Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Taja ugonjwa uliokusumbua na namna ulivyopona... Yani dawa iliyokuponyesha.

Mimi nilisumbuka na vidonda vya tumbo kiasi kwamba ilifika mahali ikawa haja kubwa inatoka na damu, nikaishiwa hadi damu ila nikaja kusoma hapa jamiiforum kwamba mashona nguo ni dawa ya vidonda vya tumbo.
Nikatumia kama ilivyoelezwa kwamba ni asubuhi kwa siku 3, sasa nilituma siku mbili tu nikapona na mpaka leo nipo fiti hadi pombe kali nagonga, maharage, pilipili na mazagazaga ya aina zote.

Kuna watu wanasumbuka na kuingia gharama hata za mamilioni kumbe nje kwake kuna dawa ya muda mfupi tu ambayo unakuta ni majani yamejiotea tu

Hayo mashona nguo nilitumia siku 2 nikaacha kutokana na hofu sababu mwelezaji aliweka tahadhari kwamba ukitumia muda mrefu yanasababisha kuwasha kwa figo
Mkuu mashona nguo ndio Nini Kama unapicha naomba uniwekee sampo...nimemaliza dawa zote za madonda ,juzi nikaagiza morogoro haijafaa kitu kabisa
 
images (9).jpeg
images (8).jpeg
Mkuu mashona nguo ndio Nini Kama unapicha naomba uniwekee sampo...nimemaliza dawa zote za madonda ,juzi nikaagiza morogoro haijafaa kitu kabisa
 
Attachments

  • images (10).jpeg
    images (10).jpeg
    20.6 KB · Views: 30
Tiba nyingine ya Vidonda vya tumbo,Chukua maji lita 1 yachemshe, tia sukari vijiko 3 vya chakula kwa kijiko kimoja cha Chumvi,yasubili yapowe yawe na uvuguvugu kwa mbali, kunywa kwa kadri utakavyoweze, utajikuta unaanza kucheua yaani kutoa gesi tumboni. Mungu ndiye mponyaji zaidi
Shukrani sana
 
Tiba ya Ugojwa wa PUMU kifua kubani, mgojwa kushindwa kupumua huwakuta zaidi watu wanaokaa sehemu za baridi,Naanzani kila mtu anamjua Mchwa,Chimba wanapopatikana mchwa,utakuta kuna vitu vinakuwa kama masega ya nyuki,vinakuwa vya rangi ya njano ya kufifia na ni duara,

Chukua kiweke chini ya kigai cha mkaa wa moto unapopikia, kiache kipigwe na joto au moto mpaka kiwe cheusi,kisage unga wake, piki uji wa mahindi, unapochemka tia kijiko kimoja cha ule unga wa mchwa uchemke nao, Subiri uji upoe mpe mgojwa wako, nakuahidi siku tatu ni nyingi, hata kama karazwa hospital atatoka.Mungu ndiye anayejua zaidi
 
Aisee halaf ndio kuna mtu hapa atakuja kusema hizi tiba za giza au ushirikina..mara ni dhambi mbele za Mungu....unakaa unajiulizaaa sasa bapa ushirikina uko wapi...
Kwamfano mmoja hapo kasema

Chimba kichuguu chenye mchwa
Tafuta masega yake meupe yatoe
Kayaweke yapate joto kwenye jiko
Yasage kisha unga wake pikia uji

Unajiuliza mbona hiz ni process za kawaida kabisaaa.

Aisee..hizi dini hzi !??!!!!
 
shukran mkuu kwa uzi wako

mimi na ugonjwa ambao mpaka sasaiv ni mwaka wa kumi unanitesa . huu ugonjwa ulianza katikati ya tumbo panakuwa panauma. Siku zilivyo enda nilianza kuwa nahisi baridi na kutetemeka alfu badae nakuwa sasa .

kuna siku nililala usku iyo hali ya baridi ilinijia nilianza kusikia kama akiri yangu inachanganyikiwa nikaanza kujikuta napiga keleke bila mimi kupenda yani najihic kama kuna nguvu inanisukuma nipige kelele . walinipeleka hospital wakahisi wenda itakuwa ni maralia ya kichwa nilipewa dawa ila iyo hali ilipotea nikawa sawa.

zikapta kama wiki mbiri ile hali ikanirudia na bado nakuwa napiga kelele yani tena ikazidi kunakuwa kama kuna kitu kwenye akiri kinanilazimisha kupiga kelele yani nikama nilianza kuchanganyikiwa ivi. mana ilifika atua nikawa natamni kutembea uchi .

nikiwa natembea kama gari inakuja kuna akiri inaniambia niingie kwenye uvungu wa gari yani nikama nimechanganyikiwa kama nikienda kisimani kuchota maji natmni niingie kisimani yani ivyo .

sasa ikabidi nianze kuzunguka kwa waganga nimetembea kwa waganga wengi sama mkuu ila bado hali aikuwa sawa.

