Nitaitoa CCM peke yangu tu, kwa njia mbadala

Nitaitoa CCM peke yangu tu, kwa njia mbadala

Kama unaweza kuitoa serikali iliyopo madarakani kwa maombi.

Kwanini huo muda na hizo nguvu za hayo maombi usitumie kutatua shida zako mwenyewe na hayo mateso unayopitia?

Nijibu.
 
Nimeamua kuachana kabisa na harakati za kisiasa kwa nia ya kuitoa CCM. Nimeamua kuachana na njia za kisiasa kama kupiga kura, maandamano ya amani na mikutano ya kisiasa kwa sababu CCM haiheshimu maamuzi ya wananchi wengi kwa njia ya kura,au sauti za walio wengi. CCM wameamua kutumia nguvu za Dola kubaki madarakani.

Sasa nimeamua Mimi peke yangu kutumia njia ya MAOMBI, Mimi peke yangu nitakua namuomba Mungu wa Ibrahimu Isaka na Yakobo
Aitoe CCM madarakani kwa aibu na fedheha kubwa.

Aanze kuwatoa VIONGOZi wa CCM mmoja kila baada ya mwingine kwa muda mfupi Sana bila kuleta madhara kwa Taifa.
Mimi sio mlokole, Wala mtakatifu, lakini Ni Binadamu.

Na Mungu anasikia kila neno litokalo kwa kiumbe wake. Hivyo kwa imani bila kushirikiana na Watanzania wengine mimi peke yangu tu naweza,kwani Mungu katoa nafasi hiyo ya mtu yeyote kuweza kuomba na kujibiwa.

Mungu atajibu tu. Mungu anaona mateso yetu.
Le mutuz akisoma ujumbe wako kwake itakuwa fursa kubwa kuvuna pesa za miccm kwa kisingizio cha kuwaazima waganga wa kienjeji apige pesa mda huu, wapo watanzania wengi wanaandamana mioyoni mwao kwa bidii hawajachoka kumlilia mungu na ipo siku atawajibu vilio vyao kwani kupora haki za wapiga kura ni Dhambi kubwa isiyo na msamaha kwa mungu
 
Ukishaitoa CCM madarakani unakileta chama gani icho cha Mungu muumba?
CCM ikifariki chama chochote kitaweza kuongoza Nchi kwani CCM yenye vilaza kama kabudi imewezaje kukaa ikulu kisha vyama vinginevyo vyenye watu wenye busara vishindwe?
 
Uyo mungu wako, kakuamuru uziheshimu mamlaka zinazo kuongoza.

Maana yake, Mungu kampa baraka zote Mh John Pombe, Magufuli kukuongoza.
Mungu yupi? Labda mungu wako binafsi na mungu wa kabudi na polepole siyo mungu wa watanzania wenye Akili timamu
 
Maskini kwa hiyo maombi ya akina Askofu Mwamakula,Askofu Bagonza na Shehe Ponda Mungu kayatupa kwenye dustibin yako ndiyo atayapokea?
Mungu yupi unamsemea? Mungu wa Gwajima aliyeshiriki kula kondoo wake? au mungu yupo?
 
Mungu ni wa haki.Ataangalia ni upande upi una haki.Unafikiri Mungu atakaa upande wa walioiba kura?
Ha haaa wanasiasa wote ni waongo , wanajijali wao tu. Mungu hana mpango nao ana mengine muhimu zaidi ya kufanya, sie tupambane tu
 
CCM ikifariki chama chochote kitaweza kuongoza Nchi kwani CCM yenye vilaza kama kabudi imewezaje kukaa ikulu kisha vyama vinginevyo vyenye watu wenye busara vishindwe?
Mfano labda wa chama kingine che Mungu chenye watu wa busara ni kipi icho tukijue?
 
Ha haaa wanasiasa wote ni waongo , wanajijali wao tu. Mungu hana mpango nao ana mengine muhimu zaidi ya kufanya, sie tupambane tu
Bahati mbaya kila kitu ni siasa.Hata wewe mpango wa kuweza kuwa hapa JF sasa hivi ni mchongo wa siasa!
 
CCM ikifariki chama chochote kitaweza kuongoza Nchi kwani CCM yenye vilaza kama kabudi imewezaje kukaa ikulu kisha vyama vinginevyo vyenye watu wenye busara vishindwe?
Nadhani prof Kabudi siyo kilaza, anajua anachotaka na analofanya
 
Kuna jamaa kila alipokuwa anataka kulala,alikuwa anamtukana magufuri kutokana na kutokutoa ajira,lakini baadae jamaa alipata ajira serikalini,nkahis magufuri kaogopa
 
MIMI NI CCM DAMU-----MIMI NI YANGA DAMU-----MIMI NI TANZANIA DAMU----MIMI NI TEAM MAGUFULI DAMU---- MIMI NASEMA KWA KAULI MOJA "MITANO TENA, KAZI IANZE"
Usije kujinyea takecare
 
Wewe mpagani tu hakuna wa kukusikiliza
Unatakiwa umuombe Mungu wako sio wa wenzio wa watu wengine.

Wewe unataka umuombe wa Mungu wa Ibrahim Yakobo na Isaka huna wako wewe

Wa kwako yuko wapi? Kafariki dunia au huna kabisa pagani wewe
Umewaona wafuasi wa mungu wa ccm mwenge Nyamrunda ?
 
Ungana na CUF nao Wana ajenda kama yako ya maombi huenda mkiongeza nguvu mnaweza kufanikiwa.
 
MIMI NI CCM DAMU-----MIMI NI YANGA DAMU-----MIMI NI TANZANIA DAMU----MIMI NI TEAM MAGUFULI DAMU---- MIMI NASEMA KWA KAULI MOJA "MITANO TENA, KAZI IANZE"
Kazi na iendelelee
 
Labda utaitoa ukiwa ndotoni, ila sio CCM ya Jiwe ambayo kigogo2014 amenyoosha mikono mwenyewe
[emoji23][emoji23][emoji23]Nmemuona kule twiter kapost mabawa ya ndege anasema anarudi ughaibuni haraka haraka baada ya kumzika babaake kwa kumuogopa jiwe!

Kumbe zile mbwembwe zote anafanya akiwa nje ya nchi huku akitudanganya hakuna wa kumpata,
 
Ina maana hata kura hakupiga [emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom