Nitakuwa tofauti na Mh. Spika kuhusu hili la Bandari ya Bagamoyo

Nitakuwa tofauti na Mh. Spika kuhusu hili la Bandari ya Bagamoyo

Bandari ya Bagamoyo, LNG plant Lindi na uchimbaji wa Hellium, hizi inshu zitakuja kulaza watu jela, hata kama ni baada ya miaka 10, jinai haifi, tutakuja kuyafukua na kurudisha pesa za watz mnazotaka kuwaingizi mkenge. SSH yeye ameingia tu anataka kuuza kila kitu, wenzie wangefanya hivyo yeye angekuta nini?

Kama ulikalia kimya wizi wa kura, ni kipi kinakufanya ushangae maamuzi ya watu wasio waadilifu? Hilo bunge liliwekwa na Magufuli kwa matumizi mabaya ya madaraka, hivyo hawajali lolote maana wamejua wananchi wanaweza kufanyiwa dhuluma na wakanyamaza. Sasa subiri hizo ndege uone zitakavyouzwa kwa bei ya vunja bei. Hapo ndio utajua ccm ni genge haramu na hatari kwa nchi hii.
 
Na Thadei Ole Mushi.

Spika wa Bunge kaishangaa Serikali kuanza kutengeneza Reli badala ya Kuanzia na bandari. Si mara ya kwanza Kwa Mh Ndugai kusema kuhusu ujenzi wa BANDARI hii mwaka 2019 alisema hata wachina wanatushangaa na wakatufananisha na MTU aliyetanguliza mkokoteni mbele halafu punda nyuma. Kwa maana ya kwamba kujenga Reli ni kutanguliza Mkokoteni Mbele halafu Punda nyuma.

Wachina wana hamu na ujenzi wa Bandari hiyo kuliko hata watanzania wenyewe. Je ni kweli wachina wanatupenda kiasi hicho?

Fact

Mwaka juzi China ilianza kushikilia mashirika muhimu ya Zambia baada ya Zambia kushindwa kulipa madeni inayodaiwa na China.

China ilishikilia Shirika la Utangazaji la nchi hiyo pamoja na Shirika la Umeme la Zambia (ZESCO) na bado wataendelea kutaifisha mashirika mengine kadri muda utakavyokwenda.

Huko Sri-Lanka nako wameshikilia Bandari ya nchi hiyo kwa Lengo lile lile la kulipa madeni ya China.

John Perkins kupitia kitabu chake Confession of an Economic Hit man anatufunulia jinsi sera ya Conspiracy inavyofanya kazi.

Perkins anaelezea kazi aliyokuwa akiifanya bila yeye kujua kwenye Kampuni la MAIN (Consulting and engineering Company)

Aliajiriwa kama mfanyakazi kwenye kampuni hilo ambalo ni Kampuni binafsi ila shughuli zake ziliathiriwa na mkono wa Serikali (Ujasusi) bila yeye kujua.

Kazi yake kubwa ilikuwa ni kushawishi nchi maskini zikope mikopo kwa ajili ya miradi mikubwa katika nchi zao. Miradi kama vile ujenzi wa miundombinu ya Reli,Ujenzi ya Umeme ambayo utasaidiwa kukopeshwa aidha na World bank, IMF au USAID.

Perkins alikuja kugundua kuwa njia hii ya kukopesha mikopo mikubwa ambayo hailipiki ni njia mojawapo ya Taifa la Marekani kuendelea kupata maeneo ya kunyonya katika nchi maskini.

Perkins anatoa mifano jinsi alivyofanikisha kuingiza Indonesia kwenye Mtego huo na nchi nyingine nyingi.

Kwa nchi ambazo zinaendelea na zenye rasilimali kama Gesi, Madini na mafuta Marekani huwa hawalali kwenye kuhakikisha inatafuta kuwakopesha.

China nayo imeaanza kunufaika na Sera hii ya conspiracy kila mahali wanajenga ushawishi mkubwa kutoa mikopo kwa ajili ya miradi mikubwa. Wanajua mikopo hii hailipiki hivyo wanaweza kunufaika wao.

Bandari ya Bagamoyo ikikamilika inafunika zote Afrika Mashariki, hivyo wateja wengi watahamia Bagamoyo ambayo itakuwa inaendeshwa na mchina baada ya sisi kukosa fedha za kumlipa mchina. Najiuliza Je China inaweza kutupenda kwa kiasi hicho? Je tunaweza kumlipa mchina?

