Niukatae vipi mchepuko wa zamani?

Niukatae vipi mchepuko wa zamani?

okiwira

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2018
Posts
2,856
Reaction score
3,003
Moja kwa moja kwenye lengo la uzi.

Nipo ndoani miaka 7, miaka 3 nyuma nilikuwa na mchepuko ambao nilidumu nao miaka 3 baadaye mchepuko ukaja ukaolewa.

Tukapotezana hewani mwaka mzima sasa umerudi upo kwao hautaki kurudi tena kwa mumewe. Kabla haujaolewa tuliahidiana kuja kuzaa watoto wawili na ikiwezekana ulikubali uwe mke wa pili.

Sasa unadai kwa mume hauendi kamwee na anataka nizae mtoto hata kama sitaki kumuoa kwa sasa. Tangu amerudi sitaki kabisa kukutana naye faragha, SABABU KUU ni kuwa hawajaachana na mume wake hivyo bado ni mke wa mtu.

Mke wa mtu na mimi ni NYEUSI NA NYEUPE.

Mliyowahi kukutwa na masaibu ya mahusiano ya aina hii mlijivuaje?
 
Hua nashangaa sana hivi mwanaume unashindwaje kumuacha mwanamke?, Unamuonea huruma au unaogapa atakuharibia ndoa? Hebu kua mwanaume mkuu.

Pili inaonesha wewe ni hatari sana kwenye haya mambo na ulianza ukiwa bado hujakomaa kiakili, 25 years upo kwenye ndoa miaka 7, na mchepuko ulikua nae kwenye mahusiano kwa miaka 3 na ukapotezana nae mwaka mzima baada ya kuolewa, aseeh hebu kua kwanza maana bado una mengi ya kujifunza.

Man up
 
😆😆😆jibu lilijibiwa kulingana aina swali lilivyokuja.

Achana NA NAMBA HIZO😆😆Mwamba
Yaani swali lije kivyovyote vile mwamba..!! Kama kwa sasa una 25 years, na umekaa kwenye ndoa kwa miaka 7 hadi sasa, basi, ulipotimiza 18 years uliowa..!!!
 
Yaani swali lije kivyovyote vile mwamba..!! Kama kwa sasa una 25 years, na umekaa kwenye ndoa kwa miaka 7 hadi sasa, basi, ulipotimiza 18 years uliowa..!!!
😆😆😆Hatujaelewana bila shaka!!

Unazani kwanini aliuliza vile?

Na mwisho akanipa SULUHU YA SWALA LANGU?

Piga hatua walau mbili katika swali lake ndipo nilipomjibia🙏
 
Achana nae utakuja kujuta. Focus na familia yako moja.
Asante sana Demi njia rahisi namuoondoaje.

Kumwambia akae mbali namimi kwake ni kama nyimbo nzuri masikio mwake.
 
Back
Top Bottom