Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Nina shida ya kisunzua (wart) ilianza kama kipele kidogo, baadae kimeenda kimekua mpaka kikawa kisunzua,
Mwenye dawa tafadhali
 
Kwa tatizo la ugonjwa wa ini.nitafute dawa ninayo unapona haraka TU.0717707565
 
Taja ugonjwa uliokusumbua na namna ulivyopona... Yani dawa iliyokuponyesha.

Mimi nilisumbuka na vidonda vya tumbo kiasi kwamba ilifika mahali ikawa haja kubwa inatoka na damu, nikaishiwa hadi damu ila nikaja kusoma hapa jamiiforum kwamba mashona nguo ni dawa ya vidonda vya tumbo.
Nikatumia kama ilivyoelezwa kwamba ni asubuhi kwa siku 3, sasa nilituma siku mbili tu nikapona na mpaka leo nipo fiti hadi pombe kali nagonga, maharage, pilipili na mazagazaga ya aina zote.

Kuna watu wanasumbuka na kuingia gharama hata za mamilioni kumbe nje kwake kuna dawa ya muda mfupi tu ambayo unakuta ni majani yamejiotea tu

Hayo mashona nguo nilitumia siku 2 nikaacha kutokana na hofu sababu mwelezaji aliweka tahadhari kwamba ukitumia muda mrefu yanasababisha kuwasha kwa figo

View attachment 2557696
Unatumiaje haya mashona nguo. Kikabila tuna yaita kimbara
 
Big Pharma wanapiga hela kwenye antibiotics.

Unakumbuka cha mseto?Kila ukipima malaria 3 5 10 ila sasa hakuna
Siku hizi magonjwa mengi yamekuwa sugu kwa sababu ya dawa dhaifu,bila shaka ni mkakati wa kibiashara zaidi.Antibiotics nyingi watu wanameza hazitoi matokeo kama ilivyokuwa zamani.Nina miaka zaidi ya mitano sasa bila kubugia vidonge zaidi ya hizi za mitishamba na ninajivunia kuifahamu maana niko imara kwelikweli.
 
Kupitia jukwaa hili pendwa,niwashauri watu wote kuwa tujiridhishe kwa vipimo sahihi kabla hatujakalilishwa kuwa tuna UTI huku mifumo yetu ikiendelea kulika. Katika harakati zangu kama mtu wa tiba za mimea nimekutana na kesi nyingi za namna hii watu wakitahitaji tiba ambapo baada ya ushauri na kufuata vipimo vya kiwango cha juu, iligundulika kuwa wanaishi na magonjwa ya zinaa kwa muda mrefu ambayo yamejenga usugu na hivyo yanakula polepole kwa sababu kila mara yanatulizwa na Antibiotics na mwisho wa siku inakuwa hatari zaidi.
Wanalazimika kusema UTI kwakuwa baadhi ya waganga wanatoa siri za wagonjwa mtaani "...unamwona yule mama, ni mke wa polisi pale alipo ana gono... alikuja nikampiga sindano, kama huamini subiri jioni atakuja kumalizia dozi ... wanasikika wakisema"
 
Mimi nataka dawa ya biashara kuvuta wateja .

I'm ready to pay kwa atakaenifundisha. Sio kunipa dawa, NATAKA KUJUA DAWA sio KUPEWA DAWA
 
Jamani mwenye Tiba ya UTI sugu ambayo inatoa mpaka usaha nimetumia azuma mpka basi nimekunywa bicarbonate lakini bado msaada tafadhali

NB;UTI ambayo ni sugu na imepanda juu sana msaada
Tafuta hii mizizi ya mimea uchemshe kwa pamoja
1.Mbono
2.Papai dume
3.Mhoshi
Kunywa kila wakati kama maji ya kunywa.Kama utapata pia mzizi wa zile katani ndogondogo weka.Ukipona katoe sadaka na uache ngono zembe.

Kama utahitaji iliyoandaliwa kitaalam pia ipo!
 
Tafuta hii mizizi ya mimea uchemshe kwa pamoja
1.Mbono
2.Papai dume
3.Mhoshi
Kunywa kila wakati kama maji ya kunywa.Kama utapata pia mzizi wa zile katani ndogondogo weka.Ukipona katoe sadaka na uache ngono zembe.

Kama utahitaji iliyoandaliwa kitaalam pia ipo!
Mhoshi ndo mti gani
 
Mitishamba ya kutibu vidonda vya tumbo ni ?
Tafuta majani ya mashona nguo,chemsha na kuchuja vizuri kisha utumie kikombe kidogo cha chai kutwa mara 3.Lakini pia tafuta unga wa mizizi ya mjafari ulioandaliwa vyema unakuwa unatumia kijiko kidogo kwenye maji moto mara 3 kwa kutwa.Kama utahitaji tiba hii iliyoandaliwa tayari unaweza kuniambia pia.Dawa hizo zote na nyingine kwa ajili ya tatizo hilo zipo.
 
Mkuu nilikuwa naomba kuuliza kuhusu dawa ya Degedege, pia naweza kuipata wapi ?
 
Tafuta majani ya mashona nguo,chemsha na kuchuja vizuri kisha utumie kikombe kidogo cha chai kutwa mara 3.Lakini pia tafuta unga wa mizizi ya mjafari ulioandaliwa vyema unakuwa unatumia kijiko kidogo kwenye maji moto mara 3 kwa kutwa.Kama utahitaji tiba hii iliyoandaliwa tayari unaweza kuniambia pia.Dawa hizo zote na nyingine kwa ajili ya tatizo hilo zipo.
Mkuu naomba kujua tiba ya amoeba sugu zinazosababisha kikoozi sugu kisichopona.
 
Mimi nataka kujua tiba ya acid reflux,mwanzoni nilijua ni vidonda vya tumbo na nikawa nahangaika kuvitibia. Nimekuja gundua ni acid reflux. Hizi dawa za hospitalini zinatuliza tu,hakunaga za kienyeji? Wengi wanaojitangaza mtandaoni nawaona kama matapeli tu.
 
Back
Top Bottom