Nitazidi kuongea hata kama mkiniita tapeli

Nitazidi kuongea hata kama mkiniita tapeli

Nipo sekta ya innovation na uzalishaji

Unaniuliza kuhusu Financial Markets najua kiasi changu,zaidi unajua wewe

Sitaki Forex wala Bitcoin kwa sasa

Usinilazimishe

Wewe pia hujui chochote kwenye sekta yangu ya innovation and manufacturing,ila sikulazimishi uje huku

Nyie mnafungua mauzi kila siku mnataka watu waje huko eti kuna pesa sana,mtu hataki yanini unamfungulia uzi kila siku?

Wewe umepata hela sana,tuzione basi!

Huna
Mkuu kwani unalazimishwa kusoma hizo nyuzi,? kila kitu kina audience au wateja wake! Usilazimishe misimamo yako iwe sawa kwa wote
 
Nipo sekta ya innovation na uzalishaji

Unaniuliza kuhusu Financial Markets najua kiasi changu,zaidi unajua wewe

Sitaki Forex wala Bitcoin kwa sasa

Usinilazimishe

Wewe pia hujui chochote kwenye sekta yangu ya innovation and manufacturing,ila sikulazimishi uje huku

Nyie mnafungua mauzi kila siku mnataka watu waje huko eti kuna pesa sana,mtu hataki yanini unamfungulia uzi kila siku?

Wewe umepata hela sana,tuzione basi!

Huna
Nani kakulazimisha.. acha kuendelea kuwa kuenyesha ujinga.. muite hata mwanao kama unaye.. akusaidie kusoma uzi kwa mara nyingine halafu umuulize kama kuna mahali, mtoa mada amelazimisha watu..

Usiwe mjinga ukapitiliza..
 
Mkuu kwani unalazimishwa kusoma hizo nyuzi,? kila kitu kina audience au wateja wake! Usilazimishe misimamo yako iwe sawa kwa wote
Na anasema haelewi vema kuhusu financial markets ila nashangaa anajeuka kuwa msemaji..
 
Mentality ya watu tayar ipo corrupted.. yaani kuleta tu uzi wa aina hii.. kuna tayar wanadhani eti nataka kuwatapeli akati sijawaomba hata kumi..

Yaani watu hawaangalii upande wa elimu wanaangalia pesa na kutapeliwa.. ni mentality za kimaskini
Hiyo kwa lugha nyepesi inaitwa 'self defence'

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
embu niwekee link hapa na mimi nkafaidike na hizo network marketing, nisije nikawa nimezubaa nikapitwa na mambo
Wajina, hii sio network marketing.. kama unataka ku invest kwenye cryptos ingia google uisome kwanza uielewe
 
According to you. PERIOD
This is PRIMITIVE kilichobadilika ni platform inakofanyikia Hii issue ya electronic coins.

Hapo katikati kulikuwa na Mchezo wa Rupia ya mjerumani... Very clever scheme.. mtu anakuja Bushi ananunua pasi sijui ina alama gani na Rupia.

Mnunuzi anajifanya ameweweseka kwa alichokiona ..anadai kwa kuwa hela ni nyingi hana uwezo wa kulipa, anamuomba mwenye mali.. ambaye hajui hata thamani yake waelekee pamoja mjini wakamuone dealer Mkuu.

Wanafika kwa dealer, naye anaogopa mmh.. hii hana hela yake.. na biashara Hii mwiko uzurumaji.. 🙂 ila wapo wagiriki Nairobi wanaweza kabisa kununua. Hapo unakuta value inaongelea milioni 300 kwa coin.. 🙂 (matapeli sio Watu)

Mwisho kabisa unakuta coin imekosa alama moja tu au nukta imekosekana.. au mwaka haumatch basi mnarudi.. hapo mko hyped mnaanza kuisaka yenye mwaka unaotajwa.. 🙂

Mara mnasikia kuna mtu Sumbawanga anayo.. mnasafiri mnafika yeye anakuwa kauzu hana mpango na maujinga yenu ya safari kama mnataka mmpe hela.. 🙂

Anataja hata milioni 100 hapo ndio inakuja kama inakataa.. unakuta mzee kauza nyumba kwenda kununua coin ya mjerumani, mara pasi.. sijui sufuria 🙂 😀

Long story short Bitcoin ni kitu kile kile.. value ni perception... Na Watu wachache wanaweza wakaamua hata kinyesi cha kanga kiwe na value ..ukiwa Mjinga utajikuta unakimbilia kila utumbo wa kuku unaoanikwa...

Universally agreed upon system ipo.. kuliko kukaa unapoteza muda kumine Bitcoin.. mine information it's far more great and valuable than huo utumbo.

Na ulisha lipa 23000$ mkawa wengi somehow.. value inashuka mpaka zero unakuwa umepoteza kila kitu... Maana hizi coin haziko stable na hakuna system ya kucontrol hilo..

#Ushauri#
Utajiri uko sehemu mbili tu.. Either ukae kwenye supply side of money.. Banking and Insurance etc. Au ukae kwenye Assets.. where money is spent.. Industries, Real estate etc... Wengine wote hapa katikati wanacreate vallue for the two groups... ASSETS HOLDERS AND MONEY SUPPLIERS.
 
Yani jinsi bei ya bitcoin inavyozidi kwenda juu ndivyo majuto yanavyokuwa mengi kwa upande wangu natamani miaka irudi nyuma mpaka angalau 2019 February ila siwezi

Mwaka huu mkubwa kwa waliozichanga karata zao vyema kwenye hizi issue za cryptocurrencies wamepiga pesa nzuri tu.Kuna kitu wanaita DEFI & yield farming watu wameweza kupata pesa walizowekeza kwa zaidi ya 2000%

Nina majuto makuu ningejua ningeitoa kafara hata laki 5 niweke kwenye hays madude sasa hivi ningekuw na $5000 ama zaidi
 
Sio msimamo wangu pekee yangu,watu wengi unaochat nao hapa wote wana negative views with all these you are saying!

Kusema ni mimi pekee yangu unaonesha wewe sio honest opinion giver!

Uzi umekuja public,ni wajibu wetu public kuusoma na kuchangia bongo zetu zinavyotaka

Kama ulikua hutaki watu kama mimi tuchangie basi usingeuleta public hivi!

Kila kitu kina audience yake,hapa public audience ipo mchanganyiko,utapata views mchanganyiko,wewe ndio uvumilie majibu na sio public!
Tatizo lako kubwa wewe unataka kuwaaminisha watu kile unachofikiria wewe
 
Na wewe hulazimishi?

Mimi sijatoa uzi,mmetoa nyie!

Tuko hapa tunapambana kutoa ideas,best ideas win!

Wewe bwana,toa nondo tukuelewe,acha fujo!
Uzi sijautoa mimi pia lakini acha watu wawe impacted na knowledge, kwani kuna mtu kachangishwa pesa humu? Mbona zipo nyuzi nyingi pia humu zinatoa elimu mbalimbali kwa faida ya watu lakini hatuwaoni mkipinga, ila when it comes to Forex ,Cryptocurrency and digital currencies mnatokwa povu??

Guys relax this is where the world is heading. huwezi kuzuia mafuriko kwa kiganja cha mkono. Acheni watu wapate Elimu waamue wenyewe siyo kutanguliza Negative thinking.
 
Back
Top Bottom