Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Habari mkuu mimi nina basi la abiria dala dala tatizo la gari yangu mara nyingi clach inazingua, kila mwezi mara mbili au tatu je nini suluhisho? je ikiwa halijarekebishika kabisa je kunaweza kisababisha kuharibu vitu mwengine kwenye gari? Asante
 
Mkuu mimi nina Grand Escudo V6 H27A ilianza catalyst conveter kuwa inaziba baadae fundi akashauri tuitoe zile parts za ndani wavu fulani na unga matokeo mlio mbaya siupendi kabisa je kuna madhara na nitaurekebisha vipi?
 
Nimesikitika sana nimekuwa natumia 20W 50 kwa suzuki grand 2730cc si nimeua?
 
Mkuu mimi nina Grand Escudo V6 H27A ilianza catalyst conveter kuwa inaziba baadae fundi akashauri tuitoe zile parts za ndani wavu fulani na unga matokeo mlio mbaya siupendi kabisa je kuna madhara na nitaurekebisha vipi?
Inawezekana ikawa inakula mafuta sana sasa, lakini hakuna madhara makubwa kwenye injini
 
Catalytic converter zinauzwa bei mbaya sana; huwa Kuna mafuta ya kuzisafisha yanaitwa Seafoam. Kwa vile umeshitoa, basi badilisha na muffler pia uweke kubwa
 
Nilichokigundua katika kipindi hiki cha kujihusisha na uuuzaji wa oil nimegundua vitu vifuatavyo?
1 wamiliki wengi wa magari hawanunui oil wenyewe wengi wao wanawapa mafundi gari na yeye fundi ndo atajua oil gani ya kuweka kulingana na pesa aliyomtajia boss na imekua kawaida kwa mafundi kuwadanganya wateja wao kwa kuwambia kiasi kikubwa cha pesa lkn kinachowekwa ni oil ya bei rahisi na nisisitize ukimpa fundi yeye haangalii ubora wa oil anaangalia masirahi
2 wamiliki wengi wa magari hawafuati manual za magari yao badala yake wanasikiliza kile ambacho anaambiwa na fundi "yaani mwenye chombo ambae ni mtengenezaji anakwambia weka kitu hiki lakini unashindwa kumuelewa badala yake unamsikiliza mrekebishaji" angejua sana si atengeneze gari yake huyo fundi wako na yenyewe itembee
3 wamiliki wengi wa magari hawahitaji ubora wa kitu ila wengi wanafuata unafuu wa bei na hapa ndo wengi wao utawasikia oil ni oil tu halafu gari si ya kwangu weka yyt tu ila baadae likibuma ndo hao hao wa kwanza kuja humu na kuanza kuomba ushauri" kama kweli umetoa pesa zako ukanunua gari ikawa yako mkononi plz ukiepuka hizo sababu tatu hapo juu hakika hiyo gari badala ya kukuchoka utaichoka wewe
 
Mkuu nakumbushia ombi langu hili, natanguliza shukrani
Samahani nilipitiwa; mambo mengi sana siku hizi. naomba unibipu Ijumaa kusudi nikutafutie wakati wa weekend
 
mkuu maoni yako gari kluger tairi ya mbele kushoto inapata moto sana nikitembea nini shida itakuwa?
 
mkuu maoni yako gari kluger tairi ya mbele kushoto inapata moto sana nikitembea nini shida itakuwa?
Either brake pad zinabana, kwa hiyo unakuwa umekanyaga accelerator wakati wote ili gari liende mbele, ukiachia tu linapunguza mwendo; au wheel bearing zimeanza kufa. Lakini nadhani sehemu kubwa ni breki kubana; jaribu kuachia steering kama hutaona gari linataka kuelekea upande unaopata joto.
 
shukrani mkuu kuna mtu nilimuuliza akaniambia brake caliper something like that ,ngoja nikawabane vzr mafundi warekebishe
 
Inauzwaje hii boss
Alikuwa anauza TZS 110,000.00 lakini tukapunguziana mpaka 100,000.00. Ni Mza pale Sinai. Kuna mwingine alikuwa ananitafutia aina ya TOTAL mjini kati, mwenye nayo alikuwa anauza TZS 20,000/L na mbaya zaidi akawa amefunga yuko mbali.
 
Reactions: 365
Naolba kuuliza mkuu nna vits rs manual gear leaver yake inakua ngum unapoweka gia kama inakwama flan hv halaf na steering nayo ngumu...shida inaweza kua nn??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…