Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Nina shida ya kisunzua (wart) ilianza kama kipele kidogo, baadae kimeenda kimekua mpaka kikawa kisunzua,
Mwenye dawa tafadhali
 
Kwa tatizo la ugonjwa wa ini.nitafute dawa ninayo unapona haraka TU.0717707565
 
Unatumiaje haya mashona nguo. Kikabila tuna yaita kimbara
 
Big Pharma wanapiga hela kwenye antibiotics.

Unakumbuka cha mseto?Kila ukipima malaria 3 5 10 ila sasa hakuna
 
Big Pharma wanapiga hela kwenye antibiotics.

Unakumbuka cha mseto?Kila ukipima malaria 3 5 10 ila sasa hakuna
Siku hizi magonjwa mengi yamekuwa sugu kwa sababu ya dawa dhaifu,bila shaka ni mkakati wa kibiashara zaidi.Antibiotics nyingi watu wanameza hazitoi matokeo kama ilivyokuwa zamani.Nina miaka zaidi ya mitano sasa bila kubugia vidonge zaidi ya hizi za mitishamba na ninajivunia kuifahamu maana niko imara kwelikweli.
 
Wanalazimika kusema UTI kwakuwa baadhi ya waganga wanatoa siri za wagonjwa mtaani "...unamwona yule mama, ni mke wa polisi pale alipo ana gono... alikuja nikampiga sindano, kama huamini subiri jioni atakuja kumalizia dozi ... wanasikika wakisema"
 
Mimi nataka dawa ya biashara kuvuta wateja .

I'm ready to pay kwa atakaenifundisha. Sio kunipa dawa, NATAKA KUJUA DAWA sio KUPEWA DAWA
 
Jamani mwenye Tiba ya UTI sugu ambayo inatoa mpaka usaha nimetumia azuma mpka basi nimekunywa bicarbonate lakini bado msaada tafadhali

NB;UTI ambayo ni sugu na imepanda juu sana msaada
Tafuta hii mizizi ya mimea uchemshe kwa pamoja
1.Mbono
2.Papai dume
3.Mhoshi
Kunywa kila wakati kama maji ya kunywa.Kama utapata pia mzizi wa zile katani ndogondogo weka.Ukipona katoe sadaka na uache ngono zembe.

Kama utahitaji iliyoandaliwa kitaalam pia ipo!
 
Mhoshi ndo mti gani
 
Mitishamba ya kutibu vidonda vya tumbo ni ?
Tafuta majani ya mashona nguo,chemsha na kuchuja vizuri kisha utumie kikombe kidogo cha chai kutwa mara 3.Lakini pia tafuta unga wa mizizi ya mjafari ulioandaliwa vyema unakuwa unatumia kijiko kidogo kwenye maji moto mara 3 kwa kutwa.Kama utahitaji tiba hii iliyoandaliwa tayari unaweza kuniambia pia.Dawa hizo zote na nyingine kwa ajili ya tatizo hilo zipo.
 
Mkuu nilikuwa naomba kuuliza kuhusu dawa ya Degedege, pia naweza kuipata wapi ?
 
Mkuu naomba kujua tiba ya amoeba sugu zinazosababisha kikoozi sugu kisichopona.
 
Mimi nataka kujua tiba ya acid reflux,mwanzoni nilijua ni vidonda vya tumbo na nikawa nahangaika kuvitibia. Nimekuja gundua ni acid reflux. Hizi dawa za hospitalini zinatuliza tu,hakunaga za kienyeji? Wengi wanaojitangaza mtandaoni nawaona kama matapeli tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…