Nitakulipa vizuri ukinipa hotuba ya Nyerere kama India Republic Day Guest of Honour, 26 January 1971

Nitakulipa vizuri ukinipa hotuba ya Nyerere kama India Republic Day Guest of Honour, 26 January 1971

Natafuta sana hii hotuba ya Nyerere aliyotoa India pale alipoalikwa kama mgeni rasmi katika sherehe za India kuwa Jamhuri, tarehe 26 January, 1971.

Kuna jambo kubwa sana alilisema ambalo tunapaswa tuliandike katika herufi za dhahabu katika historia ya Tanzania na India

Nimeuliza ubalozi wa India wanasema ni zamani sana hawana rekodi.

View attachment 2389074

..hiyo hotuba haipatikani ktk vitabu vya hotuba za Mwalimu Nyerere.

..nakumbuka kulikuwa na vitabu vitatu vyenye collection ya hotuba zake.
 
Mcheki Madaraka Nyerere,yule Bwana ana damu ya kupenda kusoma na kuandika Kama Baba yake,na pale Butiama Kuna siku TBC alikuwa anaelezea vitabu na machapisho ya Nyerere kwenye Library ya Mwalimu.
 
..Kuna vitabu vitatu vyenye hotuba za Mwalimu Nyerere.

..Kitabu cha kwanza kiliitwa " Uhuru na Umoja / Freedom and Unity. "

..Kitabu cha pili kiliitwa " Uhuru na Maendeleo / Freedom and Development. "

..Kitabu cha tatu nimekisahau jina lake.

..Yeyote anayependa kusoma hotuba, au uandishi wa hotuba, ata-enjoy kuwa na vitabu hivyo.
 
Nimeuliza ubalozi wa India wanasema ni zamani sana hawana rekodi.
Hao hawakupenda tu kukusaidia.
Hata kwenye kumbukumbu za nchi yao hawawezi wakaipata?

Hata magazeti tu yatakuwa yalichapisha hotuba hiyo, watakuwaje wasiwe na rekodi?
 
Mcheki Madaraka Nyerere,yule Bwana ana damu ya kupenda kusoma na kuandika Kama Baba yake,na pale Butiama Kuna siku TBC alikuwa anaelezea vitabu na machapisho ya Nyerere kwenye Library ya Mwalimu.
Inawezekana umemwelekeza mahala sahihi mleta mada ni wapi anapopaswa kwenda kuipata hiyo hotuba.

Nami niongezee: Daily News watakosa hotuba kama hiyo kwenye 'archives' zao?
 
Mnatafuta sana makosa madogo madogo kwa wenzenu. Na wewe tuambie "ndo" maana yake nini?
Kama ilivyo mie badala ya mimi, sie badala sisi, nyie badala ya nyinyi au kwa Malkia kule it's instead of it is, can't instead of can not etc na n.k.
 
Kama ilivyo mie badala ya mimi, sie badala sisi, nyie badala ya nyinyi au kwa Malkia kule it's instead of it is, can't instead of can not etc na n.k.
Kajifunze tena kiswahili
 
Hao ndiyo usijisumbue tu hovyo kabisa hao akina butiku
Hata mimi nilifikiria kwamba kwenye Foundation ndipo pa kuanzia. Usiwahukumu kwa kufikiria tu. Jaribu kwanza. Wakisema hawana ndipo upumue na kusema nilidhania hivyo.
 
Nenda TBC huko utapata audio Kuna library ya kutosha kuhusu kumbukumbu za mwalimu hapo.
 
Wacheki ndtv wanaweza kukupatia, nenda kwenye picha husika hapo chini, click kwenye email,
 
Back
Top Bottom