Yaani mi na unazi wangu wote wa mpira yaani kuanzia nikiwa mdogo let say kuanzia 2000 nipo la 3 huko nafatilia mpira sana hasa chama langu man u ambalo sa ivi ni tia tia maji.... Ila sikuwahi kushabikia Mpira wa bongo kabisa... Yaani nilikua siuelewi kabisa Wala Sina timu
Mzee wangu alikua mnazi wa Simba, nilianza kuwachukia Simba nikiwa mdogo siku Mzee Simba imebamizwa huko akaja home na hasira zake kosa kidogo tu tukatembezewa stick, ndo Maza badae anatuambia Leo Simba kafungwa mkileta utundu huyu Mzee Leo atawaua
Miaka kama mitatu nyuma ndo nimeanza kushabikia yanga, eti sa ivi wameniingia siwezi kukosa mechi zao wakati man u msimu huu sijaangalia hata mechi Moja nishawapotezea kabisa