Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Nitajie tarehe yako na ya mwenza wako nikwambie mpo vipi na hatima yenu, siri yake n.k

Rakims mimi ni mwanaume jina linaanza na S na nimezaliwa tarehe 17 july 1984 na wife jina linaanzia herufi A amezaliwa tarehe 21 October 1987. Nahitaji uchambuzi wako mkuu.
 
Hawezi kuja huyo, lengo lake sio kutoa msaada humu bali ni kiwapiga pesa. Na ndio maana katoa maelezo mengi halafu kaweka na namba za simu ili wakuingia kingi aingie kwa kumtafuta kwenye simu. Angekuwa mtoa huduma angewajibu watu humu ila ni mtumia fursa huyo
No free lunch mkuu,sio mbaya mkimchangia hata ya soda..
 
Ke ni 7/3 herufi H..Me ni 8/6 herufi R
Kwa mtizamo wewe unaonekana ni upepo wa chini na yeye ni maji yaliyotulia(kisima) kwa muunganiko huu inaonyesha dhahiri kwamba ni watu wawili hamuendani hata kwa kuendana kwenu ni kwa asilimia 9 pekee hivyo kwa hapa hata urafiki tu kwa ushauri huwezi kuwa nae kirafiki hakuna popote ambapo mnaendana maana hata kwenye kukutana kimwili ni asilimia 15 tu hakuna kitu kinaenda pamoja nae rohoni ni mtu hamuendani kwa vyovyote lakini kama tu unataka kujua muunganiko wenu hakuna kwenu nyinyi ni baina ya mbingu na ardhi na hata ukilazimisha sana utajitesa wewe na ndugu,jamaa,marafiki hakuna atakae mkubali labda kwa miujiza ya Mwenyezi Mungu jitahidini kila mtu atizame muelekeo mwingine.
Lakini kama utang'ang'ana nae huyo huyo naweza nikakuchambulia kwa undani zaidi

Rakims
 
Mkuu hivi ni kweli hunielewi .....mbona nimeandika clear kabisa ....

Me na ke nimeainisha vizuri kabisa hapo .....mm ni Me.
Nimeomba urudishe kuandika quote yako ikiwa imejitosheleza na sio mimi kuanza kurejea kurudi kwenye quotes za nyuma kutafuta ulisema nini kuna shida?
 
Rakims Mimi nimeoa Ila nishaweka taarifa Mara mbili unanipita tu.
Mimi ni mwanaume jina linaanzia I tarehe yangu 26/06 na mke ni M tarehe 15/08
 
Mimi ni mume jina linaanzia I tarehe ya kuzaliwa 26/06 na mke wangu ni M tarehe ya kuzaliwa 15/08
Kwa mtizamo wewe unaonekana ni mwenye asili ya maji ya bahari na yeye ni moto wa mkaa hivyo kwa mchanganyiko huu sio mzuri sana kindoa kwa maana ni baina ya maji na moto wewe utakuwa kwake ni kama unazima mambo yake na wewe anakuwa anakukausha kuna mambo unakuwa unakosa,
Mnaendana kwa asilimia 28 tu. kitu kinachowalinda ni huruma na uaminifu tu mlionao kila mmoja kwa mwingine laki kiuhalisia hamuendani na mtu katika hali ya ndoa ndoana lakini mnaweza kujifariji kwa imani na huruma tu pia inaonekana nyote ni wenye upendo kila mmoja kwa mwingine ingawa kila mmoja wenu ana utazamio wake kwa mwenzie.
Ingawa unaonekana ni mtu unaweza kuvumilia mitoko na uchangamfu wake kwa watu ikiwa utazuia hilo basi yeye huanza kukuona hunauelekeo sawa na yeye na pale anapotaka mambo yake unakuwa unambishia na kukaza msimamo basi ndio mambo huanza kuharibika ukimchunguza ni mtu ambaye hupenda kulelewa kama malkia na kila kitu yeye ndio awe mtawala umakini na utulivu wako wa akili ni kitu pekee au silaha ambayo mkiwa nae inakuwa inakusaidia kutokana na tabia yake ya jeuri,kiburi na kuzila pamoja na ukali.

Yeye ni mtu hupenda kusifiwa sifiwa na kubembelezwa pale anapokuwa kakasirika
Na yeye utakuta ni mwenye kujisifu mnapokuwa chumbnani na kuona kama kwenye tendo huwa anakuzidi na mara nyingi wewe huonekana kama mzembe hapo mchezoni kwa mtizamo wake.
Unaweza kufurahishwa nae kwa kipindi fulani hasa ukizingatia ukipoa anaweza kukuchemsha lakini still bado mpo tofauti sana katika mlango wa ndoa maana hata mkioana mnaingia mlango wa 9 ambapo kama ni watu hamna elimu za dunia basi lazima imani za dini ziwabebe tofauti na hapo kila mmoja hubaki anajuta rohoni bila kisema kwa uwazi.

SEHEMU YAKE YA HISIA;
Sehemu yake kuu ya hisia ni kifua na eneo la moyo kuja hadi nyuma kwenye mgongo wa juu upande wa kushoto kushuka hadi kwenye kalio la kusho sehemu hizo kwake huwa ni kama umeme ninaposema kifua simaanishi maziwa sehemu ya maziwa ni watu kama wewe wenye asili ya maji ya bahari lakini kwa yeye ni eneo la moyo na mgongo wa nyuma hasa akiwa mtupu ukapapasa huko huhisi ashiki za kiwendawazimu na kutamani kufanya tendo na ni mtu mwenye kupenda sana kufanya kwa mikiki na pia huwa hakubali kushindwa hizo ndizo sehemu kuu zinazotawala hisia zake

Rakims
 
M 08/11
M 08/11
(me vs me)
Niangalizie hapo nikiwa singo mambo yanakuaje
Tembelea jukwaa la chitchat kuna makala kule nyingi tu zinakufaa mkuu unaweza kutoa maoni huko wakakujibu kwa usahihi kabisa
 
Rakims Mimi nimeoa Ila nishaweka taarifa Mara mbili unanipita tu.
Mimi ni mwanaume jina linaanzia I tarehe yangu 26/06 na mke ni M tarehe 15/08
Mkuu nilikuwa nimebanana kidogo niwie radhi kila anaeweka details huwa najibu nimekujibu hapo.
 
Soma thread tena mkuu utajua ni vitu gani navihitaji
Mimi ni Me jina linaanza na A na tarehe ya kuzaliwa ni 28/8

Mpenzi (Ke), jina linaanza na M tarehe ya kuzaliwa ni 22/7,

Tumezidiana miaka miwili, mimi Me ni mkubwa kwake
 
Back
Top Bottom