Nitaijua vipi nyota yangu kwa jina langu na mama?

yassn

New Member
Joined
Jul 15, 2017
Posts
3
Reaction score
5
Niliwahi kusikia kuwa njia rahisi ya kutambua nyota ni herufi ya mwanzo ya jina na Tarehe ya kuzaliwa..

Herufi ya jina ni nyota nyingine na tarehe ya kuzaliwa ni nyota nyingine..

Hapo ipi nzuri kuifuata.?? Kwasababu tabia ni kama haziendani..

Nilisikia kuna njia ya kutumia jina langu na jina la mama. Je hesabu zake zinakuwaje.?
Msaada tafadhali..
 
Njia za kujuwa nyota yako Njia ya kwanza ni jina lako herufi yako ya mwanzo ndipo utajuwa nyota yako kwa kutumia herufi ya mwanzo wa jina lako. Njia ya pili ya Kwa Kujuwa nyota yako unachukuwa Tarehe yako ya kuzaliwa na mwezi uliozaliwa ndipo utakapoweza kujuwa nyota yako ni ipi? Na Njia ya 3 Njia ya mwisho kujuwa nyota yako kwa kuchukuwa jina lako na jina la mama yako kwa idadi ya herufi za Abjadi unajumlisha herufi za jina lako na jina la mama yako.Kisha una gawa kwa 12%12 itakayobaki ndio itakuwani nyota yako. Kwa Mfano imebaki namba 1: nyota yako ni nyota punda ikibaki namba 2: nyota yako ni nyota ng'ombe ikibaki namba 3: nyota yako ni nyota ya mapacha. Ikibaki namba 4: nyota yako ni nyota ya kaa. Ikibaki namba 5: nyota yako ni nyota ya Simba.Ikibaki namba 6: nyota yako ni nyota ya mashuke ikibaki namba 7: nyota yako ni nyota ya mizani ikibaki namba 8: nyota yako ni nyota ya nge. Ikibaki namba 9: nyota yako ni nyota ya Mshale .Ikibaki namba 10: nyota yako ni nyota mbuzi. Ikibaki namba 11: nyota yako ni nyota ndoo. Na ikibaki namba 12: nyota yako ni nyota ya Samaki. Jifunze kusoma Herufi za Abdjadi kwa kuangalia Video hapo chini.


Your browser is not able to display this video.
 
Amakweli haitokaa itokee wajinga wakaisha....😂😂😂
Huu ni upuuzi tu kama upuuzi mwingine.
 
Mambo ya nyota na mienendo yake hayafungamani hata kwa udogo wa kucha inayokatwa na maisha binadamu. Ni nadharia zitakazokuingiza kwenye utumwa.
 
Mambo ya nyota na mienendo yake hayafungamani hata kwa udogo wa kucha inayokatwa na maisha binadamu. Ni nadharia zitakazokuingiza kwenye utumwa.
Wewe kama huamini ipotezee mbali hii Thread na wala usijishughulishe ukapoteza muda wako. Kulikuwa hakuna haja ya wewe ku Comment hapa. Unapoteza muda wako kwa mambo ya kipuuzi mkuu? Tuache sisi na nyota zetu wewe shughulika na dunia yako unaonaje ushauri wangu juu yako?
 
Elimu ya falaki ambayo kwa Kiingereza ni Astronomy. Pia ina matawi yake mengine kama vile Astrophysics (Fizikia ya umbile za Falaki), Astrometry (Fizikia ya Mienendo na Miale ya Sayari); Cosmology (Elimu ya asili na maumbile ya Anga la juu) n.k

Mingoni mwake Elimu ya Utabiri wa hali ya hewa inaptikana ambayo ni elimu ya maumbile ya Ulimwengu na dunia yetu nyota (mfano Jua), Mwezi, Sayari, Mbingu. Elimu hii inayoelezea na kuchambua maumbile ya vitu hivi ikijumuisha mienendo yake, tabia zake na mahusiano yake n.k

Ninyi hii elimu ya falaki mnaitumuia mnaitumia kwa kufananisha mienendo ya anga ya juu na bunadamu imma kwa kufungamanisha na mwezi aliozaliwa au herufi yake ya awali ya jina n.k

Upuuzi ni upumbao! Unachoshughulika nacho si upumbao bali unajiangamiza wewe mwenyewe kimwili na kiroho.
Sayari haziathiri mwezi wa mtu aliozaliwa na mienendo yake haifungamani na asili ya binadamu kwa lolote. Elimu ya falaki ina manufaa lakini si katika hayo unayoyapigania.

Ameanza kwenye nyota yake! Atakuja kwenye nyota ya anayetaka kumuoa/aliyemuoa. Kama hajaoa mtampangia kuwa nyota yako haiendani na nyota yake. Ya kwake ni ni asili upepo na ya kwako ni asili ya moto. Mtampangia muda wa kuoa, siku na ramli nyingi.

Inaharibu mwili wa mtu na roho ya mtu. Sijagusia upande wa dini hapo!
 
