Pelvic Inflammatory Disease (PID) ni nini ?
ni maambukizi kwenye viungo vya uzazi vya mwanamke. PID hutokea pale bakteria waenezwao kwa ngono wanaposambaa kutoka kwenye uke hadi kwenye nyumba ya uzazi (uterus), mirija ya uzazi (fallopian tubes) na ovari. Dalili za PID huweza kuwa ni ngumu kueleweka. Baadhi ya wanawake hawaoni dalili zo zote.
Kwa maana hiyo, unaweza usihisi cho chote hadi pale utakaposhindwa kupata ujauzito au hadi utakapoanza kupata maumivu ya kiuno. DALILI ZA PID
PID inaweza isilete dalili zo zote mbaya na ndogo zikitokea zinaweza kuwa ngumu kuzigundua. Baadhi ya wanawake hawapati dalili zo zote. Pale zinapojitokeza, zinaweza kuwa:
.Maumivu yanayoweza kuwa madogo au makali maeneo ya chini ya tumbo au nyonga Uchafu usio wa kawaida au mzito ambao unaweza kuwa na harufu mbaya
. Kutokwa damu kusiko kwa kawaida, hasa wakati wa tendo la ndoa, au katikati ya siku za hedhi
. Maumivu wakati wa kujamiiana
. Homa, wakati mwingine kusikia baridi
. Maumivu wakati wa haja ndogo, haja
Ndogo ya mara kwa mara au haja ndogo kutoka kwa shida.
CHANZO CHA PID
Kuna bakteria wa aina nyingi wanaoweza kusababisha PID, lakini maambukizi ya gonorrhea na chlamydia ndiyo yanayoonekana zaidi. Bakteria hao huambukiza wakati tendo la ndoa linapofanyika bila ya kutumia kinga.
Agharabu,bacteria hawa huingia vya uzazi vya mwanamke pale ulinzi wa shingo ya kizazi unapovurugwa.
Hii inaweza kutokea mathalani wakati wa hedhi na baada ya kuzaa au mimba kuharibika au kutoka mara chache Bakteria huweza kujipenyeza wakati kifaa chochote cha tiba kinapo ingizwa
MAZINGIRA HATARISHI YA KUPATA PID.
Kuna vipengele ambavyo huweza kukuweka kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata PID, navyo ni:
. Kuwa mwanamke uliye chini ya miaka 25 unayeshiriki ngono
. Kuwa na wapenzi zaidi ya mmoja
. Kuwa na mahusiano na mpenzi mwenye wapenzi zaidi ya mmoja
. Kufanya mapenzi bila kinga
. Kujisafisha na maji mara kwa mara
. Kuwa uliwahi kupata PID kabla au magonjwa mengine ya ngono
MADHARA YATOKANAYO NA PID.
PID ambayo haikupata tiba husababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke.
. Vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi.
Madhara yanayoweza kutokea ni pamoja na:
. Mimba nje ya mirija.
PID ndiyo sababu kubwa ya mimba kutunga nje ya kizazi. Mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo PID imesababisha makovu ndani ya uzazi. Makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya uzazi.
Badala yake yai hunata ndani ya mirija ya uzazi.Mimba nje ya kizazi husababisha utokaji wa damu usio kawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.
Maumivu sugu ya nyonga.
PID inaweza kusababisha maumivu sugu ya nyonga yanayoweza dumu miaka mingi.
Makovu ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kuleta Maumivu wakati wa kujamiana na wakati yai linadondoshwa
Kutunga usaha na majipu ndani ya njia ya uzazi.
PID husabibisha usaha na majipu ndani ya njia ya uzazi mara nyingi majipu hayo hutokea ndani ya mirija ya uzazi na ovari
Ingia hayawezi kuota ndani ya nyumba kizazi kama tiba haita tolewa,unaweza kupata makizi hatarishi
TIBA YA UGONJWA WA PID
Tiba ya maramoja kwa kutumia dawa itaondoa maambukizi mambukizi ya PID lakini haita ondoa makovu na kukarabati
kwenye njia ya viungo vya uzazi vilivyotokana PID.
Tiba ya PID inaweza kuwa
ANTIBIOTICS
Daktari atakuandikia dawa kuendana na chanzo cha tatizo
Utasubiri siku kama tatu kuona kama dawa ulizopewa zinafanya kazi
KUMTIBU MWENZA WAKO.
Kuzia maambukizi unatakiwa kumchunguza kumtibu mwenza wako.
KUACHA KUFANYA NGONO KWA MUDA.
Acha kushiriki ngono mpaka umalize tiba na kuona umepona