Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Daah aise shukran sana boss ni mle mle
 
Msaada:
Me. 17/01 S
Ke. 09/10 M
Mahusiano haya ni sawa na watu wawili waliokosa uelekeo hawa ndio ukiskia mtu kakosea kuoa au kuolewa.
Wewe ni mchanga wa bahari na yeye ni upepo wa juu licha ya kutokuendana hata kukaribiana hamkaribiani,
hili utajionea maana ya ile kauli kwamba unaweza kukaa kwenye uhawara miaka 10 lakini mwaka mmoja wa ndoa ukakushinda.

Mtizamo upo hivi:
Wewe ni mtu mwenye kuvutiwa na yeye kwa sababu ana mvuto ambao wewe unajikuta ni mtu wa kumbembeleza pamoja na kubembelezea mapenzi. Upendo mlionao unaweza kukuokoa kwa kipindi fulani lakini hizi ndio ndoa ambazo wenza huwa wanarushiana ngumi maana ni uvumilivu hadi una fikia hatua ya kukata tamaa.
Japo mtafanikiwa kupata watoto kirahisi na mtazaa watoto wazuri kwa kuwa tu mnaingia mlango wa 5 kwenye ndoa yaani kizazi na mali lakini mateso ni makubwa kuliko mapenzi.

Yeye ni mtu mwenye tamaa na wewe kwenye mahusiano kwa muda huo ambao utakuwa nae au mtakao kuwa pamoja.
Elewa ya kwamba mahitaji yake katika mapenzi kuna jinsi na hali atakazo kuwa anataka uwe na wewe hutakuwa na uwezo wa kumpatia, Kikubwa wapo ni hisia haijarishi utafanya nini kwake hataona ukweli wa hisia zako kumpenda na ataona ni maneno tu.
Pia kutoshelezana kwenu ni kwa uchache sana yeye anapenda sana mauno na wewe magoti kidogo itafikia sehemu itakuwa ni mtihani kipindi hiki kwanza utakua huelewi elewi utakuwa unaona kama ni mtu asiyesomeka,
Baadae mwezi wa 9 hadi wa 10 kama hujamuoa anaweza kukwambia anaona uelekeo wa maisha hauoni na kuna uwezekano mkubwa mwezi huo wa mwaka huu akaanza kujihusisha na mtu mwingine na pia utapata habari kupitia mawasiliano yake kwa hivi sasa.

Atapenda mambo ambayo hutaweza kumtimizia kwa wakati anaoutaka sio kwamba huna uwezo wa kutimiza na akiwa tofauti na mtu mwingine utaona hiyo tabia hana atakuwa nayo kwako.

Na katika hali za kujionyesha na kuwaonyesha watu kuwa ana jambo fulani ni tabia ambayo wewe huna kitu ambacho yeye hupenda mtu aliyenae awe hivyo
Na utakuwa ukimuheshimu kwenye mahusiano na yeye atakuwa anakuchukulia kama ni mpuuzi atakuona mbinafsi na unakosea na mapenzi hayapo hivyo na utatolewa kasoro kila mara.

Baada ya hapo kwenye mahusiano hukugeuka na kuanza
kuangalia mahali pengine na kukuweka uwe na wivu nae kwake ni starehe yake japo ni jambo litakalo kuwa linakutesa.

Japo kuwa ni mtu mzuri kwa watu wengine kwako wewe mahusiano haya ni Kichocheo cha maafa (Sijataka kwenda deep sana kwenye case ya wazazi ambayo ndio inanifanya nikwambie ni mtu asiyekufaa.

SEHEMU YA HISIA:
Kiuno chake ndio sehemu inapotawala hisia yake utaona analalama kiuno kinasumbua ili tu kupata kupapaswa na kukandwa eneo hilo.

Rakims
 
Me 07/12 A
Ke 11/08 k
 
Me 07/12 A
Ke 11/08 k
Katika mahusiano yenu wewe unaonekana ni mwenye asili ya moto wa nyasi na yeye ni moto wa mkaa mnaendana vema kila mmoja kati yenu anamuona mwenzie anamfaa zaidi.

Kuna mambo mengi ya kusisimua yatakayo kuja kuwatokea kwenye mahusiano yenu, yeye mwenye kujiamini inatoa uhakika kabisa kwamba atafungua hisia zako zote za tamaa ulizonazo katika mapenzi, na mapenzi yenu ni ya maajabu sana, nyote mnafurahia kusafiri pamoja, kukutana na watu wapya, na kila mmoja kati yenu anafurahika kuwa karibu na mwenzie yeye ni mwenye kupenda uhuru sana ikiwa ni pamoja na wewe,

Hivyo katika mahusiano yenu kutakuwa hakuna matatizo ya wivu ikiwa ni pamoja na kutawaliana ni couple moja nzuri sana mkipatana.

Wewe una mwanga mzuri wa kuendana nae kimazungumzo na vile vile ni mwenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na Gubu lake.

Hakuna maelezo mengi kuhusu mausiano yenu isipokuwa jambo kubwa moja ni kwamba nyie ni Grand mating.

Ukimpoteza huyo kumpata wa hivyo huwa kazi.

