Nitazidi kuongea hata kama mkiniita tapeli

Nitazidi kuongea hata kama mkiniita tapeli

Hapana,hapa umekuja na Forex na Bitcoin

Sana sana Forex....

Hii ya kutudanganya hapa eti "Financial Markets" kama yote ni uongo.....

Unaongelea FOREX tupu hapo....hakuna any other instruments za finances ambazo ni tradable ulizozungumza,acha uongo!

Forex thieves!
Mkuu wewe ni kichaa mpaka udanganywe? Kijana umejaa sumu kweli[emoji23][emoji23]
 
Nani na nani huu uzi ni msaada kwao na waliconfess kwako?

Wataje tuwajue na tuwaulize

Huna jina....

Hapa unaweza ongea lolote ukadhani tutapokea bila swali...lete majina ya hao walioona msaada wa huu none sensical thread!

taja majina yao!
Unataka kufahamu majina yao ikusaidie nini ? wewe elewa tu hivyo
 
Humu ndani ukizungumza habari za Forex na Bitcoin, unaitwa tapeli. Iteni mpendavo lakini lazima niwachangamshe akili kidogo.

Bitcoin moja leo imefika USD 23,000 ( Kama Tzs 53 Million.

Na tarehe 16 March mwaka huu 2020, bei ya bitcoin moja ilikuwa inauzwa kwa Tzs 11 Million, maana yake ni kwamba kama uliwekeza milioni 11 mwezi march, sahiv ungekuwa na faida kama Tzs 42 Million.

Yaani ungeweza kabisa ku postpone kununua IST na ukarisk kwenye bitcoin, ungekuta sahiv unaongelea kununua Ford Ranger!!.

View attachment 1652679

Anyway, lengo la uzi wangu sio kuwatia watu machungu, najua kuna matomaso hapa wataniuliza, wewe umetengeneza faida ya sh ngapi mpaka sasa..?

Lengo langu kwenye huu uzi ni kuwakumbusha kwamba, FINANCIAL MARKETS IS REAL..

Somewhere, someone is making good monies out of it, so sio vizuri kutukana hustlers wa kwenye bitcoin na forex.

Kama kitu hutaki, potezea kimya kimya.. ila usiwavunje watu moyo.

Hivo yani.
Kuna grouo lilianzishwa lakuwaketa watu na ushawishi wa kujiunga kwenye hii kitu Bitcon toka mwaka 2018 Wanagroup wamejikatia tamaa baada ya kuona hii kamari ni imani na sii uhalisia.
Wanagroup wameligeuza group kuwa la imani kwa Mungu na mahubiri kwa sana.
Ni afadhali imani iwe ni kwa Mungu aliye roho kuliko kuiweka kwa intelligencia ya binadamu aliye mwili usiotaka kujidhihirisha.
 
Hivi hizi habari za Forex badogo tu zina-trend huku JF?

Wabongo waambie kuhusu kulima matikiti pamoja na kuchoma mkaa.

Hizi fursa zilizopo kwenye digital world ukiwaambia akili zao zinawatuma kuibiwa tu.

Mbongo anaamini hili apate hela ni lazima avuje jasho na aumie kidogo.

Mbongo anaamini fursa pekee iliyopo kwenye internet ya kutengeneza hela ni kubet Kati ya Manchester United na Southampton.

Matumizi makubwa ya internet kwa mbongo ni kuangalia umbeya Instagram na matukio ya ajabu ajabu huko YouTube.

Ukimwambia mbongo hiyo simu yake ya kiganjani na laptop yake vinaweza kumfanya akawa millionaire, atakuona wewe ni mwendowazimu.

Hii Forex tuliipigia campaign Sana miaka ile kabla Sirjeff hajakimbia Hili jukwaa na tulikuja na solid evidences kwa kila kilichokuwa kinaulizwa na wale critics.

Leo nafungua huu uzi naona mambo bado ni yale yale tu, hofu na maswali ya kejeri.

Ukishawaelewa wabongo fursa Kama hii sio ya kuwashirikisha kihadhara, shirikisha watu wako wa karibu tu ambao wako open-ended, hawa wengine acha waendelee kulima.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Unajua ni kwanini wanahofu kuwa wanaweza kutapeliwa? Kwa sababu nchi kama Bongo hakuna mtu ''anayepigia debe'' tena kwa nguvu zote kueleza watu njia za kuwa matajiri. Unakuta mtu anatumia nguvu na muda wake kuwahisi watu wafanye jambo fulani eti watatajirika! uzoefu wangu unaonyesha watu wengi kabisa wakipata channel ya mchongo hutaka watu wengine wasijue hata kidogo na wapo tayari hata kufanya hujuma ili wengine wasijue. Sasa wewe huu wema umetoka wapi?
Kwanini usinichukulie kama economic activist? Kwani hawa wanaharakati ambao kwa mfano wanapigania haki kwa mfano za watoto ama haki nyingine zozote, wanapata nini in return?

Watu wengine, tunapenda tu kutoa elimu kwa watu... Hayo unayowaza wewe kwamba labda mtu ana hidden agenda, hiyo ni uamuz wako kufikiri..

