Nissan Dualis zitajiondoa zenyewe sokoni

Nissan Dualis zitajiondoa zenyewe sokoni

Je, unamaanisha magari ya Nissan Dualis yatakoma kutengenezwa na kusambazwa?

Ikiwa ndio maana yako, basi ni muhimu kuelewa kwamba mzunguko wa maisha wa magari ni wa kawaida
Mfano mzuri huu hapa

Makampuni ya magari huacha. kutengeneza magari fulani kwa sababu kadhaa, ikijumuisha:


Mabadiliko ya teknolojia: Magari ya kizazi kipya yenye teknolojia bora zaidi huletwa, na hivyo kufanya magari ya zamani yasionekane kuvutia kwa wateja.
Mfano huu hapa
Mabadiliko ya mahitaji ya soko: Ikiwa mahitaji ya aina fulani ya gari yanapungua, kampuni inaweza kuamua kuacha kuitengeneza.
Sababu za kiuchumi: Sababu kama vile gharama za uzalishaji zinazoongezeka, ushindani mkali, au mabadiliko ya sera za serikali zinaweza kusababisha kampuni kuacha kutengeneza magari fulani.
Cheki hapa

Kwa sasa, hakuna tangazo rasmi kutoka kwa Nissan kuhusu kuacha kutengeneza Nissan Dualis. Hata hivyo, kama ilivyoelezwa hapo juu, ni jambo la kawaida kwa magari kuacha kutengenezwa baada ya muda.
Ikiwa unapanga kununua Nissan Dualis, ninakushauri ufanye utafiti wa kina zaidi. Zungumza na wafanyabiashara wa Nissan, soma maoni ya wateja wengine, na uchunguze mifano mingine inayofanana ili kufanya uamuzi bora.
Kwa msaada zaid angalia hapa
 
Nimeiona mahali hii!
 

Attachments

  • NISSNA DUALIS.jpg
    NISSNA DUALIS.jpg
    95.2 KB · Views: 13
Ngoja nisiongee maneno mengi,kuna mdada mmoja siku hizi hapa kazini hata salamu hanipi tokea anunue Dualis yake namba E,halafu naona pia speed yake ya kutembea kama imeongezeka ghafla,kawa kama vile mdada wa kizungu step za harakaharaka...
 
Tunashukiru kwa ajira zinazotolewa na hizo mamlaka za ukaguzi. Hivi unakagua kitu ambacho hata spare moja huwezi kutengeneza si ubabaishaji tu. HIzo mamlaka hazina tofauti na takukuru. Anyway wako bize na ishu za uchaguzi labda tusubirie majibu 2026
 
kitu nilichojifunza ukitaka kununua gari usiende kichwa kichwa nenda na watu wenye uzoefu wa magari.
Siku nakwenda kununua gari kuna yard nilikuta wanauza Nissan xtrail bei che sana kulingana na hela niliyokuwa nayo.Ilikuwa milioni 14 na yule mpakistani alinilazimisha sana.Mtaalamu wangu akaniambia mzee twende tukaangalie kwingine.
Tukakuta gari aina ya Subaru Forester bei milioni 12 ubahili wangu nikataka kuchukua yule jamaa akaniambie mzee kwa umri wako wewe unakaribia kustaafu halafu hili ni gari la vijana wewe unataka kukimbia kwa speed unataka kushindana na nani nikamsikiliza.
Hapo hapo kwenye yard nikakuta kitu RAV 4 kimetulia mke wangu ni mchaga akasema baba naniliu hapa sitoki chukua huu mzigo nitakuongezea 1m nikaichukua kwa milioni 17.5M hadi leo sijutii uamuazi wangu nilijifunza kitu kikubwa mno.Hiyo ilikuwa mwaka 2018.Baadae yule dereva akaniambia kuhusu ule uamuzi wa Nissan XTRAIL akaniambia hii gari ni too much electronics itakusumbua mzee zaidi ya yote Nissan vipuri vyake ni bei ghali.

