Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Mimi mwanaume-Tarehe 13/12-Herufi G
Mwanamke. -Tarehe 15/7-Herufi E
 
Mimi 14 December
Yeye 24 february

Wote herufi 'F'

Mimi mwanaume
 
Duuuuh shukrani sana mkuu, nimepata kitu na mengi uliyosema ni kweli kabisa.....!

Hii elimu wenzetu mnajifunza wapi?
 
Mimi ni Me, naitwa N, nimezaliwa tarehe 22/12.

Yeye Ke, anaitwa J, amezaliwa tarehe 2/8.

Ahsante!..
 
me 18/6
ke 26/7
 
Unaweza kutupa solution ili mambo yabadilike?
 
Ke ni 7/3 herufi H..Me ni 8/6 herufi R
Kwa mtizamo wewe unaonekana ni upepo wa chini na yeye ni maji yaliyotulia(kisima) kwa muunganiko huu inaonyesha dhahiri kwamba ni watu wawili hamuendani hata kwa kuendana kwenu ni kwa asilimia 9 pekee hivyo kwa hapa hata urafiki tu kwa ushauri huwezi kuwa nae kirafiki hakuna popote ambapo mnaendana maana hata kwenye kukutana kimwili ni asilimia 15 tu hakuna kitu kinaenda pamoja nae rohoni ni mtu hamuendani kwa vyovyote lakini kama tu unataka kujua muunganiko wenu hakuna kwenu nyinyi ni baina ya mbingu na ardhi na hata ukilazimisha sana utajitesa wewe na ndugu,jamaa,marafiki hakuna atakae mkubali labda kwa miujiza ya Mwenyezi Mungu jitahidini kila mtu atizame muelekeo mwingine.
Lakini kama utang'ang'ana nae huyo huyo naweza nikakuchambulia kwa undani zaidi

Rakims
 
Mkuu mimi ni mume jina E tarehe ni 6/12
Mke jina nalo ni E tarehe ni 18/1
Habari kwa wewe na yeye nyote mnasimama mlango mmoja wa upepo wa kimbuga kuwa na pacha wa kiroho haimaanishi kwamba ndio kila ja mbo mtaendana hapana unaendana nae mengi isipokuwa nikitaka kukupangia kwa asilimia nitakwambia hivi;
  • Sextendo 50%
  • Uaminifu 100%
  • Maelewano 70%
  • Hisia 40%
  • Kuthaminiana 80%
  • Kushirikishana 99%
Sasa kwa maana hiyo mnakuwa mnaendana kwa asilimia 75 tu. hii ni kutokana mnakuwa mmekosa mambo mawili kwenye sex itafikia sehemu utaona hakuna jipya tena na itakuwa ni kitendo cha kawaida tu kama wajibu na sio starehe tena na pia hisia kwa maana upepo ukiwa mkali wote mnakuwa na same feeling na ukishuka mnakuwa sawa yaani kwa maneno mengine ni kwamba wakati wako wa kufurahi kama umetoka na mambo yako unafurahi ukirudi ndani unakuta nae siku hiyo ana furaha ukija upo hovyo nae utamkuta hivyo hivyo muhimu mtakuwa na maelewano mazuri yaani ukitaka akuache hata kabla hujamwambia anaweza kukuacha utulie mwenyewe;
Uchambuzi wenu unakuwa hivi;- Mnaonekana ni wenye kupendezana na wote mnapendana,
na wote mnakuwa na furaha za kila mmoja katika hali za ucheshi yaani kuna muda mnakuwa ni watu wa matani na mnakuwa mnafurahia matani hayo
Uvumbuzi wa baadhi ya mambo yenu mkiwa na maelewano au katika kusolve jambo mnakuwa ni wenye maelewano makubwa na yenye kuvutia mnaendana pia kingono na mnaendana katika matamanio yenu na pia nyote mnafanana katika mipango na uwekezaji mnakuwa mnaridhiana na mnaweza kuishia kama marafiki na kuwa wapenzi kisha kuwa wapenzi na kurudia urafiki na hata mkipishana kila mtu anafanya wajibu wake katika ndoa au mahusiano hamna vita zisizo na maelewano na vile vile jambo la kugombania mara nyingi mnakuwa hamna au sababu ya ugomvi mnakuwa hamna, na mara nyingi mnaweza kukaa mbali mbali na umbali kwenu sio tatizo katika ndoa au mahusiano yenu.
Nyote wawili huendekeza busara zaidi kuliko hisia kitu ambacho kinafanya muwe wa kipekee
Upendo wenu haupo deep sana mfano wa kuzama sana kwenye dimbwi la mapenzi lakini mapenzi yenu yanakuwa yanatoshana


SEHEMU ZA HISIA:
Sehemu zake za hisia ni sawa na zako yale unayopenda kufanyiwa utakuta na yeye ni hayo hayo anapenda kufanyiwa na sehemu zenu nyote za hisia zipo kwenye supu za miguu ya chini ikiwa umeshajua hilo au bado basi jaribu kufuatilia miguu ina nafasi kubwa sana katika hisia zenu na hata maumivu mara nyingi kwenu huwa ni miguuni.