Lakini pia ukipitia uzi mzima, kuna watu kibao nimewaelekeza wakavisome hivi vitu google ili kuvielewa zaidi.. Na kwenye huu uzi sijasema natoa training wala sijadai chochote.. sasa mpaka hapo kwanini watu mnadhani kwamba nna hidden agenda?

Yaani mtu kuwa mwema nayo ni suala la kuhoji? Wengine ndo tupo hivo
 
Kwaiyo hapa unataka kuzungumzia nini. Embu nipe uwelewa wako kwenye suala la kuuza na kununua au currency

Prediction zako ni zipi mpaka March mwakani kwenye BTC kana kwamba rate ya btc 1 itaendelea kupanda au huwenda ikashuka ?
Imeweza ku break USD20K ambayo ilikuwa ni prevuous all time high.. so possibility ni kwenda up..

Halafu ukumbuke watu wanakimbilia kwenye cryptos kwa sababu hii covid crisis ime trigger quantitative easing ambayo impact yake inaweza kushusha thamani za hizi fiat currency.. kwa hiyo watu ni kama wanaji protect kwa kuiveat kwenye cryptos
 
Hapana,hapa umekuja na Forex na Bitcoin

Sana sana Forex....

Hii ya kutudanganya hapa eti "Financial Markets" kama yote ni uongo.....

Unaongelea FOREX tupu hapo....hakuna any other instruments za finances ambazo ni tradable ulizozungumza,acha uongo!

Forex thieves!
Mbona nimesema wazi kwenye uzi, pitia tena kama hujaona mahali nimeandika " Financial market is real".. tatizo lako umeshachagua upande kwa hiyo sikulazimishi kufikiri vyovyote..waza chochote.. una uhuru wa kufanya hivo
 
Mkuu ungejaribu kujishughulisha kidogo maana google wamejibu maswali mengi uliyoyauliza, Jaribu kuitafuta elimu ya suala husika before hujaja public ku criticize, maana inaenekana kabisa wengi wenu mpo kupinga ilhali hamna hufahamu na suala husika
Tatizo kuna taarifa nyingi sana juu ya hili.. na nyingi zinashindwa kujibu maswali hayo! Sasa nikikutana na wataalamu kama ninyi.. natumia fursa kujifunza...

Value for money inaathiriwa na uhitaji.. na uhitaji unaviwango vinavyoweza kutoshea.. mfano hali isipobadilika kesho tukaamka na kukuta Dola inauzwa kwa sh. 7000 tutashangaa.. maana hiyo si tabia ya kawaida ya fedha..

Lakini wewe unataka sote tuwe matajiri.. na unajua majibu ya maswali yangu.. kwanini usinitafsirie!? Huenda ninasoma sielewi!? Na a true educated person can break a very complex theory into layman's Language..

Nivumilie mimi Mjinga wa Bitcoin...
 
Watu wengi wa Tanzania? Au unaongelea duniani??

Kwenye financial markets watu wakiwa wengi kwenye soko ndo efficient inaongezeka in terms of liquidity.

Ndo itakuwa vizuri kwa soko endapo kama watu wengi wakiwa wawekezaji
Kwa hiyo hawa unao shawishi mfano wawe 200 kati ya hao 195 wapigwe dola miamia nawee si unapata humo tukanwa tu mkuu mana upo kazini

Mana huwezi kuitwa tapali na bado umeganda tuu kushawishi ha ha ha
 
Kuna watu wanasema ninekuja kuwatapeli watu.. yaani kutoa taarifa tu kuhusu bitcoin ishakuwa nongwa

Kwanini usinichukulie kama economic activist? Kwani hawa wanaharakati ambao kwa mfano wanapigania haki kwa mfano za watoto ama haki nyingine zozote, wanapata nini in return?

Watu wengine, tunapenda tu kutoa elimu kwa watu... Hayo unayowaza wewe kwamba labda mtu ana hidden agenda, hiyo ni uamuz wako kufikiri..

Lakini pia ukipitia uzi mzima, kuna watu kibao nimewaelekeza wakavisome hivi vitu google ili kuvielewa zaidi.. Na kwenye huu uzi sijasema natoa training wala sijadai chochote.. sasa mpaka hapo kwanini watu mnadhani kwamba nna hidden agenda?

Yaani mtu kuwa mwema nayo ni suala la kuhoji? Wengine ndo tupo hivo
Ndiyo nikakuambie kuwa wema wa kuwafunulia fursa wengine hapa Bongo hauko. Nazungumza kutokana na uzoefu wangu. Japokuwa wewe unaweza kudhani unafanya hivyo kwa ajili ya ''wema wako tu'' lakini nakuhakikishia sivyo (japo ni kweli kabisa unaweza usiwe na nia yoyote ya kumtapeli mtu). Kama una idea ndogo kwenye mambo ya psychology, mara nyingi mtu anapofanya jambo ambalo hana uhakika nalo atapenda sana kuwavutia wengine walifanye.... kwa kifupi ni ule usemi wa ''kifo cha wengi...'' (japo hata wewe unaweza usijue hilo bali subconscious mind yako ndiyo inakutuma)
 
Back
Top Bottom