Nitakuwa wa mwisho Kuamini kuwa Uchumi wa Tanzania umeshuka kutokana na Corona na ndiyo maana Mishahara inapigwa tu 'Danadana' Kupandishwa

Nitakuwa wa mwisho Kuamini kuwa Uchumi wa Tanzania umeshuka kutokana na Corona na ndiyo maana Mishahara inapigwa tu 'Danadana' Kupandishwa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ninachojua GENTAMYCINE kwanini Mishahara imekuwa ikipigwa tu 'danadana' Kupandishwa kwa Watumishi nchini tokea 2016 hadi tarehe 17 March, 2021 ni......

1. Kukurupuka kuanzisha Miradi
2. Kuwekeza zaidi Chato
3. Kukomoa Matajiri wakubwa
4. Ufisadi mkubwa tu Serikalini
5. Kuharibu Mifumo ya Pesa
6. Usimamizi mbovu wa Mapato
7. Uhusiano mbaya Kidiplomasia

Ushauri wa bure tu kwa Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan tafadhali 'Kivuli' cha Hayati Rais Dkt. Magufuli kisikutishe katika ama Kuamua au Kufanya yale unayoyaona ni bora ( sahihi ) kwa Watanzania na Tanzania kama nchi.

Nimekuwa nikikuangalia sana kwa Jicho langu Kali la Saikolojia yangu Kubwa ya Kiasili na Kugundua ya kuwa unapenda mno kufanya Mabadiliko hasa ya Kiuongozi, Kimaamuzi na Kiutendaji kutoka kwa Mtangulizi wako ( Hayati Rais Dkt. Magufuli ) ila ni kama vile 'Unaogopa' au 'Unajishtukia' labda Watu watakuelewa vibaya.

Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan tambua ya kwamba Hayati Rais Dkt. Magufuli aliandika Kitabu chake na ameondoka nacho tayari hivyo na Wewe huu sasa ni wakati wako Kukiandika chako ili Watanzania tukukumbuke ama pale Ukistaafu au hata nawe pia Ukitwaliwa ghafla ( japo siombei ) kama Mwenzako.

Ningeshauri tu hebu weka Uwiano ( Balansisha ) katika Kuinua Vipato vya Watanzania, Ustawi Wao na Miradi Muhimu ya Kimkakati. Inauma na Kukatisha Tamaa pia kuona Serikali iko 'busy' na Miradi tu huku Wananchi wake wakiteseka na kutokuwa na Vipato, uhaba wa Ajira na Kuishi kwa Matumaini pekee hali imayopelekea hata kuharibu Saikolojia zao ( zetu ) na wengine hata 'Kujitundika' ili Wafe wakayaanze Maisha mapya huko Udongoni ( Mavumbini )

Najua Rais wa Awamu ya Nne Mzee Jakaya Mrisho Kikwete ( nae alikuwa na Mapungufu yake fulani fulani ) ila nakuomba tu Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan usione Aibu 'Kuchota' Mawazo yake hasa katika Suala zima la Watanzania wanataka nini na hiyo Miradi yako uiendeshe vipi.

Mheshimiwa Rais Mama Samia namalizia tu kwa Kukuuliza Swali nimekusikia leo ukisema kuwa Janga la Corona ndiyo limesababisha usipandishe Mishahara ila Mwakani utapandisha.

Je, Wewe ni Mfalme Njozi ambaye umeshajua kuwa Mwakani ( 2022 ) hakutakuwa na Janga lolote ama Tanzania au Duniani kwa Ujumla? Je, kukitokea Janga lingine Kubwa tena tutegemee Mei Mosi ya 2022 utakuja tena na Kauli hii ya Matumaini Kwetu au utakuwa umeshakusanya Pesa za Kutosha na kwamba hata kutokee nini Wafanyakazi ( Watumishi ) nyongeza zao za Mishahara utakuwa umeshaitenga?

Tusitumie Janga hili la Corona kama Kimbilio letu Kuu la 'Utetezi' kwa Wananchi wa Tanzania wakati wenye Akili tunajua kuwa wale 'Corrupt Players' wote waliotajwa katika Ripoti ya CAG na sababu zangu hizo Saba ( 7 ) hapo juu ndiyo Chanzo cha yote na Ugumu huu wa Maisha ya Watanzania na Kushindwa mara kwa mara Kupandisha Mishahara.

Acha Kauli za Kisiasa zitakuharibia sana.
 
Hivi kwa mshahara wa 600000/= kwahyo PAYE 1% hapo inaongezeka kama ngapi?
 
Ndugu mfanya kazi haupo kwenye hilo ongezeko la 1%, inawahusu waliopo 270k had 540k ambao walikua wanakatwa 9% sasa watakatwa 8% kwa maelezo ya rais, vinginevyo tusubir ufafaniz kutoka tra labda.
Hivi kwa mshahara wa 600000/= kwahyo PAYE 1% hapo inaongezeka kama ngapi?
 
kuna komenti aliitoa Slowly jana nikamuelewa sana.

zile pesa alizozipiga kigwanomics zinatosha kunipa mimi maisha mazuri mpaka kufa.
 
Back
Top Bottom