Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Niulize chochote juu ya tiba za Mitishamba

Taja ugonjwa uliokusumbua na namna ulivyopona... Yani dawa iliyokuponyesha.

Mimi nilisumbuka na vidonda vya tumbo kiasi kwamba ilifika mahali ikawa haja kubwa inatoka na damu, nikaishiwa hadi damu ila nikaja kusoma hapa jamiiforum kwamba mashona nguo ni dawa ya vidonda vya tumbo.
Nikatumia kama ilivyoelezwa kwamba ni asubuhi kwa siku 3, sasa nilituma siku mbili tu nikapona na mpaka leo nipo fiti hadi pombe kali nagonga, maharage, pilipili na mazagazaga ya aina zote.

Kuna watu wanasumbuka na kuingia gharama hata za mamilioni kumbe nje kwake kuna dawa ya muda mfupi tu ambayo unakuta ni majani yamejiotea tu

Hayo mashona nguo nilitumia siku 2 nikaacha kutokana na hofu sababu mwelezaji aliweka tahadhari kwamba ukitumia muda mrefu yanasababisha kuwasha kwa figo

View attachment 2557696
Unayatumiaje haya mashona nguo?
 
Tiba ya Ugojwa wa PUMU kifua kubani, mgojwa kushindwa kupumua huwakuta zaidi watu wanaokaa sehemu za baridi,Naanzani kila mtu anamjua Mchwa,Chimba wanapopatikana mchwa,utakuta kuna vitu vinakuwa kama masega ya nyuki,vinakuwa vya rangi ya njano ya kufifia na ni duara,

Chukua kiweke chini ya kigai cha mkaa wa moto unapopikia, kiache kipigwe na joto au moto mpaka kiwe cheusi,kisage unga wake, piki uji wa mahindi, unapochemka tia kijiko kimoja cha ule unga wa mchwa uchemke nao, Subiri uji upoe mpe mgojwa wako, nakuahidi siku tatu ni nyingi, hata kama karazwa hospital atatoka.Mungu ndiye anayejua zaidi
mkuu hii dawa pia ni kwa watu wanaoumwa kifua sio cha pumu ila anakohoa sana?
 
mkuu hii dawa pia ni kwa watu wanaoumwa kifua sio cha pumu ila anakohoa sana?
Kwa huyo anayekohoa sana.Nenda kwenye maduka ya dawa asili za mitishamba,tafuta msukuma mwambie akupe unga wa mimea ifuatayo.
1.Kumbwa mbezo
2.Ng'watya
3.Ngakama

Akuchanganyie dawa hizo tatu zote kwa ratio sawa.

Mpatie mgonjwa nusu kijiko katika maji moto mara tatu kwa siku.Au unaweza kuchukua kopo lile la lita moja na nusu ya maji ya kunywa unaweka vijiko 3 vya mchanganyo wa dawa hiyo unatikisa vizuri na baada ya saa moja mgonjwa anaanza kutumia.Anatumia kama maji ya kunywa asubuhi mchana na jioni.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
asante sana, ubarikiwe
 
Kuumwa kizazi kiasi unaona moto unawaka.

Nilichofanya nimeacha kabisa kutumia sukari. Inasemekana sukari inachochea kansa.

Nikawa natafuna majani ya mlonge, kiasi cha kujaza ngumi yangu, kila siku asubuhi kabla sijala kitu chochote.

Sasa sijambo na pia mlonge una busti sana memory.

Uzi mzuri.
Sawasawa
 
Jambo watu wa Mungu!

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na changamoto kubwa ya ugonjwa wa UTI (maambukizi katika mfumo wa mkojo),ugonjwa huu sasa umekuwa ni wimbo wa kila mmoja bila kujali jinsia.

Ni kweli kabisa kuwa,kulingana na mazingira yetu yanayotuzunguka uwezekano wa kupata maambukizi ya ugonjwa huu yamekuwa makubwa.Lakini kuna watu wana magonjwa hatari ya zinaa na bado wanaamini ni UTI kwa sababu ya kutokupata vipimo sahihi. Unakutana na kijana wa kiume anakwambia "nikiamka asubuhi naona uchafu kwenye nguo yangu ya ndani, nilipima nikaambiwa nina UTI lakini nilishatumia dawa ila siponi na sasa nina miaka miwili na tatizo hili" ukifuatilia unagundua kabisa kuwa hajapata vipimo vinavyostahili kubaini tatizo lake la msingi isipokuwa anabugia tu Antibiotics tatizo linajituliza na baada ya wiki kadhaa linarudi tena kwa kasi huku likiendelea kumtafuna.

Vivyohivyo kwa wanawake,wanaendelea kuhangaika na magonjwa ya zinaa kwa muda mrefu bila kupona kwa sababu hawajapata vipimo sahihi vya kubainisha magonjwa hayo.Mwisho wa siku inawapelekea kuathirika kwa mifumo yao ya uzazi na kupata maambukizi makubwa(PID) jambo linaloweza kusababisha adha na madhara makubwa na hata kutokupata mimba.

Kupitia jukwaa hili pendwa,niwashauri watu wote kuwa tujiridhishe kwa vipimo sahihi kabla hatujakalilishwa kuwa tuna UTI huku mifumo yetu ikiendelea kulika. Katika harakati zangu kama mtu wa tiba za mimea nimekutana na kesi nyingi za namna hii watu wakitahitaji tiba ambapo baada ya ushauri na kufuata vipimo vya kiwango cha juu, iligundulika kuwa wanaishi na magonjwa ya zinaa kwa muda mrefu ambayo yamejenga usugu na hivyo yanakula polepole kwa sababu kila mara yanatulizwa na Antibiotics na mwisho wa siku inakuwa hatari zaidi.

Tujitahidi kuwaona madaktari wabobezi wa mifumo hiyo ili watupe vipimo na majibu sahihi,siyo kukimbilia maabara kila siku kupima mkojo.
 
Tatizo wabongo wabishi Sana,

Mchai chai ndo Tiba na Kinga ya Karne na Karne ya magonjwa yote yanayohusu sehem za Siri.

Wabongo waachane na matakataka ya azuma
Asante kwa kutoa hii Elimu kubwa wengi hawafahamu.
 
Hata Mimi siku hizi sijawahi yasikia yale magonjwa yaliyo tutesa miaka ya tisini Kama kisonono, pangusa, mandeletele na kaswende sijui ndio yameji-apdate imekuwa UTI.
 
Tatizo wabongo wabishi Sana,

Mchai chai ndo Tiba na Kinga ya Karne na Karne ya magonjwa yote yanayohusu sehem za Siri.

Wabongo waachane na matakataka ya azuma
Huo mchai chai unafanyaje
 
Hata Mimi siku hizi sijawahi yasikia yale magonjwa yaliyo tutesa miaka ya tisini Kama kisonono, pangusa, mandeletele na kaswende sijui ndio yameji-apdate imekuwa UTI.
Yapo sana! Mwanamke atakwambia nina PID sugu.Maana yake kizazi kinalika lakini chanzo ni hiyo zinaa.
 
Back
Top Bottom