NIT yazindua rasmi School of Aviation Techology.

NIT yazindua rasmi School of Aviation Techology.

Jana waliinzindua rasmi. Nafikiri watatoa utaratibu muda si mrefu. Nilizo pata juu juu, ni kwamba watakua wanahitaji C tano ( Grade C 5) na awe ana Diploma ya Automobile au Mechanical, hili niliambiwa na mtu mmoja wa pale ila sio official. Paka sasa ivi wana ndege moja ya kufundishia.

Imeanza lini,qualifications za kujiunga ni zipi?
 
Ni hatua nzuri sana kwj kuanzia, na nawapongeza sana Menejimenti ya NIT kwa wazo la kisasa na lenye uhitaji mkubwa sana kwa Tanzania ya leo.

Kwa ufupi uhitaji wa marubani wazalendo, kwa maana ya Weusi, ni wa juu sana hapa Tanzania, nadhani tunazidiwa kwa kiasi kikubwa na Kenya na Uganda.
Ni jambo la kusikitisha sana kwamba ndege za Mashirika ya Serekali na za makampuni binafsi nyingi hapa Bongo zinarushwa na Weupe kwa maana ya Wazungu.
Inashangaza kidogo unapokuta marubani Wazungu wanarusha PW!
Kwa tathmini yangu binafsi, ningeambiwa nikadirie mlinganyo kati ya marubani weupe na weusi hapa bongo ningeweka ratio ya 10:2.
Huu mlinganyo unatisha sana kwa mtu anayethamini nchi yake na anayejua kuwa kiakili hatuna tofauti kubwa na weupe.

Historia ya Eneo la Afrika Mashariki inasema kuwa enzi za Afrika Mashariki ile ya mwanzo kulikuwa na chuo cha marubani kule Soroti Uganda kilichokuwa kinamilikiwa na shirikisho hilo.
Chuo hicho kilizalisha marubani wengi sana ambao hadi leo wapo wengi tu wakiendelea kutumika, japokuwa kipindi hicho wengi wao kama si wote walikuwa ni marubani maalum kwaajili ya majeshi yetu ya Ulinzi na Ndege za serikali.

Hata ukirudi nyuma miaka kama 10 tu iliyopita utakutana na idadi kubwa ya marubani weusi ambao ni product ya Soroti, na ambao walishastaafu huko majeshini, sasa wakawa wanamalizia maisha yao kwny ndege za binafsi.

Miaka ya kuanzia 2000 ndipo tumeanza kuona ongezeko la marubani weusi hasa baada ya kufunguliwa kwa milango ya mahusiano ya kibiashara na teknoloji duniani, au kwa kifupi Utandawazi.

Kwa sasa ukitazama rika la marubani weusi utaona kuwa asilimia kubwa ni wa kizazi fulani cha kati, au vijana, hii ikionyesha kuwa walipata fursa ya kupata shule hiyo katika enzi za Year 2K!

Katika kipindi chote hicho Marubani weupe wametesa sana humu nchini, na walionekana kuwa wao ndio weledi wa kazi hiyo kuliko binadamu weusi.
Ilifikia wakati Waziri mmoja wa nchini Kenya wa enzi za Mzee Kenyatta alitoa kauli kuwa "SIWEZI KUPANDA NDEGE INAYORUSHWA NA RUBANI MWEUSI"...!

Sasa basi, nia yangu kutoa uchambuzi huo mfupi ilikuwa ni kuonyesha safari ya profession hii kwa hapa Tanzania, lakini zaidi kuwapongeza kwa mara ingine NIT kwa kuja na wazo hili jipya la kozi za urubani.

Tunategemea kwa kuanzishwa kwa elimu hii hapo chuoni bei za kozi hii zitakuwa nafuu, tofauti na sasa ambapo ili kupata leseni ya PPL, rubani mwanafunzi anatakiwa kuwa na salio si chini ya milioni 50!

Kwa maana hiyo kwa masikini kusoma urubani ilikuwa kama kitendo cha kwenda kwenye sayari ingine!

Hata ukiwatazama hawa mapilot wengi wa kizazi cha dot.com utakuta kuwa historia yao inaonyesha kuwa ni watoto wa wenye vijisenti.

Well, kuna exceptional case ya pilots na engineers wa ndege waliosomeshwa kwa hisani ya Tcaa au CATC, ambapo walikuwa na programu ya kuchukua wanafunzi wenye perfomance nzuri kutoka DIT na kuwapeleka Afrika kusini au ethiopia kusomea fani hizo.
 