Umeanza vizurii, umekuja kuteleza mwishoni.

Swali fikirishi, ilikuaje yule mzee marehemu alikua maarufu duniani. Akawa na ofisi miji mikubwa duniani hata kabla ya uhuru wa inchi yake Tanganyika.

Kua na ofisi London hasa kwa kipindi kile na ni mtu mweusi alafu akapewa wadhifa wa juu kama kiongozi wa elimu ya anga, kuna jambo zitooo.

Elimu pana sana ila nasikitika hutakuja kuona mtalaa kwenye chuo unafundisha. Mtaala tulio nao unazalisha watumwa endelevu kwa kivuli cha neno "sayansi".
 
Tuache na Elimu yetu ya falaki kama huipendi usi comment . Kwanini unasumbuka na sisi tunaye amini Elimu ya falaki? kinacho kuumiza roho ni kitu gani Mkuu? Ipuuze Elimu ya falaki kama kwako wewe haina faida hakuna ya haja ya wewe kuweka comment yako hapa. Usipoteze muda wako kwaku comment kitu cha kipuuzi hakina faida kwako Mkuu.
 
Siku zote mambo yaliyo juu ya ukawaida wa mazingira na mazingara ya binadamu imma yawe ya kweli au yawe ya kusadikika yanastajaabisha na yanavutia kwa wakati mmoja na ndicho kilichokuwa kwa huyo Mzee.

Yule mzee hakuwa na elimu ya astronomy hii ambayo ya kuchunguza maumbile asili ya anga na kutambua mienendo ya juu bali alikuwa na elimu ya unajimu (astrology).

Elimu hii ni elimu inayotaka kuhusiana au kuendana na elimu ya astronomy ila utofauti wake ni kuwa astrology inaelezea sana mwenendo wa viumbe hai kwa ujumla na inahusisha viumbe hai na anga. Ila elimu ya astronomy inaelezea elimu ya anga peke yake.

wanajimu wanaamini elimu ya anga ambayo ni nyota, sayari na mwezi zina uhusiano wa kitabia, kiasili, kimaumbile, kimaisha, kimali, kimaradhi, kitiba na kifo na kimajira ya sayari ya dunia na vilivyomo. Wanajimu wanaamini Mungu aliumba vitu na viumbe kimahesabu, mahesabu hayo yanakani inayoingiliana na mwenendo wa maisha ya viumbe hai alivyoviumba Mungu.

Kwa kuwa vilivyomo angani na magimba na sayari zilizokusanya na nyota kwa kuwa zinakwenda kimahesabu maalumu: Kwa hayo wanajimu wanaamini Mungu aliumba asili 4. Asili ya vilivyo na moto, udongo, upepo na maji. Wao wanaamini asili hizi nne(4) ziliweza kuzaa asili saba (7) na matawi yake mawili (2) ambayo Mungu aliumba mbingu saba (7), ardhi saba(7) kwa tabaka, bahari saba (7), mabara saba (7), sayari kubwa zipo saba(7): kwa hayo wanajimu wanaaamini vitu hivyo saba vinatokana na asili hizo nne.

Kwa hayo mahesabu wanaamini kwa dhati kabisa ya kwamba; Bahati, raha, shida, mafanikio, maradhi, kifo na maisha yote kwa ujumla yanayomwangukia binadamu qadar/dira/uongofu wake yanahusiana kwa dhati kabisa na mzunguko wa nyota, sayari na mwezi.

Wanajimu wanachokifanya ni ramli! Ni udanganyifu, ni utapeli. Hata huyo marehemu alishindwa kutabiri kifo chake, walau hata mahali atakapofia au siku pengine. Hayo yote alishindwa. Hiyo elimu inafika mbali kabisa inajihusisha na ushirikina. Kwa sababu marehemu miaka ya nyuma kabisa huko kabla ya kujikita rasmi kwenye hiyo elimu alikamatwa akiwa pamoja na mwalimu wake aliyemfundisha huo unajimu.

Mwalimu wake alimuaga anaondoka kwa kujigeuza umbile kuwa chura na kutoka ndani ya selo.
 
Kuna Sayari inaitwa "Alama simsima." Haihusiani na masuala ya mahesabu ya kiunajimu.

Allah subhanahu wataala baada ya kumuumba Adam A.S kutokana na udongo huo huo akaumba mtende. Kwa udongo huo huo uliobaki akaumba "Alama simsima".

Hii ni sayari! "Akrimuu ammatakumunakhla" Mtume S.A.W aliuita mtende kwa kuupa sifa ya ndugu wa binadamu. Hii sayari ni kubwa! Kuna watu wanaishi kama mimi na wewe na kuna njia ukiifanya unafika na kuingia kwenye sayari. Kuna Malaika pia.

Sijigambi ila najua usichokijua. Sikudharau wala sioni upuuzi. Ninachokiona ni kuwa unajiangamiza wewe mwenyewe na hicho si kitu kizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…