Bila shaka hamjambo kabisa watu wa Mungu na wadau wa jukwaa letu pendwa la JF.
Nimeamua kuandika jambo hili ili kuweka msisitizo zaidi,Nikiwa kama mdau wa tiba ninakutana na changamoto nyingi sana kwa vijana wa kiume zinazotokana na athari ya kitendo hiki cha kujichua.Kwa hiyo nina uhakika usio na shaka kuwa jambo hili ni janga kubwa kwa vijana na linaendelea kuwadhoofisha sana.Kwa hiyo ni bora tuendelee kusisitizana zaidi ili kujiepusha na jambo hili ambalo matokeo yake ni fedheha na kuishia kulialia.
Wavulana wengi wamekuwa wakiathirika sana na tatizo hili la kujichua, hasa wanapokuwa katika shule na vyuo, mchezo huu wa kujichua wamekuwa wakiutumia sana. Sababu kuu inayopelekea kujichua ni kutamani, wengi huangalia picha za utupu(xx) katika mitandao ya kijamii na baadaye fikra huathiriwa na video hizo jambo linalopelekea kujichua huku wakivuta kumbukumbu kupitia video walizozitazama. Tukio hili la kujichua huendelea katika fikra za vijana huku wakiwa na wapenzi wengi wa kufikrika(sawa na kuota ndoto unamiliki ghorofa kubwa,unapoamka unagundua ilikuwa ni ndoto) , jambo linalopelekea kuathirika kisaikolojia na kushindwa kabisa kuhimili tendo la ndoa pindi wakutanapo na wanawake halisi, maana uume husinyaa kabisa na kushindwa kufanya tendo la ndoa maana fikra zimegawanyika.
MADHARA YA PUNYETO
Madhara ya punyeto ni mengi sana, kumbuka mtu aliyezoea kujichua maana yake anamiliki wanawake wengi wa kufikirika, hivyo unapofikia wakati wa kuwa na mke halisi fikra hutatanika kwa kukumbuka wapenzi wale wa kufikrika aliofanya nao ngono kwa njia ya kujichua. Na kwa kuwa mke halisi ni mmoja na wale wa kufikrika ni wengi, akili hushindwa kutambua upande upi ni bora kwake, hivyo uume kushindwa kusimama vyema kwa sababu ya mwathiriko wa kisaikolojia. Kumbuka tendo la ndoa hufanyika tu pale akili inapokuwa na utulivu. Madhara mengine ya mtu aliyejichua kwa muda mrefu ni;
1.Kuathirika(kusinyaa) kwa mishipa ya uume, hivyo kushindwa kujaa damu inayopelekea kusimama kwa uume wakati wa tendo la ndoa.
2.Kuathirika kwa mfumo wa mkojo, jambo linaloweza kusababisha tezi dume.
3.Kupungua kwa hisia za kufanya tendo la ndoa.
4.Kuathirika kwa mfumo wa uzalishaji wa mbegu za kiume.
5.Maumivu ya kichwa, mgongo, kiuno na uchovu mwingi kila wakati.
Madhara makuu zaidi ya mtu aliyeathirika na punyeto ni kupungukiwa nguvu za kiume na hivyo kupelekea kufika kileleni mapema zaidi wakati wa tendo la ndoa, Kwani mishipa ilishasinyaa na hivyo haiwezi kustahimili kubeba damu inayopelekea maumbile kusimama kwa muda mrefu wakati wa tendo la ndoa.
Kumbuka tiba ya Malaria siyo kulala kwenye chandarua wakati tayari una malaria, tiba ni kutumia dawa ili malaria ipone, na ushauri ni kulala kwenye chandarua ili usiumwe na mbu ukaugua malaria tena.
Hivyo kama ulifanya punyeto na imepelekea upungufu wa nguvu za kiume, hakikisha unajitibu ama kutibiwa kikamilifu ili kuweka mfumo wako wa mishipa na misuli katika hali ya awali, na ushauri usirudie tena kufanya punyeto. TAFADHALI SANA AMUA KUACHA PUNYETO SASA.KUPANGA NI KUCHAGUA.
[emoji120][emoji120]
Sent from my TECNO BA2 using
JamiiForums mobile app