Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Kwanini watu wanao kaa Sana karibu na air-conditioning au feni kwa muda mrefu wanapata tatizo la meno kufa ganzi

Ni Nini solution kwa mtu Kama huyo..
 
Baadhi ya meno yangu yanapiga shoti kila nikila punje ngumu mfano mahindi,mchele, nikila wali nakula kwa tahadhari sana nikigonja jiwe tu shiti ninayopata sio ndogo.

Nifanye nini
 
Nini kinasababisha kupata maumivu kwenye meno ninapokula kitu chenye sukari nyingi? i.e. chocolate, sometimes hata asali nikiweka kwenye meno pia huwa napata maumivu
 
umefanya jambo la maana sana kuleta uzi huu hapa,kama ukiwa serious utasaidia watu na utapa wateja wengi.

inawezekana nikatatua changamoto ya maumivu ya meno kabisa bila kutoa au kuziba?
 
Je kuna namna ya kusafisha meno bila kupaka rangi,maana meno yangu ni gold na sitaki kupaka rangi.
 
Uzi ukisipovamiwa na wanamasihara utanufaisha wengi. Naomba kujua gharama ya kung'arisha meno especially kwa smoker
 
Kwa nini mpaka leo hakuna tiba ya meno zaidi ya kung'oa?
Hapana, Dawa ya jino sio Kung'oa kuna matibabu zaidi ya kuokoa jino ili lisiondolewe kinywani ikiwepo
. Huduma ya mzizi wa jino ( kuondoa ufahamu wa jino , jino linabaki imara na utaendelea kulitumia kama kawaida ( Root canal Treatment)

. Kukata kiiini cha Jino na jino litaendelea kubaki imara
Hivyo unaweza fika kwenye hospital/ kliniki za kinywa na meno ukapata ushauri na matibabu zaidi
 
Kinacho sababisha kinywa kunuka hasa ni nini? Meno au ulimi?
Vyote kwa pamoja kitaalamu harufu mbaya mdomoni tunaita (Halitosis)
Visababishi
.Meno yaliyotoboka
.magonjwa ya Fizi
.Matumizi ya baadhi ya madawa
.Mdomo mkavu
. Kutosafisha kinywa vizuri
.Hivyo unashauriwa kufika kwa mtaalamu wa mtaalamu Wa kinywa na meno uweze kutibiwa , kama una tatizo hilo unaweza wasiliana nami kwa namba hizi 0658 950 085
 
Je meno yenye rangi ya kahawia kama waliyonayo watu wa baadhi ya maeneo nchini, ni kweli yameoza? Je nini kifanyike kama.Meno yangu ni ya kahawia na hayajatoboka ila nataka yawe meupe kama Meno ya watu wengine?
A.K.A MENO YA ARUSHA

Meno Kahawia (Fluorosis) hutokea mtoto anapopata kiwango kikubwa cha fluoride akiwa tumboni au katika miaka ya mwanzo ya maisha. Meno huanza kutengenezwa kati ya wiki ya 3 hadi 6 ya ujauzito. Ikiwa mama anapata maji au vyakula vyenye fluoride nyingi, meno ya mtoto yanayokua yanaweza kuathirika, na kusababisha madoa meupe au rangi ya kahawia kwenye meno baada ya kutokeza.
Matibabu ya meno ya kahawia

1. Kupiga mswaki na polishing– Kusafisha sehemu za juu za meno ili kupunguza madoa mepesi.
2. Bleaching – Njia ya kusafisha kitaalam kwa kutumia kemikali ili kupunguza rangi ya meno.
3. Veneers – Viboreshaji vidogo vya porcelaini au composite vinawekwa kufunika meno yaliyoathirika.
4. Crowns – Kofia za meno zinavaliwa kwenye meno yaliyoathirika sana ili kuboresha muonekano na uimara.

Kujua matibabu yapi hutegemea kiwango cha fluorosis, Unaweza fika ofisini kwetu ukapata huduma hiyo kwa gharama rafiki , tuwasiliane kwa 0658 950 085
Ahsante
 
Ndugu mtaalamu mimi nikinywa kitu cha baridi kwenye soft palate nahisi maumivu makali na kichwa kinauma tiba ni nini?
Mkuu tuwasiliane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…