MPaka sasa ivi wana ndege moja ya kufundishia.
Kimsingi hili lingekuwa swali langu kwa mleta mada au yeyote aliyefuatilia habari hizi.

Chuo chochote, mbali ya kuwa na madarasa maalum yenye simulators za kurusha ndege, ni lazima mwisho wa siku kiwe na ndege kwaajili ya field work, ambapo bila hivyo kinakuwa cha kufundisha UKIHIYO!
Ninachojiuliza hadi sasa NIT wamewezaje ku'acquire ndege hiyo ya mazoezi.
 
Ni hatua nzuri kwa NIT kuzindua school of Aviation, ila uongozi uwe madhubuti haswa maana kwenye school of driving vyeti feki vingi sana viko mitaani na ajali bado zinaendelea, chonde chonde yasije tokea na huko maana itakuwa MAJANGA.
 
Hii ndege wapewa msaada.
Na ndio itayo tumika kufundishia wanafunzi, Pia wapo kwenye mazungumzo na jwtz kupitia kituo chao cha mafunzo, ili pia waweze kutoa kozi za uhandisi wa ndege.
Chuo kina mpango mzuri katika hili swala sijaona porojo.. Ingawa kuna mapungufu kidogo yatakuwepo amabayo yanaweza kurekebishwa hapo mbeleni.

Kimsingi hili lingekuwa swali langu kwa mleta mada au yeyote aliyefuatilia habari hizi.

Chuo chochote, mbali ya kuwa na madarasa maalum yenye simulators za kurusha ndege, ni lazima mwisho wa siku kiwe na ndege kwaajili ya field work, ambapo bila hivyo kinakuwa cha kufundisha UKIHIYO!
Ninachojiuliza hadi sasa NIT wamewezaje ku'acquire ndege hiyo ya mazoezi.
 
Hili la vyeti feki, sasa ivi limekua tatizo sugu kwakweli. Hivi vyeti vinatengenezwa sana hasa kwenye ma stationary.
Kwa PPL itakua ngumu sana.

Ni hatua nzuri kwa NIT kuzindua school of Aviation, ila uongozi uwe madhubuti haswa maana kwenye school of driving vyeti feki vingi sana viko mitaani na ajali bado zinaendelea, chonde chonde yasije tokea na huko maana itakuwa MAJANGA.
 
Itakuwa vizuri sana imeanza lini
Wamesema wamezindua jana.

Kikubwa ninachokiona mimi hapo ni kuwa upande wa Elimu ya theory wataipata, tena nzuri sana. Kuna walimu wengi sana wazuri pale CATC ambao naamini watawatumia kama hawajapeleka wa kwao kwenye training.
Ila wanapaswa kuongeza ndege ya pili ya mazoezi, maana hiyo moja haitakidhi. Najua itakuwa ni single engine, ambapo wanapaswa pia kuwa na twin engine ili kutoa marubani wa kiwango, pia kama hiyo moja ikipata snag hapatakuwa na kusimamisha madarasa ya field.

Tatizo linalovishinda vyuo vingi binafsi ni running costs za hizo ndege. Kuwa na ndege na kufanikiwa kui'sustain ni field inayojitegemea kabisa, na zaidi wanafanikiwa waliojikita kwenye biashara hiyo.
Inataka umakini wa hali ya juu kusustain ndege ya kufundishia wanafunzi parse!,vinginevyo ndani ya mwaka mmoja itakuwa grounded pale Jnia, huku ikiwa na madeni ya dola lukuki.
 
Ni hatua nzuri na inahitaji pongezi, nafkiri chuo pia kikingia ubia na JWTZ itasaidia sana, manaake wale jamaa wapo vzuri
 
Aero - Lease Investment ndio iliyo wapatia NIT ndege kwa ajili ya mafunzo ya marubani kwa ngazi ya PPL.

Pia wanashilikiana na TGFA ili kukamilisha utaratibu wa kufundisha marubani walio na leseni za PPL kuweza kusoma mpaka CPL.

Wamesema wamezindua jana.

Kikubwa ninachokiona mimi hapo ni kuwa upande wa Elimu ya theory wataipata, tena nzuri sana. Kuna walimu wengi sana wazuri pale CATC ambao naamini watawatumia kama hawajapeleka wa kwao kwenye training.
Ila wanapaswa kuongeza ndege ya pili ya mazoezi, maana hiyo moja haitakidhi. Najua itakuwa ni single engine, ambapo wanapaswa pia kuwa na twin engine ili kutoa marubani wa kiwango, pia kama hiyo moja ikipata snag hapatakuwa na kusimamisha madarasa ya field.

