Ni hatua nzuri kwa NIT kuzindua school of Aviation, ila uongozi uwe madhubuti haswa maana kwenye school of driving vyeti feki vingi sana viko mitaani na ajali bado zinaendelea, chonde chonde yasije tokea na huko maana itakuwa MAJANGA.
Mkuu wangu
Lily Flower,
Umeongea pwenti ya maana sana.
Umenikumbusha "legend story" moja ya pale Jnia, ambapo kuna kijana muosha ndege aliyefanikiwa kujifunza vitu vyote vya ndege kwa maana ya urubani, kupitia kuona tu, na kugusagusa.
Na kwa bahati nzuri alishapata kuruka na marubani mara kadha. Baadhi yetu wanajua kuwa ukikaa siti ya co-pilot na kama unaelewana na pilot huwa anaweza kukuachia control gear ya ndege uiongoze.
Kijana huyu alishafanya hivyo mara nyingi na kumudu.
Pia kwa utundu alijua radio telephony na communications kwa hatua zote za kuanzia start-up request, taxiing request na system checklist procedure. Kwa ufupi alikuwa 'rubani-pori'.
Siku moja rubani wa ndege yao alikuwa likizo, na kukatokea hitaji kubwa la usafiri wa ndege kwenda Zanzibar!
Kijana akachanganya na zake fasta, akaamua kuchukua tenda ya vichwa full on board, akachuna nauli, akapiga ndege moto na kuomba clearance na flight level kama kawa, akawa granted.
Sekunde kasoro ngoma ikaenda Airborne, akaruka low-level ili asionwe na radar hadi Zanzibar, akatua vizuri sana na kudisembark abiria.
Fasta kama kipanga akapiga turn-around ya haraka ili asistukiwe, na ngoma ikawa en-route back to Dar airport.
Akatua na kupaki vizuri.
Yaliyompata baada ya ishu hiyo kubumbuluka mnaweza kuyahisi, kwani hamjui kuwa hata msafara wa JK unaingiliwa na walinzi feki?...na je nini kinawapata?
NIT, jueni kwamba fani hiyo haitaki vihiyo wala sound.
Unqualified Licence in this field is simply a DEATH LICENCE!