sasa pembeni ya tumbo kunakama kitu kinakuwa kama kinakwangua tumbo alfu sasa kinakuwa kinanichosha. napiga miayo balaaah. mkono wangu wa kushoto na mguu wangu wa kushoto Auna nguvu sasa hili ndio moja ya tatizo linalo nitesa sana tumboni kwangu cjui kuna nini mkuu . nilisha enda hospital kupimwa lakn nikaambiwa hakuna ungonjwa . nikisimama kujinyosha nahic kizungu zingu

msaada mkuu nimeelezea kwa ufupi

Sent from my SC-03J using JamiiForums mobile app
 
Tiba ya KIFUA kikavu kilichobana, mpaka sauti inakauka,Kila mtu humu ndani atakua anajua majani ya NDURA, iko kama nyanya chungu, mti wake unamiba na hutoa matunda furani ya duara, hupenda kuota sehemu zenye ukame hasa kipindi cha kiangazi.
Chimba mizizi yake, isafishe na maji kuondoa mchanga, ibabue kwenye moto, yaani unaichukua unaiweke kwenye majivu ya moto, au juu ya moto, yaani isiungue ila ibabuke, tafuna maganda yake, fyonza mchuzi wake meza, maganda tema,ndani ya siku mbili utakuwa umepona.
Mungu ndiye mjuzi zaidi
 
Mimi nina maumivu ya ndani, kiunoni, nyuma ya mabega, shingo, kukosa umakini (focus)., kupoteza kumbukumbu na usingizi wa mara kwa mara

nimemtumia dozi ya Neurotone na vitamin b complex, Zimekua zinanipa Nafuu ya Muda Mfupi, lkn tatizo bado linanitesa na linanikwamisha sana utendaji wangu wa kazi

Nimekua mtu wa Mazoezi kila siku kwani ndo yananipa nafuu kidogo
 
Aisee halaf ndio kuna mtu hapa atakuja kusema hizi tiba za giza au ushirikina..mara ni dhambi mbele za Mungu....unakaa unajiulizaaa sasa bapa ushirikina uko wapi...
Kwamfano mmoja hapo kasema

Chimba kichuguu chenye mchwa
Tafuta masega yake meupe yatoe
Kayaweke yapate joto kwenye jiko
Yasage kisha unga wake pikia uji

Unajiuliza mbona hiz ni process za kawaida kabisaaa.

Aisee..hizi dini hzi !??!!!!
Mwenyezi Mungu kamuumbia mwanadamu marazi na akampa tiba,mimea mingi sana ni tiba,sema tumeizarau sababu ya utamaduni wa kizungu,Uchawi ni pale mtu anapokwambia unapokunywa simama mlangoni,au katikati ya njia na mengineyo kama hayo
 
Taja ugonjwa uliokusumbua na namna ulivyopona... Yani dawa iliyokuponyesha.

Mimi nilisumbuka na vidonda vya tumbo kiasi kwamba ilifika mahali ikawa haja kubwa inatoka na damu, nikaishiwa hadi damu ila nikaja kusoma hapa jamiiforum kwamba mashona nguo ni dawa ya vidonda vya tumbo.
Nikatumia kama ilivyoelezwa kwamba ni asubuhi kwa siku 3, sasa nilituma siku mbili tu nikapona na mpaka leo nipo fiti hadi pombe kali nagonga, maharage, pilipili na mazagazaga ya aina zote.

Kuna watu wanasumbuka na kuingia gharama hata za mamilioni kumbe nje kwake kuna dawa ya muda mfupi tu ambayo unakuta ni majani yamejiotea tu

Hayo mashona nguo nilitumia siku 2 nikaacha kutokana na hofu sababu mwelezaji aliweka tahadhari kwamba ukitumia muda mrefu yanasababisha kuwasha kwa figo

View attachment 2557696

Hujaeleza ulitengenezaje hiyo dawa ulichemsha?
 
Hujaeleza ulitengenezaje hiyo dawa ulichemsha?
Nimeeleza kwenye comment chini... Chuma majani yake saizi ya kiganja chako uyaoshe, alafu chemsha maji kikombe kidogo yakishachemka tu epua alafu dumbukiza humo hayo majani ukae kana dakika mbili utaona maji yanakuwa na rangi ya chungwa. Kunywa hayo maji kisha tafuna na hayo majani umeze... Siku mbili tu hata kama ulikuwa unaumwa utajisikia sawa. Inakuwa kama muujiza lakini ndio kweli
 
Aisee halaf ndio kuna mtu hapa atakuja kusema hizi tiba za giza au ushirikina..mara ni dhambi mbele za Mungu....unakaa unajiulizaaa sasa bapa ushirikina uko wapi...
Kwamfano mmoja hapo kasema

Chimba kichuguu chenye mchwa
Tafuta masega yake meupe yatoe
Kayaweke yapate joto kwenye jiko
Yasage kisha unga wake pikia uji

Unajiuliza mbona hiz ni process za kawaida kabisaaa.

Aisee..hizi dini hzi !??!!!!
Wana hofu na viwanda vyao vya kutengeneza dawa.
Wanaohubiri dhambi wamekaririshwa tu, hata hivyo vidonge,vingine ni process zimeanzia kwenye miti ikaboreshwa mpaka kupata vidonge
 
Back
Top Bottom