Rakims
 
Ahsante mkuu
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
Aiseee Asante
 
Asante sana mkuu.. yaani kila kitu ulichoongea nakiona kinafanana na maisha tulonayo..sijui nifanyeje maana tumeishi miaka mitano na tayari tuna watoto wawili wazuri kwelikweli. Hatujafunga ndoa kila tukipanga linatokea jambo la kuahirisha. Sijui nifanyeje
 
Msaada
Me 7/2 A
Ke 7/7 F
 
KE 22/7
ME 29/12
 
Msaada
Me 7/2 A
Ke 7/7 F
Utangamano
Mahusiano haya ni baina ya Nyota ya maji ya bahari na upepo wa kimbunga, Kiasili wawili hawa wakiwa pamoja kwa upole basi utaona kila mtu anapenda mapenzi yao ya awali na kila mtu atawaonea tamaa mahusiano yao.
Lakini ukweli ni kwamba upepo wa kimbunga na bahari siku zote mapenzi yakitaka kuwa moto moto basi Dhoruba hutokea.
Ukiwatizama wawili hawa wewe mwenye nyota ya Kaa unakuwa na tabia za uchangamfu, kujituma basi utaona ni mwenye kupatiana sana na Ndoo ambaye ni mwenye tabia ya kujitawala.

Kwa upande mwingine utaona wewe ni mwenye kung'ang'ania vitu ni tabia ambayo itamuonyesha waziwazi na humfanya yeye (Aquarius) ajisikie amebanwa na anakosa uhuru binafsi kama awali.

Na kwa kuwa yeye ni mwenye akili ya haraka, asiyetabirika, utamuona anaanza kupapatika na tabia yako ya kung'ang'ania vitu, wewe (Kaa) una ubishi na ujeuri wa asili na pia huwa ni king'ang'anizi.

Na kwa wewe mwenye roho ndo ni rahisi sana kuumizwa na masihara yake ya kutaka kukucheka yaani unaweza kuleta hisia na yeye akawa anakiucheka ama kuonyesha kutokujali,
Wewe binafsi ni mtu ambaye utajikuta humuelewi yeye hasa ukizingatia kwamba wewe ni mwenye kupenda kujihisi umelindiwa mapenzi yako na upo karibu na mwenza wako, lakini yeye ambaye ni mtu wa ajabu na matukio hukufanya ukihisi kukosa ukaribu nae kulingana na visa vyake.

Yeye kwako ni sawa na mbwa mwitu, kwenye sex mnaendana sana isipokuwa kuna kitu kinakosekana kikubwa kwenye mahusiano haya.

Rakims
 
KE 22/7
ME 29/12
Mahusiano:

Kati yenu kuna mvuto mkubwa sana wa kingono na pia mnaendana vizuri na kimtizamo mnaendana vema sana kwa maana yeye ni mchanga wa bahari na wewe ni maji ya bahari hivyo mna mtizamo mmoja katika mambo yenu mengi na mnaendana kwa asilimia nyingi

Kama mtaweza tu kuwezana tabia zenu basi moja kwa moja mtakuwa na mahusiano yenye bahati na mafanikio makubwa kindoa mfano wake utasikia watu huyu kaoa leo nyota yake imeng'aa au mafanikio yake yamefunguka yupo vizuri kwa kila sekta hii ni kwa maana kuwa hata mkiingia kindoa mnapatikana katika mlango wa 12 yaani mzunguko mzima wa nyota 12 unakuwa pamoja na nyinyi bega kwa bega na kila mmoja wenu anakuwa kayapatia maisha na hakuja haja ya kuhofia riziki kwa maana kwenu mkiwa pamoja kila jambo huenda vizuri na kwa ufasaha zaidi.

Lakini kwenye mlango wa kazi pia unatakiwa sana ujitahidi kumuachia yeye pia afanye kazi na kama ni biashara mpe nafasi ya yeye kuisimamia utaona maajabu ya Mungu kwa maana wewe asili yako ni mazingira ya nyumbani na yeye ni mtafutaji mzuri na ana nyota ya mafanikio na ndio bahati yako imelalia kwake usije kumvuruga wala kumuharibia muelekeo,
kwani huyu unaweza kutembelea nyota yake pindi utakapofunga nae ndoa na ukitaka kuthibitisha hapa kwa watu kwamba haya mambo sio kubahatisha basi muoe siku ya jumatatu kama sio saa 1 asubuhi saa 8 mchana na kama sio hapo basi saa 3 usiku.

Ukizingatia hayo unaweza kujiuliza ulichelewea wapi kwa maana usiku wa kwanza tu mmeanza kuitumikia ibada ya ndoa matunda yake siku inayofuata hadi kuingia usiku utaona matokeo na hapa nazungumzia ndoa sizungumzii uhawara.
Ni mtu sahihi kwako na ana maslahi mengi na hutaamini ukiwa nae na pia ni mtu ambaye anaweza kukukamilishia all the attention you need.

Na vile wewe ni mtu wa aibu na mwenye hisia kali na kupenda kukosoa basi huyu kwako ni sahihi;-
Mtizamo unaonyesha wewe ni mtu wa aibu,hisia na mwenye kutaka affection wakati yeye ni mtu wa kuondoa aibu,kuponya maumivu ya hisia na kutawala ndio sifa zake basi popote utakapo hisi you are down she will lift you up haijarishi kipesa mawazo au hisia.

Tofauti zenu zinaweza kuwa kubwa sana ambazo zitaleta furaha za muda mrefu, yaani hapo ni mfano wewe ni hasi na yeye ni chanya. Perfect Match.

Rakims
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…