Kwani Zanzibar ndio mara ya kwanza kuifunga taifa stars. Kama unakumbuka kipindi cha maximo pia ilikiwa sawa na juzi tu. Mpira wetu sie upo kwenye magazeti tu. Nenda kaangalie wazenji wanavyoandaa watoto kuja kucheza mpira. Kuna ligi za watoto zinasimamiwa na ZFA kuanzia watoto wa miaka 12 wanacheza juvenile league, junior league na central league.
Hivi ndio viwanda vyao kila siku utaona vipaji vipya ndio mazao ayo ya kina agry, kanavaro, sabri china, baby wapo wengi tu. Huku sie kelele magazetini tu. Kwa kumalizia ndio maana wazenji wanadai nchi yao kwa sababu ya kuwanyanyasa na kuwadharau tu. Na iko siku hawa jamaa tutawatafuta ngoja wapate nchi yao utakuja kukumbuka haya maandishi.