Nitampataje mume mwenye vigezo hivi?

Nitampataje mume mwenye vigezo hivi?

Susy tunasubiri majibu mamii?:laugh::laugh::laugh::roll:
 
Huyo wa kwenye mtandao hayupo! Muombe Mungu akupe wa chaguo lake maana yeye anakujua vizuri zaidi kuliko unavyojijua. Mfano ukipata type unayodhani ndio saws inaweza kupelekea ukamsahau Mungu hata jumapili huendi kanisani. Au ambaye Hana kitu mkatafuta pamoja Kwa hila na dhuluma mkawa mnajitengenezea njia ya kwenda Kwa ibilisi. Inawezekana wachumba wanakuzunguka wengi Ila unachagua
mno. Hakuna short cut ni kuomba Kwa kusali na kufunga bila kumpangia Mungu kuwa awe Fulani
 
Jamani huyo Suzy amepata ndo wako busy ametutosa mapambe janvini?
 
Hongera sana,huo ni uamuzi wa busara.Mwombe mungu tu usikutane na mume maslahi
 
Omba mungu wengine wamo humu walikuw wanataka wake labda watakupm maana wakishaweka tangazo tunakuwa hatujui kama wamefanikiwa au vipi maana hawarudi kutujuza
 
Wapendwa nawasalimu!!

Ninatumai kila mtu ana sifa za ama mke au mume anayemtaka, rafiki zangu wa JF, napenda sana nipate mume mwenye vigezo hivyo hapo nilivyovitaja lakini kila siku imekua kinyume kabisa na matarajio yangu.

1. Awe Mkirsto
2. awe mweupe
3. awe na feature ya maisha, kwani fedha hutafutwa
4. awe mrefu wa wastani
5. kuanzia miaka 30 kuendelea

Dada yangu alishawahi kunitania kuwa eti niwatongoze wale ninaowapenda na nikitu ambacho siwezi hata kujaribu kufanya. Jamani nisaidieni au ndio niendelee kusubiri ubavu wangu kutoka kwa Mungu?

Naombeni mawazo yenu, pengine nafikiri hadithi za kujenga magorofa hewani.

Ukimpata mwenye 3/5, chukua!!, alafu hizo 2/5, kazi kwako kumjaliza!
 
My gosh!.......... Am so unlucky.
Hii mambo ya kuwa busy kule siasa si unaona mpaka nakosa mchumba.

Ngoja kwakuwa ni wewe kijana wa nyumbani,nitafikiria kukutanisha tena recruitment team ili tuweze kuona kama unaweza kuwa mwenzi!!:laugh:
 
Wapendwa nawasalimu!!

Ninatumai kila mtu ana sifa za ama mke au mume anayemtaka, rafiki zangu wa JF, napenda sana nipate mume mwenye vigezo hivyo hapo nilivyovitaja lakini kila siku imekua kinyume kabisa na matarajio yangu.

1. Awe Mkirsto
2. awe mweupe
3. awe na feature ya maisha, kwani fedha hutafutwa
4. awe mrefu wa wastani
5. kuanzia miaka 30 kuendelea

Dada yangu alishawahi kunitania kuwa eti niwatongoze wale ninaowapenda na nikitu ambacho siwezi hata kujaribu kufanya. Jamani nisaidieni au ndio niendelee kusubiri ubavu wangu kutoka kwa Mungu?

Naombeni mawazo yenu, pengine nafikiri hadithi za kujenga magorofa hewani.

Wewe mbona vigezo features zako hujaweka, wewe una kipi hasa cha zaidi mpaka uwe na power ya ku-dictate vigezo wakati wewe hujatuambia ukoje, una umri gani? elimu? etc
 
kabila? una mgongo? mimi hizo sifa ninazo lakini mgongo na paja la haja lipo?
 
Back
Top Bottom