Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Chuma majani yake saizi ya kiganja chako uyaoshe, alafu chemsha maji kikombe kidogo yakishachemka tu epua alafu dumbukiza humo hayo majani ukae kana dakika mbili utaona maji yanakuwa na rangi ya chungwa. Kunywa hayo maji kisha tafuna na hayo majani umeze... Siku mbili tu hata kama ulikuwa unaumwa utajisikia sawa. Inakuwa kama muujiza lakini ndio kweli
 
Ww nenda kaombewe,hizo nguvu za giza na sio ugonjwa tena simama hasa kwenye maombi
 
Misuri ya mgongoni na ganzi mikononi pamoja na miguuni..yaani mama akitembea hatua 50 lazima aweke kituo kupoza miguu.. Naombeni tiba ya hili
Pole sana kwa Mama! Unapswa kuhakikisha mama amepata vipimo ili tuweze kumpa ushauri sahihi kulingana na vipimo vya kitaalamu.
Pamoja na hilo,kwa uzoefu wangu katika vipimo na tiba za mimea mara nyingi matatizo hayo huambatana na msingi wa tatizo kwenye moyo.

1.Inaweza kuwa mishipa ya damu kwenye moyo imesinyaa na hivyo kusababisha changamoto kubwa wakati wa usukumaji damu na reflection yake anaipata kupitia maumivu kwenye hizo sehemu za mgongo,maeneo ya shingo na hata wakati mwingine maeneo ya kifuani.Hiyo ganzi sehemu za mikono na miguu maana yake kuna changamoto ya ufikaji wa damu maeneo hayo kwa kipimo na wakati sahihi.
2.Inaweza kuwa ni matatizo katika pingili za mgongo,hivyo baadhi ya neva zimeathirika na hivyo kusababisha hali inayompata.

Hakikisha mama anapata vipimo vya kitaalamu ili kubaini tatizo lake.

Matatizo yote hayo yanatatulika.Fuatilia kuna somo niliweka hapa namna ya kuandaa Tonic.Hiyo Tonic akiitumia kwa muda wa wiki moja lazima hali hiyo itabadilika tu na atapata unafuu mkubwa.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kuna watu hasa wasomi,na wenye Imani za Dini tofauti, huwa wanachanganya tiba za asili za na Uganga wa Uchawi, naomba leo nieleze kidogo kwa ueleo wangu mdogo,

Kwanza utamjuaje mganga wa Mungu,na Mganga mshirikina wa shetani,

Mganga mshrikina wa shetani unapofika ofisini kwake utakutana na vitu vifuatavyo, ngozi za wanyama,mikia ya wanyama,vinyago vya wanyama,ngoma na vitamba vya rangi nyeupe na nyekundu.na hupenda kukwambia maisha yako ya baadaye, au kukwambia mambo yaliyojificha kama sijui anakuloga nani?na Mengine.Anayejua mambo ya kesho ni Mwenyezi Mungu peke yake,

Mganga wa kweli anatasikiliza shida zako,atakupa dawa, zisizokuwa na masharti yoyote yale
 
Shukrani Sana kwa maelezo mazuri hakika nimekuelewa vema ,,je baada ya tiba anaweza kunyooka Kama mwanzo maana kwa Sasa amepinda yaan hatembei akiwa mnyoofu??
Na je wapi naweza kupata vipimo kwa kwa upande wako?
 
Sisi wasambaa mashona nguo ni mboga tamu sana tunaita mbwembwe
 
Pole sana!
(Blood viscosity
Vascular resistance
Cholestrol) Haya ninmiongoni mwa matatizo yaambatanayo na shida katika moyo. Maana yake unaweza kuwa na shida ya mishipa yako ya damu inayosababisha mzunguko wako wa damu kutokuwa mzuri.Ndiyo maana ukifanya mazoezi hali inakuwa nzuri kukiko ukikosa mazoezi.Watu wengi sana wana shida hizi bila kujijua na dalili ni zilezile unazoainisha hapa.Bahati mbaya sana hata katika hosp zetu imekuwa ngumu kubaini labda utembelee hosp kubwa zenye wataalam wa hali ya juu. Andaa Tonic juice yako kama nilivyoelekeza katika uzi wangu uliopita utumie baada ya mwezi leta mrejesho hapa.

Lakini pia kama unaweza kupata mmea wa Mkundekunde na mwembe pori.Unga wa mizizi yake unautumia katika maji ya moto kila siku kwa siku 21.Hiyo itakusafisha mishipa yako ya damu vizuri kama bomba la maji lililozibuliwa baada ya kuziba.



Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Shukrani Sana kwa maelezo mazuri hakika nimekuelewa vema ,,je baada ya tiba anaweza kunyooka Kama mwanzo maana kwa Sasa amepinda yaan hatembei akiwa mnyoofu??
Na je wapi naweza kupata vipimo kwa kwa upande wako?
Mitishamba/Mimea ni hazina kubwa na ina maajabu mengi.Hutibu yanayoonekana na yaliyo sirini. Kikubwa sisi binadamu tunahusika tu lakini mponyaji ni Mungu.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kunywa marobaini iliyochemshwa jioni ikapoa unywe alfajiri mwili wote utatikisika

Mwarobauni ni dawa ila sijui unatibu nini
 
Kichaa hicho wahi milembe
 
Pole sana.Huu siyo ugonjwa sugu tena bali ni tatanishi maana kwenye kipimo hauonekani.Kuna mimea inaweza kukusaidia sana lakini changamoto ni Lugha ya pamoja( kiswahili).Naifahamu kwa lugha yangu ya Kisukuma.Kama unaweza kuelewa nijulishe.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Yapo nyumbani kwangu yananisumbua huwa nayakata hapa naandika reply nipo sehem yalipo bado machanga ngoja yatoe mbegu niyafanyie
 
Dawa ya pumu mtoto wangu inamtesa Sana
 
Habari members

Hongera kwa topic nzuri Baba Vladmir na wachangiaji wengine.

Mama yangu anasumbuliwa na mgongo na ikampelekea kutembea kuwa tabu, hospital vipimo vilionesha disc za mgongo zimesagika na kufanya pingili za mgongo kusuguana, Daktari akamuambia afanye mazoezi na kuandikiwa dawa za maumivu na ganzi na kupewa magongo ya kutembelea. Toka apate changamoto ya kutembea ni miezi minne sasa.

Anaendelea na mazoezi lakini hali yake haitengemai na maumivu kuna siku yanakuwa makali haswa akisimama.

Msaada tafadhali wa dawa kwa tatizo lake. Na mbarikiwe wote.
 
Atapona moja kwa moja au kila akijisikia vibaya tunatakiwa kumpa Tena?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…