Tatizo linalovishinda vyuo vingi binafsi ni running costs za hizo ndege. Kuwa na ndege na kufanikiwa kui'sustain ni field inayojitegemea kabisa, na zaidi wanafanikiwa waliojikita kwenye biashara hiyo.
Inataka umakini wa hali ya juu kusustain ndege ya kufundishia wanafunzi parse!,vinginevyo ndani ya mwaka mmoja itakuwa grounded pale Jnia, huku ikiwa na madeni ya dola lukuki.
 
Ni hatua nzuri kwa NIT kuzindua school of Aviation, ila uongozi uwe madhubuti haswa maana kwenye school of driving vyeti feki vingi sana viko mitaani na ajali bado zinaendelea, chonde chonde yasije tokea na huko maana itakuwa MAJANGA.
Mkuu wangu Lily Flower,
Umeongea pwenti ya maana sana.
Umenikumbusha "legend story" moja ya pale Jnia, ambapo kuna kijana muosha ndege aliyefanikiwa kujifunza vitu vyote vya ndege kwa maana ya urubani, kupitia kuona tu, na kugusagusa.

Na kwa bahati nzuri alishapata kuruka na marubani mara kadha. Baadhi yetu wanajua kuwa ukikaa siti ya co-pilot na kama unaelewana na pilot huwa anaweza kukuachia control gear ya ndege uiongoze.
Kijana huyu alishafanya hivyo mara nyingi na kumudu.
Pia kwa utundu alijua radio telephony na communications kwa hatua zote za kuanzia start-up request, taxiing request na system checklist procedure. Kwa ufupi alikuwa 'rubani-pori'.

Siku moja rubani wa ndege yao alikuwa likizo, na kukatokea hitaji kubwa la usafiri wa ndege kwenda Zanzibar!
Kijana akachanganya na zake fasta, akaamua kuchukua tenda ya vichwa full on board, akachuna nauli, akapiga ndege moto na kuomba clearance na flight level kama kawa, akawa granted.
Sekunde kasoro ngoma ikaenda Airborne, akaruka low-level ili asionwe na radar hadi Zanzibar, akatua vizuri sana na kudisembark abiria.
Fasta kama kipanga akapiga turn-around ya haraka ili asistukiwe, na ngoma ikawa en-route back to Dar airport.
Akatua na kupaki vizuri.

Yaliyompata baada ya ishu hiyo kubumbuluka mnaweza kuyahisi, kwani hamjui kuwa hata msafara wa JK unaingiliwa na walinzi feki?...na je nini kinawapata?

NIT, jueni kwamba fani hiyo haitaki vihiyo wala sound.
Unqualified Licence in this field is simply a DEATH LICENCE!
 
Last edited by a moderator:
Aero - Lease Investment ndio iliyo wapatia NIT ndege kwa ajili ya mafunzo ya marubani kwa ngazi ya PPL.

Pia wanashilikiana na TGFA ili kukamilisha utaratibu wa kufundisha marubani walio na leseni za PPL kuweza kusoma mpaka CPL.
Inatia moyo!
Ukitembelea shule yoyote ya kindergatten na ukauliza watoto...when you grow up, whom do you want to be, watakujibu PILOT!...huenda ndoto za watoto wetu zikatimia endapo bei za chuo hiki zitakuwa za kizalendo.

Nimefurahi kusikia kuwa TGFA wataingia kama wabia, jambo ambalo linatoa mwanga zaidi wa professionalism kwenye fani hii kupitia NIT.
Jamaa hawa wako vizuri sana kwenye fani, na wanatembea kwa viwango, labda huenda ni kwavile bajeti yao inatoka kulikoungua shoka!

Hii kampuni ya Aero-Lease ni ya watu gani?
 
Ni kweli, hata mimi nilikua nilikua napenda sana enzi za utotoni kua Pilot.

katika vyuo vyenye gharama ndogo hapa Tanzania NIT ni kimoja wapo, Pia tuombe na kwa kozi hii pia iwe ni nafuu.

Hawa Aero - Lease Investment sijajua ni watu gani bado. Ila ndio walio wafadhili wa ndege hiyo.

Back
Top Bottom