Nitajie Rais wa Africa aliyefanikiwa kudhibiti nchi kwa kuwa mlaini/mpole mpole (polite)

Nitajie Rais wa Africa aliyefanikiwa kudhibiti nchi kwa kuwa mlaini/mpole mpole (polite)

Nimekupa mfano wa Mauritius unaijua?...unge Google kwanza ...
Kweli nianze kugoogle taifa moja baada ya jingine na viongozi wake?
Ungeweka hapa wasifu wake itasaidia na wengine pia wenye kuhitaji majibu!

Huyo kiongozi alitumia mbinu gani?
Aliwezaje kudhibiti uhalifu wa kisiasa, kijamii nk? Aliwezaje kuwafanya walio chini kuwa waadilifu wakati wote? Aliwezaje kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma? Hilo taifa lina idadi gani ya watu? Wana kipato kipi?
Wanaendeshaje uchumi wao? Walianzia wapi?
 
Kwa sisi Waafrika, Viongozi bila kutumia Ubabe kiasi kwa kiasi fulani, hakuna kitakachofanyika kwa mafanikio makubwa.

Ni kwamba, Kiongozi atakuwa anajaza maji kwenye Tank, na wengine kwa wakati huo huo watakuwa watatoboa Tank hilo kwa lengo la kujinufaisha wao wenyewe tu.
 
Tunajua upole ni sifa ambayo kila mmoja anapaswa kuwa nayo pale inapostahili. Chochote kinachofanyika kinapaswa kuwa na kiasi.

Swali langu ni je, ni kiongozi gani wa nchi za kiafrika alieweza kudhibiti nchi kwa kuwa mpole?
Tuanze na Nyerere, Mandela. Kenyata nk. Je, walikuwa na haiba zipi ktk kudhibiti nchi kisiasa, kiuchumi, kijamii nk
Hatuhitaji mdhibiti nchi bali tunahitaji kiongozi anayeheshimu katiba, sheria na kanuni zote zinazoongoza nchi.
 
..tunatakiwa tuwe na katiba nzuri na sheria kali.

..pia asiwepo yeyote ambaye atakuwa juu ya sheria.

..ni makosa kumtegemea Raisi mkali atakayedhibiti nchi nzima.

..Wananchi kwa ujumla wanatakiwa wawe wanajua haki na wajibu wao.

..Pia wananchi wawe macho kulinda katiba na kutetea haki zao.
 
Tunajua upole ni sifa ambayo kila mmoja anapaswa kuwa nayo pale inapostahili. Chochote kinachofanyika kinapaswa kuwa na kiasi.

Swali langu ni je, ni kiongozi gani wa nchi za kiafrika alieweza kudhibiti nchi kwa kuwa mpole?
Tuanze na Nyerere, Mandela. Kenyata nk. Je, walikuwa na haiba zipi ktk kudhibiti nchi kisiasa, kiuchumi, kijamii nk
Kenyatta(Jomo) alitawala na aliidhibiti nchi bila ya kuwa dictator japo alipoingia Moi mambo yakabadilika, Mandela alikuwa mpole sana.
Nyerere alikuwa 'kaks' japo na busara za kiuongozi alikuwa nazo.
Uhuru Kenyatta hakutawala kiimla.
Jakaya hakutawala kiimla.
Idd Amin na Magu walitawala kiimla.
 
Ninachomaanisha hapo ni kuwa na msimamo na uwezo wa kupambana na mambo yasiyojenga taifa au yanayoliletea taifa hasara. Mfano kudhibiti rushwa, kuzuia mirija ya matumizi mabaya ya fedha za umma, kudhibiti mfumuko wa bei hata kama wafanyabiashara ni watu wake wa karibu, kulinda maadiki ya taifa nk.
Hatujawahi kupata kiongozi wa aina hiyo
Na unayetaka ionekane alikuwa hivyo hakuwa hivyo bali yeye alikuwa mtu mwenye roho ya kwanini na kila kitu alikifanya kwa utashi wake binafsi tu,
Kama kuanzisha miradi kwa kujiamulia tu nje ya utaratibu na matokeo yake kukawa na hisia za ufisadi lakini hakutaka mtu yeyote kuhoji
na aliyejaribu alishughulikiwa kisawasawa kwani alikuwa mbinafsi aliyejiona mjuwaji wa kila kitu,
Binafsi sikuwahi kumuona ni kiongozi mahiri zaidi ya chuki,dharau na uongo mwingi.
 
Tunajua upole ni sifa ambayo kila mmoja anapaswa kuwa nayo pale inapostahili. Chochote kinachofanyika kinapaswa kuwa na kiasi.

Swali langu ni je, ni kiongozi gani wa nchi za kiafrika alieweza kudhibiti nchi kwa kuwa mpole?
Tuanze na Nyerere, Mandela. Kenyata nk. Je, walikuwa na haiba zipi ktk kudhibiti nchi kisiasa, kiuchumi, kijamii nk
Kudhibiti ndio kufanya nini? Labda ungesema kuleta maendeleo ungeleeweka.

Kudhibiti ni kudhibiti nini sasa, kudhibiti mikutano ya siasa au?
 
Tunajua upole ni sifa ambayo kila mmoja anapaswa kuwa nayo pale inapostahili. Chochote kinachofanyika kinapaswa kuwa na kiasi.

Swali langu ni je, ni kiongozi gani wa nchi za kiafrika alieweza kudhibiti nchi kwa kuwa mpole?
Tuanze na Nyerere, Mandela. Kenyata nk. Je, walikuwa na haiba zipi ktk kudhibiti nchi kisiasa, kiuchumi, kijamii nk
Sheria zipo, katiba ipo, kuzifuata haihitaji upole wala ukali
Kufokafoka na kutoa mapovu ndio kudhibiti nchi?
 
Wewe nchi ni kubwa na ina watendaji wengi lazima wote wajue msimamo wako kwamba ukizingua kwenye taasisi yako au shirika unatimuliwa kwa aibu lazima tu waogope...mtoa mada hakuna rais mpole atakayefanikiwa africa Mungu ametupa mfano bora wa magufuli kazi kwetu
Magufuli alifanikiwa kwenye nini? Labda kuteka na kuua basi
 
Kwa sisi Waafrika, Viongozi bila kutumia Ubabe kiasi kwa kiasi fulani, hakuna kitakachofanyika kwa mafanikio makubwa.

Ni kwamba, Kiongozi atakuwa anajaza maji kwenye Tank, na wengine kwa wakati huo huo watakuwa watatoboa Tank hilo kwa lengo la kujinufaisha wao wenyewe tu.
Kwani hakuna sheria na katiba ndio utumie ubabe?
 
Kinacho ongoza nchi ni katiba sio ukali wala upole tatizo viongozi wa kiafrika wanajifanya wakali hili waibe sio kusimamia katiba mfano msv7 magu kagame nk
South Africa wana katiba nzuri sana, lakini rais wao yuko kwenye skandali za ufisadi karibu kila mwaka, hiyo katiba yako inasaidiaje hapo?
Kenya wana katiba nzuri, lakini wamechagua rais aliye na tuhuma za ufisadi wa kutisha, hiyo katiba yako inasaidiaje hapo?
 
Rais haihitaji kudhibiti nchi, wala haitaji kuwa katili ili watu wamwogope, ni mawazo ya ajabu kabisa.

Lakini haishangazi, hata katika familia zenu wengi wenu mnaogopwa na watoto wenu badala ya kuheshimiwa.
Huko kuheshimika kukoje boss
 
Back
Top Bottom