Nissan Dualis zitajiondoa zenyewe sokoni

Nissan Dualis zitajiondoa zenyewe sokoni

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Ni kama mamlaka za ukaguzi na KUSIMAMIA UBORA wa vyombo vya moto vinavyoingizwa nchini zimeshindwa Kazi, ama kuna uzembe mahali ama rushwa.

Kwa modeli za magari yanayoingia nchini kwasasa NISSAN DUALIS zinaongoza kwa kuwaka moto.. Hivi mamlaka halilioni hili tatizo? Ama kwa vile nyingi hazijasababisha maafa makubwa?

NISSAN anaongoza kwa model nyingi mbovu ukiachana na NISSAN safari, Nissan Caravan nk. Jiulize ni kwanini kwa asilimia 95 hakuna NISSAN (IT) Wenzetu wamegutuka nini?

Hili taifa halijaanza kuingizwa mikenge leo Miaka ile ya 80 CCM ikanunua/ikapewa magari ya Korando SsangYong
ssangyong-korando-i-k4_thumb.jpg
kutoka Korea kusini nadhani... Zilikufa zote! Leo ukimuona mtu ana Korando hilo ni body tuu engine imeshawekwa ya Toyota

Hatukukoma tuu miaka ya tisini Mwanzoni Jeshi letu likapata magari ya Hyundai

Car-History-Hyundai-Sonata-_-Body-10-1-11-22-1024x640.jpg

SONATA toka hukohuko Korea.. Magari haya waliuziwa maofisa wa jeshi. Leo ukiiona Sonata Piga nayo picha.

Miaka ya 2000 tukaingizwa mkenge tena serikalini na serikali ya South tukaagiza Nissan Pickups (hardbody) kwa fujo sana kwenye vitengo vya serikali. Kama kuna magari yaliliingizia taifa hasara ni hayo. Baadae zikaja pickup NAVARA bei ghali kweli kweli lakini ni Mulemule.

Kuna Nissan SERENA😭nililiuza 1.5M, kuna Juke macho ya panzi, NISSAN Sunny ]

GHT.jpg
nknk.. Kwa kifupi NISSAN ni majanga

Serikali kuendelea kuruhusu kuagiza hizi gari ni uharamia na uhujumu mkubwa wa uchumi. Kuagiza gari Unahitaji dola, kuagiza vipuri unahitaji dola! Kuagiza madawa gari likiungua na kusababisha majeruhi kunahitaji dola

Kwa majanga yote hayo kwanini yasipigwe marufuku!?
 
Ni kama mamlaka za ukaguzi na KUSIMAMIA UBORA wa vyombo vya moto vinavyoingizwa nchini zimeshindwa Kazi, ama kuna uzembe mahali ama rushwa
Kwa modeli za magari yanayoingia nchini kwasasa NISSAN DUALIS zinaongoza kwa kuwaka moto.. Hivi mamlaka halilioni hili tatizo? Ama kwa vile nyingi hazijasababisha maafa makubwa?
NISSAN anaongoza kwa model nyingi mbovu ukiachana na NISSAN safari, Nissan Caravan nk ..
Jiulize ni kwanini kwa asilimia 95 hakuna NISSAN (IT) Wenzetu wamegutuka nini?
Hili taifa halijaanza kuingizwa mikenge leo
Miaka ile ya 80 ccm ikanunua/ikapewa magari ya Korando kutoka Korea kusini nadhani... Zilikufa zote! Leo ukimuona mtu ana Korando hilo ni body tuu engine imeshawekwa ya Toyota
Hatukukoma tuu miaka ya tisini Mwanzoni Jeshi letu likapata magari ya SONATA toka hukohuko Korea.. Magari haya waliuziwa maofisa wa jeshi. Leo ukiiona Sonata Piga nayo picha
Miaka ya 2000 tukaingizwa mkenge tena serikalini na serikali ya South tukaagiza Nissan Pickups (hardbody) kwa fujo sana kwenye vitengo vya serikali.. Kama kuna magari yaliliingizia taifa hasara ni hayo
Baadae zikaja pickup NAVARA bei ghali kweli kweli lakini ni Mulemule
Kuna Nissan SERENA😭nililiuza 1.5M, kuna Juke macho ya panzi, NISSAN SunnyView attachment 3088295 nknk.. Kwa kifupi NISSAN ni majanga
Serikali kuendelea kuruhusu kuagiza hizi gari ni uharamia na uhujumu mkubwa wa uchumi. Kuagiza gari Unahitaji dola, kuagiza vipuri unahitaji dola! Kuagiza madawa gari likiungua na kusababisha majeruhi kunahitaji dola
Kwa majanga yote hayo kwanini yasipigwe marufuku!?
Yaani mjapani atengeneze gari mwaka 2008 aitumie miaka 16 akuuzie leo wewe ukampelekee fundi maiko wa yombo dovya akatengeneze shoti kwa kuvuruga system ya umeme uje umlaumu mjapani kweli??
 
Mtani acha wapo wenye hizo dolari,
Juzi hapo nimeona nabii mmoja anaenda kwenye mashamba yake akitokea DSM kuelekea chalinze, gari yake na nyingine mbili za bode gadi zinamfuata.

Gari kama hiyo hapo.

Mtani hela ipo hasa huko kwa hao wa politiki na hao wanaojiita manabii.
 
View attachment 3088298
Yaani mjapani atengeneze gari mwaka 2008 aitumie miaka 16 akuuzie leo wewe ukampelekee fundi maiko wa yombo dovya akatengeneze shoti kwa kuvuruga system ya umeme uje umlaumu mjapani kweli??
Nyingi zimewaka moto na upya wake.. Lakini mbona kuna Toyota na Suzuki za miaka na miaka zinatengenezwa chini ya maembe bado zipo zinadunda?
 
View attachment 3088298

Nyingi zimewaka moto na upya wake.. Lakini mbona kuna Toyota na Suzuki za miaka na miaka zinatengenezwa chini ya maembe bado zipo zinadunda?
Sababu kubwa ya dualis kuwaka ni after market asilimia kubwa sana unakuta zimechezewa mifumo ya umeme kuweka redio za android au mataa ya kudamshi damshi hizi gari iko wazi hazitaki mbwembwe kama ni mpenda mbwembwe nunua tu Doyoda sasa tukiachana na dualis kuna hizi mazda CX5 nazo ni gari mbovu kishenzi
 
Hili taifa halijaanza kuingizwa mikenge leo Miaka ile ya 80 CCM ikanunua/ikapewa magari ya Korando SsangYong
ssangyong-korando-i-k4_thumb.jpg
kutoka Korea kusini nadhani... Zilikufa zote! Leo ukimuona mtu ana Korando hilo ni body tuu engine imeshawekwa ya Toyota
Unanikumbusha enzi za SsangYong Musso gari zilipambwa sana kumbe mibovu hatari
 
Shida sio Nissan, tatizo ni uwezo wetu mdogo katika maintenance ya vyombo vya moto hasa mafundi. Ni kweli kuna cases kadhaa kwa Nissan ku-malfunction na units kadhaa kurudishwa kiwandani, ila matatizo hayo hata kwa baadhi ya models za toyota yalishatokea.

Kuna ndinga hazitaki mbwembwe, mbona nasikia hata BMW haitaki mbwembwe.
 
View attachment 3088298

Nyingi zimewaka moto na upya wake.. Lakini mbona kuna Toyota na Suzuki za miaka na miaka zinatengenezwa chini ya maembe bado zipo zinadunda?
Hiki unachokisema ndugu Mshana jr nilikuwa nakisikia tu, hadi siku nilioshuhudia kwa macho yangu maeneo ya mbezi kituo cha shule, Dualis imelipuka moto wananzengo wanahangaika na maji huku mmiliki akiwa ameweka mikono kichwani kwa hofu ya kunusurika kifo na hasara.
 
Shida sio Nissan, tatizo ni uwezo wetu mdogo katika maintenance ya vyombo vya moto hasa mafundi. Ni kweli kuna cases kadhaa kwa Nissan ku-malfunction na units kadhaa kurudishwa kiwandani, ila matatizo hayo hata kwa baadhi ya models za toyota yalishatokea.

Kuna ndinga hazitaki mbwembwe, mbona nasikia hata BMW haitaki mbwembwe.
Mkuu hizi Dualis zimezidi
 
Mtani acha wapo wenye hizo dolari,
Juzi hapo nimeona nabii mmoja anaenda kwenye mashamba yake akitokea DSM kuelekea chalinze, gari yake na nyingine mbili za bode gadi zinamfuata.

Gari kama hiyo hapo.

Mtani hela ipo hasa huko kwa hao wa politiki na hao wanaojiita manabii.
Nabii analindwa na body guard? Bila Shaka Ni yule nabii mzinzi aliyeasi mtani wa watu wa Tabora.
 
Mshana Jr umesahau na jeshi la polisi waliingizwa chaka kununua Hyundai Saloon za polisi vilijifia mapema sana vile vigari
Si ndio hizi Sonata!?😀View attachment 3088302
Shida sio Nissan, tatizo ni uwezo wetu mdogo katika maintenance ya vyombo vya moto hasa mafundi. Ni kweli kuna cases kadhaa kwa Nissan ku-malfunction na units kadhaa kurudishwa kiwandani, ila matatizo hayo hata kwa baadhi ya models za toyota yalishatokea.

Kuna ndinga hazitaki mbwembwe, mbona nasikia hata BMW haitaki mbwembwe.
Mnyama BM mpaka umpindue ama alipuke tu mwenyewe ujue umefanya Kazi kubwa mno.. Lakini DUALIS chap kwa haraka kama kumsukuma tena🤣
 
Back
Top Bottom