi wale walibadili oil ya geabox? Nikamuuliza kwann anasema hvyoo...akanijibu kuwa leo gari imegoma kuondoka alipoita fundi kuja kuikagua akamwambia gearbox haina oil, ikabidi anunue tena nyingine akaweka ndio gari ikatembea.

Nikamuuliza kwani hyo gari kuna mahali inavuja chini? Akasema hapana. Hvyo basi hzi gar bia zinatabia ya kupoteza oil ya gear box, na hyo gari hata mwaka na nusu haina.

Pili toyota ilikuwa mwanzo kabla hawajajua ila kwa sasa wanaelewa mafundi wengi ndio maan husikii tena vilio vya gearbox kama awali
 
Maeneo ya mbezi beach tangi bovu, Nissan Dualis imekutwa inawaka moto yan imelipuka. Mimi binafsi hii ni dualis ya 4 kupata taarifa imewaka moto. Hizi gari zina shida gani? Halafu hizi ndo sababu nyingine zinazochangia hata bei yake kushuka.
Tatizo gari modern sio tatizo gari kama gaei unaweaa kuta

Gari ya kisasa inahitaji ufundi wa kisasa sio wa mazoea.

Mfano, Kuna siku nimeunguza fyuzi hapa hom, naitafuta kwa fundi umeme. Ananishauri 'we hata usihangaike chukua tu kipande cha waya unganisha huku na huku itawaka!!'. Sasa kwa kujua au kutojua kazi ya vifaa vipya ndio kuna "ufundi" wa kuvibypass bypass tu. Lazma viwake vyuma.
 
Kwa kupiga Recall maana ake ni design error from the manufacturer. Sasa hizi zinazo waka ndo wajapani machi nooo hawakuzirudisha[emoji23]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Nataka niingie veta nkasome kozi ya umeme wa magari. Nataka nije niwapiku mafundi uchwara. Vp huko mtaan hii kozi ya umeme wa magari ina hela??
Utapata stress yawakufunzi wa veta..not bad mkuu ukienda ila itapendeza kama wewe binafsi ukiwa idea ya kitu unachoenda kusoma, ukiwa na interest, then upo na natural intelligence inayokusaidia kua intuitive..hiki ni kitu cha muhimu sana kwenye career maana unaweza enda ukasoma mpaka ila natural ability haipo struggle inakua kubwa but of you were made for who you want to become, basi mambo yanakuwa very easy na yanaenda so natural mkuu. Kila la kheri mkuu kuna hela nyingi huku..pia tafuta tools sahihi za kazi.
 
Kwa kupiga Recall maana ake ni design error from the manufacturer. Sasa hizi zinazo waka ndo wajapani machi nooo hawakuzirudisha[emoji23]
Alafu Kingine Wajapan Wanaweza toa model za Gari ata 8 au zaidi Engine ni aina moja. Wanaweka tofauti kidogo sana! Sisi huku ni Jalala Tunaletewa tu no quality no Support
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…