Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Misuri ya mgongoni na ganzi mikononi pamoja na miguuni..yaani mama akitembea hatua 50 lazima aweke kituo kupoza miguu.. Naombeni tiba ya hili
Pole mkuu kwa kuuguliwa.
Kuna namna 2;

1 Pondaponda magome/magamba ya mgomba mbichi,majani ya mlonge/mdongodo pamoja na mmea mmoja kwa Kijita unaitwa LILUMBA (ni jamii ya mikoko ila wenyewe kuna wakati unachomoza mizizi kutoka matawini kuelekea ardhini)( kwa Majita enzi zetu Walimu wetu walikuwa wakipendelea kutumia sehemu ya matawi yake km viboko maridadi sana kwa wasumbufu).
Mchanganyiko huo uloweke kwenye maji yenye ujazo wa kutosha kuoga.

Yakalishe eneo ambapo yanaweza kupatwa na baridi,yaweza kuwa upenoni mwa nyumba ama bafuni. Saa kumi na mbili kamili au kasolo robo asubuhi afanye kutumia huo mchanganyiko kwa kukanda eneo lenye shida.
Km ni miguu basi aikanyagishe ndani ya chombo chenye mchanganyiko huo huku akiwa km anajikanda na kutililisha maji yake eneo husika kwa muda usiopungua dakika 20.
Afanye hivyo tena mida ya saa mbili usiku kwa mchanganyiko uleule kwani kwa muda huu yatakuwa yamesha patwa na baridi kiasi.

Huo mchanganyiko anaweza kuutumia mara 6(siku 3) kutegemea na upatikanaji wa mimea hiyo.

2 Chukua majani ya mnyonyo (custor) mabichi,yachemshe kwenye maji ama yaning'inize karibu na moto mkali yapate joto haswa,yatumie kukanda sehemu ambapo misuli imekaza.

Fanya hivyo asubuhi na jioni mpaka utakapo pata ahueni.
 
Shukrani Sana Kiongozi
 
Ni mara moja kwa siku?
 
Mkuu Nina tatizo la kiuno kuuma Kama kuwaka moto hivi kwa muda,ambapo muda mwingine kinatulia lakina muda mwingine knauma hasa wakati nikiea nimekaa.
Mimi shida yangu ipo hapo ,na nimejaribu kupitia comment zote ili nione kama hili tatizo kama limetolewa ufumbuzi lakini wapu,mkuu Baba vladmir na wengineo kama mnaweza kusaidia kwa hilo naomba mtoe ufafanuzi
 
Mimi shida yangu ipo hapo ,na nimejaribu kupitia comment zote ili nione kama hili tatizo kama limetolewa ufumbuzi lakini wapu,mkuu Baba vladmir na wengineo kama mnaweza kusaidia kwa hilo naomba mtoe ufafanuzi
Maumivu ya kiuno ni dalili ya matatizo ama ishara ya tatizo katika sehemu mojawapo ya mfumo wa mwili.
1.Inaweza kuwa ni matatizo ya joint za mifupa( Arthrits).Joint zinasagana na kusababisha vimbe zinazopelekea naumivu makubwa sana.

2.Inaweza kuwa ni matatizo ya disc katika pingili za uti wa mgongo.Disc kucheza inapekekea maumivu makubwa ya neva ambayo hupelekea kiuno kuuma.

3.Inaweza kuwa ni dalili ya vijiwe kwenye figo.Hii nayo husababisha maumivu makubwa ya kiuno.

4.UTI sugu pia inaweza kuambatana na maumivu ya kiuno kwa wakati mwingine.

Unachotakiwa kufanya ni kuhakikisha unapata vipimo vikubwa kwa ajili ya kubaini tatizo.Nakushauri fanya X- rays ili uangalie mifupa na joint za kiuno pamoja na sehemu ya uti wa mgongo.Naamini utapata kisababishi ili uweze kupata suluhisho la uhakika.Kumbuka kujua ugonjwa unaokusumbua ni nusu ya matibabu.

Zipo dawa za mitishamba zinazotibu matatizo hayo ya mifupa na mambo yanakuwa vizuri kabisa.Mhimu fanya vipimo kwanza halafu leta mrejesho utasaidika vyema.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu nmekuwa nikisumbuliwa na UTI Sugu na nmejaribu Dawa mbali mbali za hospitali bila mafanikio ...hivyo nakuomba unipe mwongozo jinsi ya kuondokana na hili tatizo
Tumia majani ya mchai chai. Una chemsha na maji kias chochite unacho taka ila hakikisha mchai chai ni mwingi then kunywa glas 1x3 asubuh mchan na jion kama ni mtu wa pilika au unarza geuza kama maj ya kunywa ukipenda inadaidia kusafisha kabsa kibofu na mirija
 
Vp kuhusu nimonia,mapafu kuwasha na mbavu kubana na kukosa pumzi wakati wa mvua au baridi na misuli ya kwenye mbavu na mgongoni kuuma.Tiba ni nini Mkuu???
 
Nashukuru sanaa mkuu
 
Ahsante sana kwa ushauri mzuri ngoja niufanyie kazi nitarejea kuleta feedback
 
Vp kuhusu nimonia,mapafu kuwasha na mbavu kubana na kukosa pumzi wakati wa mvua au baridi na misuli ya kwenye mbavu na mgongoni kuuma.Tiba ni nini Mkuu???
Hii inabidi umpate mtaalamu ukae nae chini awe anakufuatilia hatua kwa hatua huku anakupa tiba hadi unapona, mama yangu anatibu Ila ni kwa watoto tu wenye tatizo km hilo ulilosema dawa anatengeneza mwenyewe home remedy sio za hospitali
 
Hii inabidi umpate mtaalamu ukae nae chini awe anakufuatilia hatua kwa hatua huku anakupa tiba hadi unapona, mama yangu anatibu Ila ni kwa watoto tu wenye tatizo km hilo ulilosema dawa anatengeneza mwenyewe home remedy sio za hospitali
[emoji120][emoji120] Umenena sahihi kabisa.Kuna Shida ni kwamba unakuta mtu ana tatizo linalomsumbua kwa miaka mingi,pengine zaidi ya miaka mitano na kuendelea halafu anataka apate kupona ndani ya wiki moja.Tunapata changamoto sana.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…