Niulize chakula chochote nikupe dondoo ya namna ya kuandaa!!

Niulize chakula chochote nikupe dondoo ya namna ya kuandaa!!

malisak

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2006
Posts
694
Reaction score
775
Kama unapenda kufahamu kuhusu vyakula mbalimbali na hujui namna ya kuviandaa njoo kwenye uzi huu uliza nitakujuza kwa wakati.
 
Kama unapenda kufahamu kuhusu vyakula mbalimbali na hujui namna ya kuviandaa njoo kwenye uzi huu uliza nitakujuza kwa wakati.
Seafood platter

1692110147684.png

1692110151525.png
 
Kakutana na KO ili jibu awezi kurudi

BTW
Kuna ile mboga ya mayai na nyanya wanapikaje?
Chapati za nyama je??
Mahtaji:
Nyanya 2
Mayai 4
Kitunguu maji 1
Hoho 1/2
Karot 1

Maandalizi

Pasua mayai weka kwenye kibakuli koroga mpaka yachanganyike vizuri ongeza chumvi kisha uandae jiko kwa ajili ya kupika mayai.

Weka sufuria jikoni ongeza mafuta kiasi yakichemka ongeza kitunguu maji, kikiiva weka hoho na karoti na ukoroge mpaka ziive kisha ongeza nyanya na ufunike ziive.

Zikiiva na kuchemka vizuri ongeza mayai yako, yaache baada ya dakika mbili na uanze kuyakoroga, rudia kuyakoroga kila baada ya dakika mbili mpaka utakapoona yameanza kutengeneza vidonge vidogo vidogo.

Funika kwa dakika 5, baada yapo mboga yako ipo tayari kwa kula na ugali au wali au kama kitafunwa cha chai.
 
Kisamvu cha karanga
Mahitaji

  • Majani ya kisamvu
  • Karanga nusu kikombe
  • kitunguu kimoja
  • nyanya mbili
  • karoti moja
  • mafuta na chumvi kiasi
Matayarisho

1. Osha kisamvu chako vizuri kisha katakata vipande vidogo vidogo

2. Unaweza kutwanga kwa kutumia kinu au kuchemsha kidogo na kisha kusaga kwa kutumia mashine. Ukitumia mashine uwe makini usije ukasaga sana ukaharibu.

3. Kaanga karanga kidogo na kisha zisage ziwe unga unga.

4. Chemsha kisamvu chako hadi kiive.

5. Katakata kitunguu, karoti na na nyanya

6. Anza kuunga kisamvu kwa kukaanga vitunguu, weka karoti na kisha nyanya na vikishaiva weka kisamvu na koroga pamoja kisha weka karanga. Acha vichemke kwa muda na unaweza pia weka na nazi tui la kwanza.

7. Baada ya muda mfupi epua na kitakiwa tayari. Waweza kula kwa ugali, wali, chapati, makande n.k

Enjoy.

NB: Kumbuka kubakiza kidogo maana kisamvu kikilala kinakuwa kitamu zaidi na ubwabwa uliolala weeee
 
Kakutana na KO ili jibu awezi kurudi

BTW
Kuna ile mboga ya mayai na nyanya wanapikaje?
Chapati za nyama je??
MAHITAJI PISHI LA CHAPATI ZA MAJI

.Unga wa ngano nusu
.Mayai mawili
.Maziwa vijiko viwili vya chakula
.Chunvi robo kijiko cha chakula
.Caroti
.Blueband nusu kijiko cha chakula

NJIA
.Chukua chombo safi weka unga kisha weka maji ya uvuguvugu kisha changanya kwa kukoga
.Weka mayai kisha endelea kukoroga kisha kwangua karoti kiasi chamganya pamoja
.Weka chunvi kiasi kisha koroga ili kupata mchanganyiko mzuri,Baada ya hapo mchanganyiko wako utakuwa tayari
.Chukua kikombe au kijiko kikubwa chota size ya chapati unayohitaji kisha choma[kaanga]pande zote mbili,Pika hadi umalize uchanganyiko wote uliyoandaa
 
Back
Top Bottom