mkuu mimi ni Me jina langu linaanzia herufi I nimezaliwa 25/07 Mke jina linaanza na herufi A kaziliwa 05/06
Sawa mtizamo unaonyesha wewe ni moto wa mkaa na yeye ni upepo wa pumzi mnaendana sana japokuwa kwenye ndoa mnaingia katika mlango wa nane mlango wa kifo na ufufuo.
Mtizamo unaonyesha ni watu mnaweza kuingia haraka kwenye mapenzi au ndoa kwa sababu ni watu mnaweza kuwa na mtizamo mmoja na wenye kupenda mambo mengi yanayoendana.
Hivyo vitu vyenu vingi nyote wawili ni maisha ya kijamii,sherehe,theater(movies & tv-shows) marafiki wengi,uchangamfu.
Yeye anaonekana anaweza kufungua (joie de vivre) kama ni mtu wa kufuatilia sana series na movies utaelewa namaanisha nini yaani anaweza kukuretea furaha tele ya maisha mambo yenu ni watu wa kukimbizana na aina mbali mbali za burudani na furaha ya maisha nyote mnaonekana kila mmoja ni mwenye kumtafutia mwenzio kuona raha ya maisha kupitia yeye.
Unaonekana ni mtu mwenye kufurahia imagination zake zinazompeleka mbali kimawazo na vile vile uchangamfu wake chumbani na utani/uchokozi unafurahia sana kucheka na kufurahi mkiwa chumbani na ni mtu wa kupata hasira na kuishiwa hamu ya kufanya tendo pale anapojaribu kuweka userious kidogo chumbani.
Yeye anaweza kuwa kichocheo kikubwa cha wewe kuwa na wivu kwake kwa sababu ya njia nyepesi yeye aliyonayo katika kugawa/kusambaza upendo kwa watu tabia yake ya kucheka na kila tu hukufanya kuamsha hisia zako za wivu .
Unaonekana ni mwenye mihemko na mkali zaidi kuliko yeye.
Maisha yenu pamoja yanaonekana ni yenye kusisimua na kukasirisha at the same time,
Lakini mnaweza kukaa kwa furaha na amani ikiwa yeye tu atakuwa muaminifu na kuendelea kubaki hivyo vinginevyo Poof!
Mwisho wa hadithi.
Hiyo ni kutokana na wewe asili yako ni kuwa ni mtu mwenye moyo mkubwa na hisia kali na usiyeweza kuvumilia usaliti.
na mwenye kuweka kitu kwenye roho kwa muda mrefu sana.
Rakims