Ole Mushi
0712702602

View attachment 1746890
Wewe Ole Mushi na Ndugai wote wana ccm. Nyote hamna jema na nchi hii
 
Tutauvunja kama wa Barick
Mkuu kwani mkataba wa Barrick umevunjwa? Hivi hujasikia juzi mama Samia alivyomuambia huko Barrick kuna mambo ambayo hayako sawa? Mkuu vuta subira, hilo genge haramu la ccm litavurugana utasikia ukweli utakao kufanya ujute kuzaliwa Tanzania.
 
Mjadala huu ungenoga zaidi kama huo mkataba mzima ungewekwa katika tovuti ili kila anayependa ausome; kisha tufanye debate sisi wazalendo tunaopinga huu mradi na wale wanaounga mkono huu mradi.

Inasikitisha mradi mbovu kama huu ambao naamini pengine hata chifu Mangungu asingeukubali lakini leo hii unatetewa na watu ambao ni wasomi! Hivi nini kifanyike ili somo la uzakendo liwaingie watanzania wote?
bila kusahau presentation iliyomkuna ndugu yai
 
Tatizo kubwa kwa viongozi wengi ni fikra na mtazamo finyu, hivyo kujadili na kuamua mambo muhimu kwa taifa kwa ufinyu huo huo.
Pia TISS ina tatizo la intelligence na hivyo kuelekeza nguvu nyingi kufanya kazi za siasa chafu ndani ya nchi badala ya kupambana kimataifa.
Maadui wa taifa siyo raia wenye mitizamo na itikadi tofauti bali nchi nyingine zenye kutafuta faida dhidi ya Tanzania.
 
Uchambuzi wako uko kwa upande mmoja, umelenga kuukosoa uwekezaji China kwenye bandari ya Bagamoyo ambao kwa sasa unatetewa mnoo na Spika Nduga.

Vipi kuhusu uwekezaji wa China kwenye ujenzi wa SGR na Bwawa la umeme ambao ulitetewa na Magufuli ?

NOTE
kuweka kumbukumbu sawa, miezi michache kabla ya kifo chake, Rais Magufuli aliutangazia ulimwengu kuwa amewasiliana na Rais wa China na kuiomba serikali ya china ije kuwekeza kwenye ujenzi wa SGR na bwawa la umeme unaoendelea sasa.
Mchina anajenga bwawa la umeme la wapi?, SGR Kapatiwa kipande cha kutoka Mwanza hadi Isaka,wapi tena wanajenga?.
 
Je, tunao ushahidi au ni propaganda kuwa Wachina wanakamata mali za nchi eti kwa kuwa nchi hiyo imeshindwa kulipa deni? Wanakamata bila makubaliano, bila matakwa ya mkataba? Leteni hiyo rasimu ya mkataba wa Bagamoyo nasi tuichambue. Kama kweli ni mbaya sisi si wajinga tutaona na tutakataa. Tusiukatae mradi kwa kuwa ni wa Bagamoyo, au ulioasisiwa na akina Kikwete, huku tukisingizia yasiyoonekana
Mkubwa

Sir lanka wanalia
 
VIchwa vibovu.

Katika moja ya mkutano na waandishi habari. Mkurugenzi wa bandari alisema walijadiliana sana na wachina hadi 2018 kuhusu mkataba huo, lakini kuna mambo ambayo China haikutaka kuyaondoa na mazungumzo yakafa. Sasa naona Boss huyu anapiga kampeni kwa vigezo dhaifu kabisa!

Yaani presentation aliyofanyiwa China ndo iwe nzuri kwake kwa miaka 5 iliyopita! Lazima kuna jingie nje ya presentation.
Mostly 10%
 
Na Thadei Ole Mushi.

Spika wa Bunge kaishangaa Serikali kuanza kutengeneza Reli badala ya Kuanzia na bandari. Si mara ya kwanza Kwa Mh Ndugai kusema kuhusu ujenzi wa BANDARI hii mwaka 2019 alisema hata wachina wanatushangaa na wakatufananisha na MTU aliyetanguliza mkokoteni mbele halafu punda nyuma. Kwa maana ya kwamba kujenga Reli ni kutanguliza Mkokoteni Mbele halafu Punda nyuma.

