Niulize chochote kuhusu biashara ya duka la rejareja

Hakuna uchawi Wala ndumba nazingatia hzi mbinu
*nafungua mapema nachelewa kufunga
*sikopeshi hata kitu Cha Mia kukopesha nikumfukuza mteja
*kuwa msafi na kupanga vitu vizuri kuhakikisha duka linavutia
*usipende tongoza tongoza wake za watu na wasichana wa mtaani hapo utajitengenezea sifa mbaya
*kuwa na huduma nzuri kwa kila mtu
*hakikisha unakua na bidhaa ambazo zinakutambulisha kuwa dukani kwako pekee iyo bidhaa inapatikana
* tafuta machimbo ya Bei rahisi
 
Hi
Hivi ni kwa nini maduka asilimia 99 mmechakachua mizani? Kwa nini huwa mnatafuta faida ya dhuluma?
 
1.Nawezaje kugundua site nzuri kwa biashara hiyo?

2.vp inawezekana kufanya biashara hiyo bila ushirikina kwa uzoefu wako

3.mbona kama faida ni kidogo sana mnawezaje kupiga hatua?
Haya maduka ya reja reja huwa nashangaa kuona mbaba mwenye familia kila siku yupo dukani na maisha yanaenda lakin nikifikiria faida iliyomo nashindwa kuelewa wanawezaje kutimiza majukumu ya familia
 
Nina mashaka kidogo juu ya wewe kufanya hiyo biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…