Nissan Dualis yawaka moto. Hizi gari zina shida gani?

Nissan Dualis yawaka moto. Hizi gari zina shida gani?

Dualis zimekuwa nyingi sana mtaani Kama ist tuu sasa zinakaribiana. Kunakipindi ist nazenyewe watu walisema zinawaka moto sana. Ila ukitaka kujua tatizo kubwa ni vile vifaa vinavyoongezwa after market kwenye gari. Unaenda pale lumumba unaambiwa kuna fundi akifungie alamu sawa, Redio sawa lights ndani sijui miguuni sawa na wala ujui hao jamaa Kama ni mafundi wa uwakika au ndo wale wameanza jana. Hapo ndo tatizo linaanza. Ukitaka kufunga hivyo vifaa vingine vya nyongeza uwe makini tafuta fundi wa uwakika wa umeme hata Taa zile Za buster za hizi gari za sikuizi sinazinguaga sana kwasababu tuu kitu kimepita mda wake Kama miaka kumi imepita sasa usikubali fundi maiko akushauri aunge direct vitaa vya kawaida badala ya busta zake utajuta.
Lamwisho maderee tuwe na fire extinguishers 🧯 za uwakika ndani ya gari siyo zile Kama kidawa cha mbu cha Bajaji na ujifunze namna ya kuitumia. Nimeshaokoa discover ilikuwa inawaka na dereee ajui kutumia extinguish na alikuwanayo.
 
Gari hii na Nissan nyingi za kisasa zinakuja na electrical system ya IPDM yaan (An intelligent electronic power distributor module with a cut-off function that ensures and manages the power supply for a scalable number of connected loads in the vehicle)..hii module ipo kwenye fuse box ya hizi gari, sasa mafundi umeme wa kibongo wengi hawajui how IPDM power distribution module works, sasa wanaishia ku-loop mawaya kizembe na ku-bypass system ambayo inaji self diagnose yenye na kuji regulate yenye for optimal power distribution kwa kuzingatia electric load za module mbalimbali za gari...sasa mbongo/fundi wa Chini ya muende anaetumia tester kufanya kazi ya umeme akisha fanya yake basi utakuta system inashindwa ku detect power load kwenye system ambayo imeguswa matokeo yake ina over power or underpower..but iki overpower system ambayo waya / njia zake zipo designed kubeba umeme mdogo basi resistance inakua kubwa na kutengeneza joto kali ambalo eventually inapelekea cheche/moto andapo tu ignition itakutana na mafuta..kumbuka kama system ingekua inafanya kazi inavotakiwa ina maana yenyewe automatically ina detect na ku regulate power output iendane na load (ndo maan system inaitwa intelligent power distribution module)

System hii haipo kwenye Toyota..ukifungua fuse box ya Toyota nyingi utakuta ni relays na fuse but hakuna card (printed circuit with chips, diodes etc..) kumbuka IPDM ni system nzuri sana ikiwa inafanya kazi.short za kipuuzi puuzi upati.
Hebu toa na ushauri sasa nini kifanyike ili kiepuka hii changamoto.
 
Soon na wakata bima watazikataa hizi dualis, kama Kenya kuna baadhi ya magari bima wamekataa kabisa mfano, Succeed, probox, subaru n.k. Bima ni biashara
Hata Tanzania kuna baadhi ya kampuni hawataki kukatia comprehensive brands kadhaa za Subaru.
 
Wapo Mafundi wanaojua ata jinisi ya Kurekebisha hizo tatizo na hapa JF tuna Fundi mzuri mbobezi wa hizi ishu, worry not , ukimwitaji ni PM nikupe ID yake umcheck ana Gereji yake Mwenge na habahatishi yupo vizuri sana
Weka namba yake hapa. Unaficha nini sasa Boss?!
 
Mshaanza mafundi maiko.
Teknolojia muwezi mnaaishia Kubahatisha tu. Kuna fundi kakorofisha Alphad mpaka ijitambui nikiwasha inafungua vioo.
Kesho namdamkia tumalizane hajui uchungu wa kununua gari
Inafikiri hauko ndani ya gari...
 
Nissan mbovu sana. Nimeshatumia matoleo yake manne sina hamu nazo
Bluebird
Primera
Serena
Navara
Esp unaponunua sec hand from Tanzania. Haya magari wengi wanayanunua sababu ni cheap.
 
Under normal driving conditions do not change ATF. Hii sentensi huwaga watu hawaelewi, fundi anakwambia ukimwaga engine oil mara ya pili ya tatu mwaga na gearbox oil. Ovyo kabisa sisi wabongo. Bro ume elezea point zako vzuri sana na huu ndo ukweli.
Ni kweli mkuu alichoeleza mtaalamu kina sound, kuna fundi aliniambia "hii transmission fluid inayokuja na gari ni ya kubadilisha" tena alisema kama ulivyoandika kuwa nikienda kumwaga engine oil nimwage na hiyo wakati mie sio mtu wa extreme driving. Ni mizunguko ya kawaida sana na mara chache route ndefu.

Nimejifunza kitu.
 
Aisee ni kweli kuna dada mmoja anayo hua ananiambia hii gari sjui ina kichaa!! Vioo vinajifungua vyenyewe tu
Sasa hiyo si shida ya umeme, hayo ni matatizo ya kawaida kwenye gari yoyote ikiwa na shida eneo la umeme.
 
Gear box ya hii gari wengi wanaua kwasababu ya hydraulic wanazoweka.. either wanaweka hydraulic isiyo sahihi(NS-2) au wnaweka hydraulic hafifu na sio kwenye level yake inaYotakiwa...lakini pia hzi gari zinatumia gear box ya belts isiyokua na gear za menomeno (yaan CVT transmission/continuous variable transmission), ambayo inafanya isiwe gearbox nzuri ya kuhandle too much power hasa kwa wale maniac/rough drivers wanaotaka ndani ya sekunde kafika speed 70, sasa watu wengi hawajui namna ya kuishi na transmission system (gearbox) hii ndo maana wanaziua..angalia hata Toyota zinazokuja na gearbox ya CVT mfano ist new,sienta,rumion, belta, ractis,vitz,premio/allion new, utakuta zipo na same problems why because of putting wrong transmission fluid....jaman always weka transmission fluid recommended na manufacturer pia avoid frequent changing ya transmission fluid... change at least after every 30,000km kama unamatumizi heavy ila kwa matumizi ya kawaida unaweza change kwa interval ya 50,000km... Tunza gari likutunze
Kaka Dualis yangu now ina ugonjwa wa kutetemeka pindi napo kanyaga mafuta kwa mengi.Nini itakuwa shida na Je Gereg nzuri ya hizi gari naipata wapi..???
 
Back
Top Bottom