Wachina wana hamu na ujenzi wa Bandari hiyo kuliko hata watanzania wenyewe. Je ni kweli wachina wanatupenda kiasi hicho?

Fact

Mwaka juzi China ilianza kushikilia mashirika muhimu ya Zambia baada ya Zambia kushindwa kulipa madeni inayodaiwa na China.

China ilishikilia Shirika la Utangazaji la nchi hiyo pamoja na Shirika la Umeme la Zambia (ZESCO) na bado wataendelea kutaifisha mashirika mengine kadri muda utakavyokwenda.

Huko Sri-Lanka nako wameshikilia Bandari ya nchi hiyo kwa Lengo lile lile la kulipa madeni ya China.

John Perkins kupitia kitabu chake Confession of an Economic Hit man anatufunulia jinsi sera ya Conspiracy inavyofanya kazi.

Perkins anaelezea kazi aliyokuwa akiifanya bila yeye kujua kwenye Kampuni la MAIN (Consulting and engineering Company)

Aliajiriwa kama mfanyakazi kwenye kampuni hilo ambalo ni Kampuni binafsi ila shughuli zake ziliathiriwa na mkono wa Serikali (Ujasusi) bila yeye kujua.

Kazi yake kubwa ilikuwa ni kushawishi nchi maskini zikope mikopo kwa ajili ya miradi mikubwa katika nchi zao. Miradi kama vile ujenzi wa miundombinu ya Reli,Ujenzi ya Umeme ambayo utasaidiwa kukopeshwa aidha na World bank, IMF au USAID.

Perkins alikuja kugundua kuwa njia hii ya kukopesha mikopo mikubwa ambayo hailipiki ni njia mojawapo ya Taifa la Marekani kuendelea kupata maeneo ya kunyonya katika nchi maskini.

Perkins anatoa mifano jinsi alivyofanikisha kuingiza Indonesia kwenye Mtego huo na nchi nyingine nyingi.

Kwa nchi ambazo zinaendelea na zenye rasilimali kama Gesi, Madini na mafuta Marekani huwa hawalali kwenye kuhakikisha inatafuta kuwakopesha.

China nayo imeaanza kunufaika na Sera hii ya conspiracy kila mahali wanajenga ushawishi mkubwa kutoa mikopo kwa ajili ya miradi mikubwa. Wanajua mikopo hii hailipiki hivyo wanaweza kunufaika wao.

Bandari ya Bagamoyo ikikamilika inafunika zote Afrika Mashariki, hivyo wateja wengi watahamia Bagamoyo ambayo itakuwa inaendeshwa na mchina baada ya sisi kukosa fedha za kumlipa mchina. Najiuliza Je China inaweza kutupenda kwa kiasi hicho? Je tunaweza kumlipa mchina?

Ole Mushi
0712702602

View attachment 1746890
Hivi maana ya EPZ nini nimesikia mama akikomaa mayo kweli si na bandari ina EPZ pia

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Naona wameamua kufanya upuuzi kwasababu sheria zipo kwa ajili ya wezi wa kuku tu.

Sasa Ndungai wakiingia kwenye mikataba ya kinyonyaji tutafukua hata kaburi lake na kupiga pingu
 
Naona wameamua kufanya upuuzi kwasababu sheria zipo kwa ajili ya wezi wa kuku tu.

Sasa Ndungai wakiingia kwenye mikataba ya kinyonyaji tutafukua hata kaburi lake na kupiga pingu
Itakuwa haisaidii tena chochote kiongozi
 
Hili la Bandari ya Bagamoyo litamtoa Mtu Madarakani ni suala la muda tu, ulafi wao na njama zao zishajulikana vzuri tu.

Kwanin Viongozi wasiwe watulivu kwanza hadi waaanze kuja na hoja zenu walakini ambazo zinaweza kuleta taharuki na hata maandamano na machafuko? Why now ambapo hata ile miradi mikubwa ya kimkakati haijaisha? Nyieeee
Bandari ya Bagamoyo ni muhimu sana kuliko kiwanja cha ndege cha chato kwa sasa.
 
Ikisha sainiwa ni too late, vizazi na vizazi wataaajibika, hahaa chezea mikataba wewe
Jamani Kenya wamejenga Bandari nyingine Malindi,inaisaidia sana bandari ya Mombasa.Sisi tunabishana kuhusu bandari ya Bagamoyo.Wenzetu wanakimbia sie tunatembea.
 
Back
Top Bottom