Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Dawa gan ya miti shamba inaweza kutibu bells palsy's?
Hii husababishwa na kufeli kwa neva au misuli ya uso jambo linalopelekea upande mmoja wa uso kupalalaizi na wakati mwingine jicho la upande huo kufumba au kuona kwa shida.Kitaalam hii hali huondoka yenyewe ndani ya wiki moja mpaka tatu,ila kama tatizo likizidi ndipo unaweza kutafuta suluhisho.

Hatua ya kwanza chemsha mizizi ya mlonge changanya na tangawizi kwa wingi na uitumie kila wakati yaani iwe kinywaji chako itakuwa vizuri zaidi kama utachanganya na limao.Huku ukitumia kwa kunywa unaweza pia kujivukiza mchanganyo huo wa tangawizi na limao kwa siku mara mbili.
 
Mtoto wa miaka 14..Ana tatizo..
Kuna kitu huwa kinamtembea ..mwilini mpaka kichwani..na kinapotembea huwa anasikia maumivu Kama kinamchuna...amewahi kunionesha kinatembea ndani ya ngozi Ni Kama gololi.

CC. BABA VLADIMIR
 
Mkuu weka hapa jukwaani nasi tujue samahani mkuu
Mkuu huu uzi umeanzishwa kwa maana sasa nikiingilia na kuanza kuweka uzi juu ya uzi itakuwa sio ustaarabu.
Ndio kisa nikaelekeza in box ili nisivurugee huu uzi mzuri kwetu sote
 
Baba Vladmir ninaomba kujuzwa dawa ya kuzuoa wezi shambani. Nimelima ekari 10 nimejaaliwa mazao yalikuwa ma,uri mnooo jamaa wameiba 3/4 ya mazao
 
nijuze dawa ya gsnzi
Loweka miguu katika maji ya vuguvugu kwa sekunde 15 kisha toa loweka katika maji ya baridi kawaida kwa dakika 1.Rudia hadi itemise dakika 15.
Zaidi ya hapo dawa ya kudumu ya tatizo hilo mlo tu mkuu. Nitafute nikuelekeze aina ya mlo kuondokana na kadhia hiyo
 
Pelvic Inflammatory Disease (PID) ni nini ?

ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari. Dalili za PID huweza kuwa ni ngumu kueleweka. Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote.

Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno. DALILI ZA PID

PID inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote. Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa:

.Maumivu yanayoweza kuwa madogo au makali maeneo ya chini ya tumbo au nyonga Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya

. Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku za hedhi
. Maumivu wakati wa kujamiiana
. Homa, wakati mwingine kusikia baridi
. Maumivu wakati wa haja ndogo, haja

Ndogo ya mara kwa mara au haja ndogo kutoka kwa shida.

CHANZO CHA PID

Kuna bakteria wa aina nyingi wanaoweza kusababisha PID, lakini maambukizi ya gonorrhea na chlamydia ndiyo yanayoonekana zaidi. Bakteria hao huambukiza wakati tendo la ndoa linapofanyika bila ya kutumia kinga.

Agharabu,bacteria hawa huingia vya uzazi vya mwanamke pale ulinzi wa shingo ya kizazi unapovurugwa.

Hii inaweza kutokea mathalani wakati wa hedhi na baada ya kuzaa au mimba kuharibika au kutoka mara chache Bakteria huweza kujipenyeza wakati kifaa chochote cha tiba kinapo ingizwa

MAZINGIRA HATARISHI YA KUPATA PID.

Kuna vipengele ambavyo huweza kukuweka kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata PID, navyo ni:

. Kuwa mwanamke uliye chini ya miaka 25 unayeshiriki ngono
. Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja
. Kuwa na mahusiano na mpenzi mwenye wapenzi zaidi ya mmoja

. Kufanya mapenzi bila kinga
. Kujisafisha na maji mara kwa mara
. Kuwa uliwahi kupata PID kabla au magonjwa mengine ya ngono

MADHARA YATOKANAYO NA PID.

PID ambayo haikupata tiba husababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke.

. Vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi.
Madhara yanayoweza kutokea ni pamoja na:

. Mimba nje ya mirija.
PID ndiyo sababu kubwa ya mimba kutunga nje ya kizazi. Mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya uzazi. Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya uzazi.

Badala yake yai hunata ndani ya mirija ya uzazi.Mimba nje ya kizazi husababisha utokaji wa damu usio kawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.

Maumivu sugu ya nyonga.
PID inaweza kusababisha maumivu sugu ya nyonga yanayoweza dumu miaka mingi.

Makovu ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta Maumivu wakati wa kujamiana na wakati yai linadondoshwa

Kutunga usaha na majipu ndani ya njia ya uzazi.

PID husabibisha usaha na majipu ndani ya njia ya uzazi mara nyingi majipu hayo hutokea ndani ya mirija ya uzazi na ovari

Ingia hayawezi kuota ndani ya nyumba kizazi kama tiba haita tolewa,unaweza kupata makizi hatarishi

TIBA YA UGONJWA WA PID

Tiba ya maramoja kwa kutumia dawa itaondoa maambukizi mambukizi ya PID lakini haita ondoa makovu na kukarabati

kwenye njia ya viungo vya uzazi vilivyotokana PID.

Tiba ya PID inaweza kuwa

ANTIBIOTICS
Daktari atakuandikia dawa kuendana na chanzo cha tatizo

Utasubiri siku kama tatu kuona kama dawa ulizopewa zinafanya kazi

KUMTIBU MWENZA WAKO.
Kuzia maambukizi unatakiwa kumchunguza kumtibu mwenza wako.

KUACHA KUFANYA NGONO KWA MUDA.


Acha kushiriki ngono mpaka umalize tiba na kuona umepona

IMG_0523.jpg

IMG_0524.jpg
 
Back
Top Bottom