Rakims
 
Mimi Me 24/1 G
Ke 11/9 M.

Soda nitatuma
Sawa mkuu kwa mtizamo unaonekana ni mtu mwenye mwenendo wa upepo wa kimbunga na yeye ni mchanga mwekundu kwa mtizamo huu tu ni watu ambao hamuendani lakini nitakufafanulia hapa kwa ziada maana mnaendana kwa asilimia 30 tu na tofauti na hii na mkuu aliye pita hapo nyuma ni vile yeye alikuwa kinyume chenu yani yeye alikuwa katika asili ya kinyume cha yako hivyo inakuwa hivi;-

Nyote mnaonekana ni watu wenye wigo mpana wa kiakili zaidi kuliko kihisia; ambapo hii inapelekea yeye kuwa zaidi anachunguza ubaya au mabaya yako kuliko wema na kuwa ni mtu wa kukushukia kwa mabaya wakati wewe unakuta ni mtu unamchukulia kawaida na unakuwa huna nafasi ya kukaa unamchunguza chunguza sana na unakuwa sana ni mtu wa kumuwekea dhana wewe unakuwa ni mtu wa kujishughulisha na mambo ya kijamii kutoka na kuwa na mzunguko mpana wa marafiki wakati yeye anakuwa ni mtu mwenye marafiki wachache na vile vile ni mbaguzi wa marafiki,
Mitizamo yenu nyote wawili inakuwa ni tofauti;- wewe unakuwa ni mtu muuangalifu iwezekanavyo hali ya kuwa yeye anataka kufanya mambo yake kwa jinsi anavyotaka yeye na hataki kuingiliwa.
Kiakili mnakuwa mnaendana lakini mahusiano hayataki akili tu hisia hucheza nafasi kubwa sana. japo kuwa kila mtu kati yenu anajielewa mtizamo unaonyesha kama mtaoana hamna maisha marefu ya ndoa.

SEHEMU YAKE YA HISIA;

Sehemu yake ya hisia zaidi ni supu za miguu na ankles. Gusa,papasa,tomasa au mbusu sehemu hizo basi ukifanya hivyo utaona hisia zake zinapanda kwa kasi na anakuwa radhi hilo ni eneo nyeti sana kwake na wengine wao hupenda kusafishwa miguu saloon hivyo Kugusa,
kusugua, kupapasa, au kumbusu sehemu hii ya mapenzi ya anatomia kwa kiasi kikubwa humuamsha hamu ya tendo.
mfanyie kumbembeleza kifundo cha mguu, kusonga hadi supu kama massage laini, na uone jinsi anajibu haraka.
Wanamaji hupenda kuwa na miguu ya chini na vifundo vyao vya miguu vilivyotiwa ujazo mfano mguu wa bia hupenda pia mchezo wa kumwagiwa maji miguuni.

Kama hatua ya awali ya kufanya mapenzi, mpe massage nzuri ya miguu. Tumia vidole vyako au kucha, na na uwe kama unampatia ganzi kiasi
utaona analalama kwa upole. Anza kwenye vifundo vya miguu, na ueleze polepole duru kuzunguka mfupa wa kifundo cha mguu.
Mpake mafuta kwenda juu kwa taratiibu hadi eneo lote la nyuma uone mguu umelegea Wakati wa kufanya mapenzi, jitahidi kushika miguu yake na kuifanyia mitelezo utaona anazidi kutoa sauti za mahaba na mawadah.
japo kuwa hamuendani hii inaweza kukusaidia kwa nafasi kubwa kuweza kumkamata.

Rakims
 
Duuuuh shukrani sana mkuu, nimepata kitu na mengi uliyosema ni kweli kabisa.....!

Hii elimu wenzetu mnajifunza wapi?
Ni elimu inataka hekima sana kuweza kuwa nayo inapatikana katika dini zote mbili,vile vile katika vitabu,vichwani mwa watu,kwa malaika,katika historia,katika majaliwa na mwanzo wake ni kwa mwenyezi Mungu yeye ambaye humpa amtakae na humnyima amtakae ambae humpa mmoja kimoja na mwingine kingine ili mizani iweze kuwa sawa katika ulimwengu na kutegemeana katika mazingira.

Rakims
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…