Nitawadharau Yanga mkicheza mechi itakayopangiwa tarehe nyingine dhidi ya Simba

Nitawadharau Yanga mkicheza mechi itakayopangiwa tarehe nyingine dhidi ya Simba

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Eng Hersi na bodi ya timu yetu ni viongozi makini na nawaheshimu sana

Kituko cha Leo Simba kususia mechi,

Naona kanuni ziko wazi na zipo upande wa Yanga

Kwa vyoyote vile mechi haikupaswa kuhairishwa na bodi ya ligi
Hapa wamefanya uhuni

Simba hawakutoa taarifa Kwa management ya uwanja kuwa Kuna ujio wao,

Simba hawakutoa taarifa Kwa mwenyeji wa mchezo ambaye ni Yanga kuwa wangekuja kufanya mazoezi
Muda waliowasili ilikuwa usiku, walitakiwa watoke taarifa ili taa za uwanjani ziwashwe maana uwanja wa Taifa kama hamna mechi wala shughuli yoyote Huwa Kuna Giza

Sasa tunajiuliza Simba walitaka kufanya mazoezi gizani na kutumia tochi za simu😅

Hakuna Kiongozi wa Yanga wala mwajiriwa wa Yanga alikuwa pale

Soma Pia: Yanga, yasema mchezo dhidi ya Simba upo palepale hakuna mabadiliko yoyote

Yanga hawamiliki njia za umeme ili kuwapa mwanga Simba

Yanga nawasihi bodi ya ligi wakiwa mazwazwa wapelekeni CAS

Kule coach wa Stars Amrouch na Samwel Eti waliishitak CAF na wameshindwa na CAF imeamuriwa kuwalipa mamilion ya dollar

Kama watu binafsi wanaishtaki taasisi kama CAF na wanashinda na kupata fidia Yanga mnaogopa nini?
 
Tarehe ya mechi itapangwa na mgeni rasmi atakuwa Samia.

Tuone hao viongozi wako ambao kimsingi ni chawa wa CCM unao wa pressure kususia mechi kama watakuwa na mikazo ya kumgomea mwenyekiti wao.
Ndo nimesema nitawadharau
Haiwezekani Simba wafanye uhuni halafu Yanga waandae timu mara mbili kucheza mechi 1
 
Ndo nimesema nitawadharau
Haiwezekani Simba wafanye uhuni halafu Yanga waandae timu mara mbili kucheza mechi 1
Kama unataka kuwadharau basi anza tu saizi kwasababu there's no way Gongowazi anaweza kuweka mikazo kususia mechi.

By the way sisi tumekuwa tukiidharau tangu mwanzo mlikuwa mnatuona haters sasa naona taratibu mnataka kuungana na sisi.

Imebaki sehemu moja tu ya nyie kuungana na sisi, kwenye hoja ya kwamba mashabiki wa Gongowazi wengi ni hamnazo.

Hili nalo sijui utaendelea kubisha hadi pale siku isiyokuwa na jina itapofika na wewe mwenyewe kukiri kama ulivyofanya leo.
 
Mashabiki wa mbumbumbu na viongozi ndo hamnazo
5imba wanakimbia mechi kama watoto wa shule
Hakika Rage alikuwa sahihi kuwaiteni mbumbumbu
 
CCM Ndio inapenda vijana Wa Tanganyika waweke nguvu zao huko kwenye simba Na YANGA".

Great Thinker
.

Leo Tutaona Nyuzi za Simba na Yanga zaidi ya elfu 60 humu jukwaani.

TUKIWAAMBIA KUSHABIKIA SANA SIMBA NA YANGA MNAANZA KUWA WA PUMBAVU HAMUELEWI
 
Kama Morrison aliwashinda kesi CAS na bado mkaja kumsajili tena, ulishindwa kuwadharau kipindi hiko kwa hili utawaonea na mtajionea wenyewe.

Uwezo wenu mdogo sana katika masuala mtambuka ya mikataba na kanuni za football.

Refer Manara alivyosema wenye akili wangapi vile?
 
Kanuni za bodi ya ligi zinasemaje wadau ikiwa timu A inasusia mechi kisa hawakupata uwanja wa kufanyia mazoezi?Je timu pinzani inafidiwa au na bodi ya ligi haina meno ya kuzuia mambo hauo ya sintofahamu
 
We umeanzisha thread kibao kwenye hili jambo, yaan Kuna watu kumbe hizi timu hamzijui mnashabikia kizwazwa tumesema tangu jana hii mechi haipo wazee wa bahasha wameshupaa
 
Baada ya kupiga hesabu zao, wakaona watafute tu kisingizio!

Kuanzia kukosekana kwa wachezaji wao muhimu kwa sababu ya majeraha, halafu mwamuzi ni yule jamaa asiye endekeza bahasha!! Wakaona wazi hali itakuwa ni mbaya! Jibu jepesi likawa ni kuuweka tu mpira kwapani.
 
Ndo nimesema nitawadharau
Haiwezekani Simba wafanye uhuni halafu Yanga waandae timu mara mbili kucheza mechi 1
Anza kuwadharau mapema tu maana hilo ni 100% mechi itachezwa na mtaleta timu
 
Baada ya kupiga hesabu zao, wakaona watafute tu kisingizio!

Kuanzia kukosekana kwa wachezaji wao muhimu kwa sababu ya majeraha, halafu mwamuzi ni yule jamaa asiye endekeza bahasha!! Wakaona wazi hali itakuwa ni mbaya! Jibu jepesi likawa ni kuuweka tu mpira kwapani.
Haya mkuu nyie mliofika mtapatiwa points zenu 3 ns magoli 3
 
Kanuni za bodi ya ligi zinasemaje wadau ikiwa timu A inasusia mechi kisa hawakupata uwanja wa kufanyia mazoezi?Je timu pinzani inafidiwa au na bodi ya ligi haina meno ya kuzuia mambo hauo ya sintofahamu
Mtafidiwa na mabaunsa wenu mliowajaza uwanjani siku moja kabla ya mechi
Bodi imeghairi mechi so technically hakuna aliyegomea mechi
 
Back
Top Bottom