Mara ya pili nikataka kununua pickup ajili ya shughuli za nyumbani sio biashara nikaenda na yule yule jamaa yangu ambaye ni dereva wa masafa marefu.Nikaona gari jamii ya kirikuu na ingine ACE ubahili wangu nikataka kuchukua.Ilikuwa mil 12 yule jamaa yangu sijui alijua niko njema nikamuona amechagua Toyota Hilux pick up sio double cabin kwa mbele na alianza kuikagua na kuiosha kabisa nilienda pembeni nikasali kwanza kumuomba mungu.Baade nikakata ushauri kuichukua ilikuwa ni 27.5m.
Nadiriki kusema hadi leo sijutii uamuzi niliochukua kwa ushauri wake.Siku moja akaniambia na mke wangu mngechukua ile kirikuu ajili ya kubania hela mngegombana na shemeji na matengenezo mngekuta ile hela mliyobania imefikia hii hiyo ilikuwa ni mwaka 2020.

Idea yangu ni 1.Ukiwa una uwezo flani usinunue kitu sababu ni bei rahisi kuna sababu shtuka 2.Usiende kichwa kichwa kununua kitu hasa gari bila kutaka ushauri kwa wabobezi.3.Uzuri wa nje wa gari usikubabaishe hata hizi Dualis mfano picha chini utaona ni nzuri sana.Hebu wewe jiulize shtuka gari la Nissan Dualis ni zuri sana kwa nje kuliko Hummer kwa nini hammer ie bei ya kutisha wakati ni kama litrekta.Usemi mmoja unasema uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti ndio unakuja hapa.

Jiulizeni yale magari yaliitwa MUSO Ssangyong,Hyundai,Koranda,Maruti,Mahendra yako wapo sasa hivi.

Msimpuuze mshanaJR ana hoja ya kusikilizwa hutaki fanya uwezavyo.Wengine humu wana mpinga hata baskeli hawana japo uwezo wa kuwa na gari wanao wanaongea kisiasa
 

Attachments

  • Screenshot 2024-09-06 090320.png
    Screenshot 2024-09-06 090320.png
    267.4 KB · Views: 15

Inasemekana baadhi ya BM tatizo ni chassis
Ila hakuna mifano hai kama jiko la gesi
Mwaka 95 serikali ilipigwana kitu kuzito ilipinunua Beijing Jeep kwa ajili ya uchaguzi.
Hawakuishia hapo, Mahita alipoingia madarakani wakakolpa Hyundai kwa ajili ya polisi, ndani ya miaka miwili hazikuonekana barabarani.
Kuna kipindi tukinunua engine za treni kutoka India miaka Ile Mshana Jr ulikua fomfoo, ikibidi zifungwe mbili ili ziweze kuhimili mzigo.
Bado hatukomi tu.
Food for thought: Mbona sioni gari ndogo za kichina kwenye barabara zetu?
Mjep bado kalikamata Soko tena kwa mikono yote miwili na miguu mitatu😀😀
Food for thought: Mbona sioni gari ndogo za kichina kwenye barabara zetu?
Nataka ninunue Kigari cha kuanzia maisha, itakuwa gari yangu ya kwanza na kwa uchumi wa kawaida bei isizidi 10M

Iwe juu kidogo na cc isiwe kubwa
Natanguliza shukran
Terois Kid
Ngoja nisiongee maneno mengi,kuna mdada mmoja siku hizi hapa kazini hata salamu hanipi tokea anunue Dualis yake namba E,halafu naona pia speed yake ya kutembea kama imeongezeka ghafla,kawa kama vile mdada wa kizungu step za harakaharaka...
😂😂😂😂😂
View attachment 3088390
Vigofu zilikuwa ni hizi, Volkswagen Golf,Polisi ndio walikuwa wanazitumia ktk kazi zao. Sonata sio golf
Roho ya paka mafuta inanusa💪🏿
 
Back
Top Bottom