Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Niulize chochote kuhusu afya ya kinywa na meno, nitakujibu

Mtaalam kijana wangu ana 8yrs, kang'oa meno mawili ya mbele muda mrefu sana almost 7months na hayajaota mapya mpaka leo, nini shida?
Meno ya ukubwani ya juu huota kuanzia miaka 6- 13 , iwapo meno yaliyotoka yalikuwa ya utu uzima hayawezi kuota. Ikiwa meno yaliyotoka yalikuwa ya utotoni ( deciduous teeth ) yataota
 
Je ni kweli kwamba kwenye kinywa cha binadamu kuna sehemu zenye nyenge ndio maana watu hupigana denda?

Ukweli ni upi mpaka watu wapende kupigana denda?
Naendelea kujifunza mkuu
 
Kwa nn watu wananuka mdomo kama chamber
Sababu za mdomo kutoa harufu mbaya
.Meno yaliyotoboka
.kinywa kikavu
.Matumizi ya vinywaji ( pombe)
.Magonjwa ya fizi
Hivyo tatizo hili linatatulika kwa kufika kliniki ya kinywa na meno na kupata tiba sahihi ya kusafisha meno, kuziba meno yaliyotoboka Nk karibu Sana
 
Sababu za mdomo kutoa harufu mbaya
.Meno yaliyotoboka
.kinywa kikavu
.Matumizi ya vinywaji ( pombe)
.Magonjwa ya fizi
Hivyo tatizo hili linatatulika kwa kufika kliniki ya kinywa na meno na kupata tiba sahihi ya kusafisha meno, kuziba meno yaliyotoboka Nk karibu Sana
Pombe unaionea
 
umefanya jambo la maana sana kuleta uzi huu hapa,kama ukiwa serious utasaidia watu na utapa wateja wengi.

inawezekana nikatatua changamoto ya maumivu ya meno kabisa bila kutoa au kuziba?
Ahsante mkuu, karibu
 
A.K.A MENO YA ARUSHA

Meno Kahawia (Fluorosis) hutokea mtoto anapopata kiwango kikubwa cha fluoride akiwa tumboni au katika miaka ya mwanzo ya maisha. Meno huanza kutengenezwa kati ya wiki ya 3 hadi 6 ya ujauzito. Ikiwa mama anapata maji au vyakula vyenye fluoride nyingi, meno ya mtoto yanayokua yanaweza kuathirika, na kusababisha madoa meupe au rangi ya kahawia kwenye meno baada ya kutokeza.
Matibabu ya meno ya kahawia

1. Kupiga mswaki na polishing– Kusafisha sehemu za juu za meno ili kupunguza madoa mepesi.
2. Bleaching – Njia ya kusafisha kitaalam kwa kutumia kemikali ili kupunguza rangi ya meno.
3. Veneers – Viboreshaji vidogo vya porcelaini au composite vinawekwa kufunika meno yaliyoathirika.
4. Crowns – Kofia za meno zinavaliwa kwenye meno yaliyoathirika sana ili kuboresha muonekano na uimara.

Kujua matibabu yapi hutegemea kiwango cha fluorosis, Unaweza fika ofisini kwetu ukapata huduma hiyo kwa gharama rafiki , tuwasiliane kwa 0658 950 085
Ahsante View attachment 3118042
Mkuu hapa umetupiga kuangalia hayo meno juu na chini si kinywa kimoja!!
 
Baadhi ya meno yangu yanapiga shoti kila nikila punje ngumu mfano mahindi,mchele, nikila wali nakula kwa tahadhari sana nikigonja jiwe tu shiti ninayopata sio ndogo.

Nifanye nini
Pole sana mkuu hapo lazima ufike hospital tufanye uchunguzi wa kinywa kujua je meno yaliyotoboka au yamesagika Nk naomba tuwasiliane kwa 0658 950 085
 
Kwanini baadhi ya detectives/askari wapelekezi hutumia mpangilio wa meno wa mabaki ya mtu aliyekufa ambaye hatambuliki kama njia ya kumtambua

Sayansi yake ni ipi hapo?
Kila binadamu ana mpangalio tofauti na mwingine size ya meno na Taya kati ya mwanamke na mwanaume ki anatomy yapo tofauti, mgonjwa Alie wahi tibiwa na kuwa registered katika mfumo sahihi mfn kafanya filling tooth no 26,27 na composite na kupitia maiti ukaona kweli kafanyiwa filling utajua ni huyo huyo utacomfirm...meno kati ya mtoto na mtu mzima yapo tofauti na uotaji wake hutegemea miaka so mtu mwenye miaka 17 ni rare kumkuta na namba 8 au mwenye miaka 10 kumkuta na namba 7 hio itakupa miaka na ukaona meno yameota hayajaunga apex mfn maiti umeona inanamba 7 na apex zipo wapi unajua kirahisi kua namba 7 unaota umri wa miaka 12-13 Ili apex ifunge unaongeza miaka 2-3 mbele ko meno Yana mengi katika utambuzi hio ni baadhi tu
 
Je impaction ni ugonjwa? Kama sii ugonjwa, je kuna umuhimu gani wa kuyang'oa wisdom teeth zenye impaction wakati hazikuumizi?
Impaction sio ugonjwa per say naweza weka kama ulemevu mfn mtu kidole kiote sehemu isiyo stahili utasema ni ugonjwa au deformity? Kwa nn itoke Kwa sababu inatabia ya kula distal root ya namba 7 na inatendency ya kusababisha malocclusion pmj na cyst
 
umefanya jambo la maana sana kuleta uzi huu hapa,kama ukiwa serious utasaidia watu na utapa wateja wengi.

inawezekana nikatatua changamoto ya maumivu ya meno kabisa bila kutoa au kuziba?
Ahsante, utapata huduma ya kuondoa mzizi wa jino ( Root canal Treatment) ambayo itaondoa maumivu ya meno na jino lako litabaki imara . Karibu Nitafurahi nikikuhudumia
 
Back
Top Bottom