Umeanza vizurii, umekuja kuteleza mwishoni.
Swali fikirishi, ilikuaje yule mzee marehemu alikua maarufu duniani. Akawa na ofisi miji mikubwa duniani hata kabla ya uhuru wa inchi yake Tanganyika.
Kua na ofisi London hasa kwa kipindi kile na ni mtu mweusi alafu akapewa wadhifa wa juu kama kiongozi wa elimu ya anga, kuna jambo zitooo.
Elimu pana sana ila nasikitika hutakuja kuona mtalaa kwenye chuo unafundisha. Mtaala tulio nao unazalisha watumwa endelevu kwa kivuli cha neno "sayansi".
Siku zote mambo yaliyo juu ya ukawaida wa mazingira na mazingara ya binadamu imma yawe ya kweli au yawe ya kusadikika yanastajaabisha na yanavutia kwa wakati mmoja na ndicho kilichokuwa kwa huyo Mzee.
Yule mzee hakuwa na elimu ya astronomy hii ambayo ya kuchunguza maumbile asili ya anga na kutambua mienendo ya juu bali alikuwa na elimu ya unajimu (astrology).
Elimu hii ni elimu inayotaka kuhusiana au kuendana na elimu ya astronomy ila utofauti wake ni kuwa astrology inaelezea sana mwenendo wa viumbe hai kwa ujumla na inahusisha viumbe hai na anga. Ila elimu ya astronomy inaelezea elimu ya anga peke yake.
wanajimu wanaamini elimu ya anga ambayo ni nyota, sayari na mwezi zina uhusiano wa kitabia, kiasili, kimaumbile, kimaisha, kimali, kimaradhi, kitiba na kifo na kimajira ya sayari ya dunia na vilivyomo. Wanajimu wanaamini Mungu aliumba vitu na viumbe kimahesabu, mahesabu hayo yanakani inayoingiliana na mwenendo wa maisha ya viumbe hai alivyoviumba Mungu.
Kwa kuwa vilivyomo angani na magimba na sayari zilizokusanya na nyota kwa kuwa zinakwenda kimahesabu maalumu: Kwa hayo wanajimu wanaamini Mungu aliumba asili 4. Asili ya vilivyo na moto, udongo, upepo na maji. Wao wanaamini asili hizi nne(4) ziliweza kuzaa asili saba (7) na matawi yake mawili (2) ambayo Mungu aliumba mbingu saba (7), ardhi saba(7) kwa tabaka, bahari saba (7), mabara saba (7), sayari kubwa zipo saba(7): kwa hayo wanajimu wanaaamini vitu hivyo saba vinatokana na asili hizo nne.
Kwa hayo mahesabu wanaamini kwa dhati kabisa ya kwamba; Bahati, raha, shida, mafanikio, maradhi, kifo na maisha yote kwa ujumla yanayomwangukia binadamu qadar/dira/uongofu wake yanahusiana kwa dhati kabisa na mzunguko wa nyota, sayari na mwezi.
Wanajimu wanachokifanya ni ramli! Ni udanganyifu, ni utapeli. Hata huyo marehemu alishindwa kutabiri kifo chake, walau hata mahali atakapofia au siku pengine. Hayo yote alishindwa. Hiyo elimu inafika mbali kabisa inajihusisha na ushirikina. Kwa sababu marehemu miaka ya nyuma kabisa huko kabla ya kujikita rasmi kwenye hiyo elimu alikamatwa akiwa pamoja na mwalimu wake aliyemfundisha huo unajimu.
Mwalimu wake alimuaga anaondoka kwa kujigeuza umbile kuwa chura na kutoka ndani ya selo.