Nissan Dualis zitajiondoa zenyewe sokoni

Nissan Dualis zitajiondoa zenyewe sokoni

Yaani mjapani atengeneze gari mwaka 2008 aitumie miaka 16 akuuzie leo wewe ukampelekee fundi maiko wa yombo dovya akatengeneze shoti kwa kuvuruga system ya umeme uje umlaumu mjapani kweli??
Swali jepesi, mbona kuna toyota, bmw ya mjerumani, na nyingine nyingi zinatengenezwa na hawa mafundi uchwara na haziwaki moto?
 
Shida sio Nissan, tatizo ni uwezo wetu mdogo katika maintenance ya vyombo vya moto hasa mafundi. Ni kweli kuna cases kadhaa kwa Nissan ku-malfunction na units kadhaa kurudishwa kiwandani, ila matatizo hayo hata kwa baadhi ya models za toyota yalishatokea.

Kuna ndinga hazitaki mbwembwe, mbona nasikia hata BMW haitaki mbwembwe.
Hapo kwa BMW ngoja ninyamaze maana mpaka sasa ni majanga. Ila tatizo kubwa ni yale kutoka Singapore, ni majanga matupu.
Hatari.jpeg
 
Ni kama mamlaka za ukaguzi na KUSIMAMIA UBORA wa vyombo vya moto vinavyoingizwa nchini zimeshindwa Kazi, ama kuna uzembe mahali ama rushwa.

Kwa modeli za magari yanayoingia nchini kwasasa NISSAN DUALIS zinaongoza kwa kuwaka moto.. Hivi mamlaka halilioni hili tatizo? Ama kwa vile nyingi hazijasababisha maafa makubwa?

NISSAN anaongoza kwa model nyingi mbovu ukiachana na NISSAN safari, Nissan Caravan nk. Jiulize ni kwanini kwa asilimia 95 hakuna NISSAN (IT) Wenzetu wamegutuka nini?

Hili taifa halijaanza kuingizwa mikenge leo Miaka ile ya 80 CCM ikanunua/ikapewa magari ya Korando SsangYong View attachment 3088300 kutoka Korea kusini nadhani... Zilikufa zote! Leo ukimuona mtu ana Korando hilo ni body tuu engine imeshawekwa ya Toyota

Hatukukoma tuu miaka ya tisini Mwanzoni Jeshi letu likapata magari ya Hyundai

View attachment 3088301

SONATA toka hukohuko Korea.. Magari haya waliuziwa maofisa wa jeshi. Leo ukiiona Sonata Piga nayo picha.

Miaka ya 2000 tukaingizwa mkenge tena serikalini na serikali ya South tukaagiza Nissan Pickups (hardbody) kwa fujo sana kwenye vitengo vya serikali. Kama kuna magari yaliliingizia taifa hasara ni hayo. Baadae zikaja pickup NAVARA bei ghali kweli kweli lakini ni Mulemule.

Kuna Nissan SERENA😭nililiuza 1.5M, kuna Juke macho ya panzi, NISSAN Sunny ]

nknk.. Kwa kifupi NISSAN ni majanga

Serikali kuendelea kuruhusu kuagiza hizi gari ni uharamia na uhujumu mkubwa wa uchumi. Kuagiza gari Unahitaji dola, kuagiza vipuri unahitaji dola! Kuagiza madawa gari likiungua na kusababisha majeruhi kunahitaji dola

Kwa majanga yote hayo kwanini yasipigwe marufuku!?
Unasema nyingi zimeweka moto je mliagiza mpya je mmenunua kwa wakala wa nissani au used japan au singapore

Je zikifika mnaweka spair sahihi

La mwisho nunua gari jipya kwa nissani uke kulalamika watakuja jipya nissani wenyewe...... sasa umenunua magari ya kajamba nani beforwad unalalamika mkuu
 

Sawa taasisi ipi wana Scania?

Dualis a.k.a mtungi wa oryx
Moto
Unasema nyingi zimeweka moto je mliagiza mpya je mmenunua kwa wakala wa nissani au used japan au singapore

Je zikifika mnaweka spair sahihi

La mwisho nunua gari jipya kwa nissani uke kulalamika watakuja jipya nissani wenyewe...... sasa umenunua magari ya kajamba nani beforwad unalalamika mkuu
Sanahani sijawahi kumiliki au kununua au kutumia gari inaitwa NISSAN DUALIS.. Ila mimi ni mdau kwenye hiyo sekta na nilichoandika ndio uhalisia kwa ground
Ishu ya kununua mpya au used sheria ya nchi yetu imeruhusu kwa masharti ya gari kufanyiwa ukaguzi
Nadhani umechangia kwa kusoma heading na si maudhui
 
Swali kwako, mbona tunanunua used na limetembea km lak 2 halikuungua? kama tatizo ni kuungua kwanini lisingeungua huko huko
Tumia akili kiduchu, bongo asilimia kubwa tunatumia used, kina dualis, patrol, ist, outlander, alphard na ndugu zao wengine, wote wametoka japan hawajaungua, lakini kuja bongo mmoja anaungua, na ukizingatia mafundi wa dualis ndio wa alphard,probox ndio wa patrol na gari nyinginezo..
 
Back
Top Bottom