Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Mkuu kuna wale wanateseka na bawasiri kwa muda mrefu sana, ni dawa gani ya kutumia

Sent using Jamii Forums mobile app
Tafuta mmea unaitwa mjafari,chimba mizizi yake(Nilishawahi kuuandika hapa) kwangua maganda ya mizizi yake vizuri na uyaanike sehemu isiyokuwa na jua kali ili kutokupoteza ubora wake (mzizi wake ni mkali,ladha ya tangawizi na uchungu mkali ndani yake).Baada ya kukauka vizuri,tafuta sufuria uikaange mpaka iingue kama mkaa,baada ya hapo saga vizuri uwe unga mweusi kama wa mkaa.

Tafuta kuna nta ya miti inaitwa DEMOAI ukiingalia vizuri inafanana na asali ikiwa kwenye chupa,ni maarufu kwa jina hilo bila shaka ni kimasai maana wao ndiyo wanaiuza sana,ingawa wanaichakachua kwa kuiongezea mafuta ya kula ili iwe nyingi kwa hiyo inaathirika na kutokuwa na ubora unaotakiwa,kama unaweza kupata pure kabisa ni jambo jema.Hii inapatikana kwenye mapori ya Morogoro,Arusha na hata pwani kidogo,lita moja inaweza kuuzwa zaidi ya laki moja.

Chukua kiasi kidogo cha unga wako wa mjafari ulioundaa kama nilivyoelekeza ( nusu kijiko kwenye kiganja) changanya matone mawili ama matatu ya nta (DEMOAI) changanya vizuri ichanganyike tayari kwa kupaka sehemu yenye tatizo.
Hakikisha unapaka mara mbili kwa siku.

Kama unakuwa na tatizo la kinyesi kigumu tumia matone yasiyozidi matatu ya nta hiyo (DEMOAI) kwenye kikombe kizima cha chai ukoroge vizuri kila siku asubuhi hutajuta tena kujisaidia huku ukitibu bawasili kwa mtindo huo wa kupaka.Sambamba na hivyo,unatakiwa upate dawa ya kunywa pia huku ukiendelea kupaka ili kutibu tatizo nje na ndani kwa pamoja.Kuna mti maarufu sana sisi wasukuma tunauita NSUHA( nilishawahi kuandika miujiza yake hapa) huu ni maalum kwa kutoa vimbe za aina zote mwilini unapochanganywa na aina nyingine ya mimea.Tengeneza unga wa mizizi yake na utatumia kijiko kimoja katika maji moto mara tatu kwa siku.


Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Tumia asali mbichi,paka eneo hilo lote sugua kama dk 10 acha ikaukiane hapo hapo, fanya hivyo mara 2 kwa siku,usiku ukienda kulala unapaka asubuhi unanawa,hakikisha nywele umenyoa
Asante sana kiongozi! Wacha nikatafute asali mbichi! Je ni asali ya nyuki gani!? wadogo au wakubwa!
 
UCHAWI HUU NA MASHETANI
 
Usimjibu mwenzako hivyo ukajiona labda wewe ni mzima,kumbuka kuna wagonjwa wapo vitandani miaka na miaka,Virema,Vichaa n.k,Siyo kwamba wamejitakia,wenda walikuwa na nguvu kama wewe,ni mitihani tu mwenyezi Mungu kawapa,ambayo hata wewe anaweza kukupa
Humu mitandaoni kuna watu wa ajabu mno!

Mtu anaandika mpaka unajiuliza maswali!
 
Jaribu kuongeza Kinga ya mwili utashangaa mapele yote YANAPOTEA KWA KASI.

Kula matunda kila siku, pamoja na kutumia vitunguu swaumu asubuhi na jioni kwa sababu vina antibiotic, antiviral na antifungal properties.

Yale madawa unayojipaka yatazidi kuua bakteria wazuri wa kwenye ngozi. ACHANA NAYO.

PIGA VITUNGUU SWAUMU KILA SIKU KWA MIEZI MIWILI USIPOPONA NAJIONDOA JAMIIFORUMS NAJITOSA BAHARINI.
 
Maelezo yako naona yanamaana mkuu maana kuna watu walisema labda nina magonjwa ya kisukari, lakini nilipima niko sawa, na wengine wakasema itakua neuropathy hivyo nianze dozi ya vitamin B, nayo haikunipa nafuu ya kudumu

Sasa hapa nakuelewa kwani nikishafanya mazoezi ndo Najisikia vizuri, tena mazoezi maalum... kama yoga na aerobic.
baada ya hapo nitashinda vizuri, ishu asubuhi Nikiamka!! hayo maumivu yananitesa mnoo.. Nakua mtu mwingine kabisa, hata mood yangu inabadilika, nakua sijiamini nachoka mwili hadi akili

Ngoja nijaribu hii mkuu
Shukrani
 
Sasa mkuu mwembe pori unakua tofauti na miembe hii ninayoijua kama maembe dodo n.k
Mwembe pori unafananaje?
Mkundekunde ni hizihizi kunde za mboga?

Natanguliza Shukrani
 
Nashukuru sana kiongozi, asante sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…