Nitawashangaa BASATA wasipomfungia ZUCHU hata miaka mtano kwa Uchache

Kusema ukweli Msanii wa Bongo Fleva ambaye leo Tar 5 Machi 2024 amefungiwa kujiahughulisha na kazi za Sanaa ktk Nchi ya Zanzibar na viunga vyake amekoswea sana.

Ndani ya Kisiwa cha Zanzibar Rais Mwinyi na Viongozi wenzake wanafanya kazi nzuri kuhakikisha anawaletea maendeleo wananchi na kupambana na hatari ya tabia mbaya za kudhalilisha watu kijinsia ikiwemo ulawiti, ubakaj, uzinzi na liwaati.

Sasa inapoonekana Msanii ambaye ameaminiwa na jamii kuonekana kuwa kinara kwenda kinyume na Jitihada za Taifa hasa kwenye Swala la maadili basi hatua kali zinapaswa kuchukuliwa.

Baraza la Sanaa la Zanzibar limechukua hatua madhubuti japo bado naona Adhabu ni ndogo.

Nitoe wito kwa Baraza la Sanaa Tanzania kuwa kinara na mfano bora kutoa usimamizi juu ya ustawi wa Mila na desturi zetu Watanzania.

Hala hala Basata tunasubiri hatua zenu ili na wasanii Wengine wajifunze.

Sanaa Zetu zijikite kuleta burudani, kuhamasisha vijana kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu viongozi ktk familia, Jamii na Taifa kwa ujumla.

Sanaa inayohamaisha watu kujikwamua na kujikomboa kifikra na kupambania haki za binadamu wengine.

Sanaa ijiepushe kuhamasisha Ngono, Ulevi, uvivu, bata, matusi na ushoga.
Kafanyaje?
 
Kwaiyo ww umeshindwa kwenda kanisani msikitini kujifunza maadili unataka wasanii ndo wakufunze maadili
Kwaiyo unataka wasanii ndo wakuhamasishe kufanya kaz kwa faida yako

Maadili kafundishwe na familia yako , ukoowako ,kabila lako na dini yako ila wasanii waache watoe burudani
Afu maadili ni nn ww kwako unaweza ona kitu flan ni maadili ila kwangu yakawa sio maadili
Maadili hutokana na mazingira

Afu uko nzenji ndo mashoga kibao na mashoga weng utoka zenji mazani wangekua wanajali maadili na kuyaheshimu bas kusingekua na mashoga
 
Huyu alitakiwa afungiwe maisha maana hili sio Onyo lake la kwanza kipindi kile katukana Hadharani BASATA wakamsamehe..
BASATA wanalea Majipu yakiwa vidonda ndo wanalalamika..

hakupaswa kusamehewa kwa kosa hili
View attachment 2925138
Anapenda sana hio michezo huyo mtoto alafu ndio lugha zao huko usafini sasa wakifika kwenye Media wanajisahau km wapo mbele ya camera sijui wanakua washapasha ubongo
 
Kusema ukweli Msanii wa Bongo Fleva ambaye leo Tar 5 Machi 2024 amefungiwa kujiahughulisha na kazi za Sanaa ktk Nchi ya Zanzibar na viunga vyake amekoswea sana.

Ndani ya Kisiwa cha Zanzibar Rais Mwinyi na Viongozi wenzake wanafanya kazi nzuri kuhakikisha anawaletea maendeleo wananchi na kupambana na hatari ya tabia mbaya za kudhalilisha watu kijinsia ikiwemo ulawiti, ubakaj, uzinzi na liwaati.

Sasa inapoonekana Msanii ambaye ameaminiwa na jamii kuonekana kuwa kinara kwenda kinyume na Jitihada za Taifa hasa kwenye Swala la maadili basi hatua kali zinapaswa kuchukuliwa.

Baraza la Sanaa la Zanzibar limechukua hatua madhubuti japo bado naona Adhabu ni ndogo.

Nitoe wito kwa Baraza la Sanaa Tanzania kuwa kinara na mfano bora kutoa usimamizi juu ya ustawi wa Mila na desturi zetu Watanzania.

Hala hala Basata tunasubiri hatua zenu ili na wasanii Wengine wajifunze.

Sanaa Zetu zijikite kuleta burudani, kuhamasisha vijana kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu viongozi ktk familia, Jamii na Taifa kwa ujumla.

Sanaa inayohamaisha watu kujikwamua na kujikomboa kifikra na kupambania haki za binadamu wengine.

Sanaa ijiepushe kuhamasisha Ngono, Ulevi, uvivu, bata, matusi na ushoga.
ayo matusi yame anza kuimbwa na Zuchu ?
 
Back
Top Bottom