Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Naomba maelezo kuhusu Ubuyu!
Chukua ubuyu wa unga, hata wa vipeke,tia ndani ya chupa ya lita 1.5 au jagi, jaza maji, kunywa mda wote, ubuyu uwe kama vikombe viwili vya chai yani
Mungu ndiye mjuzi zaidi
 
Thyroid dawa yake nin hypothyroid na hyperthyroid nasumbuliwa na hii kitu
 
Vilevile kwa Mtu anayesumbuliwa na Presha ya kupanda tumia Vitungu swaumu au Ubuyu,

Chukua punje za vitungua Swaumu robo kilo, vimenye maganda,viroweke ndani ya chupa ya maji ya ujazo wa lita 1.5, ila usivitwange kunywa maji yake kwa kadri utakavyoweza, baada ya masiku nenda kapime presha.Mungu ndiye mponyaji zaidi
Mwenye presha ya kushuka,anaaweza tumia hii tiba?
 
Taja ugonjwa uliokusumbua na namna ulivyopona... Yani dawa iliyokuponyesha.

Mimi nilisumbuka na vidonda vya tumbo kiasi kwamba ilifika mahali ikawa haja kubwa inatoka na damu, nikaishiwa hadi damu ila nikaja kusoma hapa jamiiforum kwamba mashona nguo ni dawa ya vidonda vya tumbo.
Nikatumia kama ilivyoelezwa kwamba ni asubuhi kwa siku 3, sasa nilituma siku mbili tu nikapona na mpaka leo nipo fiti hadi pombe kali nagonga, maharage, pilipili na mazagazaga ya aina zote.

Kuna watu wanasumbuka na kuingia gharama hata za mamilioni kumbe nje kwake kuna dawa ya muda mfupi tu ambayo unakuta ni majani yamejiotea tu

Hayo mashona nguo nilitumia siku 2 nikaacha kutokana na hofu sababu mwelezaji aliweka tahadhari kwamba ukitumia muda mrefu yanasababisha kuwasha kwa figo

View attachment 2557696
Mkuu kwema, samahani nauliza kuwa na uhakika, hayo majani nayafahamu ivi ukiyapondaponda alafu ukayaweka kwenye kikombe ukaongeza maji ya uvuguvugu ukanywa ulojo wake pamoja na majani itakuwa sahihi? Lakini pia maji ukiyachemsha sana ukayachanganya na hayo majani kiganja cha mkono kama maelezo yako huwezi labda kupunguza nguvu ya dawa? Tafadhali naomba nifahamishe kiongozi
 
Huchemshi hayo majani mkuu. Unachemsha maji unayaepua alafu ndio unaweka humo hayo majani
 
Tiba nyingine ya Vidonda vya tumbo,Chukua maji lita 1 yachemshe, tia sukari vijiko 3 vya chakula kwa kijiko kimoja cha Chumvi,yasubili yapowe yawe na uvuguvugu kwa mbali, kunywa kwa kadri utakavyoweze, utajikuta unaanza kucheua yaani kutoa gesi tumboni. Mungu ndiye mponyaji zaidi
Hapo unatibu gesi, sio kidonda cha tumbo!
 
Thyroid dawa yake nin hypothyroid na hyperthyroid nasumbuliwa na hii kitu
Bila shaka nilishawahi kushaurina tena na wewe juu ya shida hii.Nilikwambia hapo ukipata mimea tiba ambayo huwa inafanya kazi ya kuondoa vimbe mwilini inatosha kabisa kukutibu.
Tatizo huwa ni imani tu.Vinginevyo ufanye Surgery

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ndugu Baba Vladmir mshauri atumie nini au mimea tiba gani ili aweze kupona. Ukielezea hapa utakuwa umesaidia wengi sana. Kama unauza dawa hiyo funguka pia sema na uweke namba akutafute
 
Baada ya kupoteza ladha na uwezo wa kunusa miezi mitatu kutokana na COVID-19, niliporudi kuwa sawa pua zikaanza kuziba hasa usiku yaani nikilalia upande mmoja pua inaziba upande huo na nikigeuka inaziba tena mpaka leo sijapata suluhisho. Mwenye kujua namna naweza kutatua changamoto hii nitashukuru sana.
 
Back
Top Bottom