Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Habari mkuu mimi nina basi la abiria dala dala tatizo la gari yangu mara nyingi clach inazingua, kila mwezi mara mbili au tatu je nini suluhisho? je ikiwa halijarekebishika kabisa je kunaweza kisababisha kuharibu vitu mwengine kwenye gari? Asante
 
Ni sawa kuwa milage ni muhimu kuhusu ubora wa injini; lakini catalytic converter ndani yake mna madawa (catalyst) ambayo yana life span; baada ya muda yana-expire. Miaka minane nimechukulia umri wa chini, nyingine zinadumu mpaka miaka 15 kabla hayachoka
Mkuu mimi nina Grand Escudo V6 H27A ilianza catalyst conveter kuwa inaziba baadae fundi akashauri tuitoe zile parts za ndani wavu fulani na unga matokeo mlio mbaya siupendi kabisa je kuna madhara na nitaurekebisha vipi?
 
Sijasoma taarifa ulizoletwa kutoka Japan kwenye gari lako, kwa hiyo inawezekana sitakupa jibu kamili la swali lako. Kila gari lina grade ya oil yake kulingana na tolerance ya parts zinazotumika katika injini ya gari lile. Ndiyo maana mara kadhaa nimewaambia watu wasome vitabu vya magari yao, hakuna oil ya kutumika katika magari yote, kila gari lina optimal oil yake.

Iwapo una gari ambalo hujui oil yake, ndipo experience ya mafundi kama mimi inapokuja. Elewa kuwa oil zote za injini zina namba mbili, moja inayoishia na herufi W na nyingine haina herufi yoyote; kwa mfano 5W-20. Namba zile maana yake kwa watu wa Engineering na Physics zinaonyesha viscosity, au kwa lugha rahisi ya kiswahili ni utelezi wa oil hiyo. namba ya kwanza yenye W, ina maana ya utelezi wakati wa Winter au joto la chini sana, na namba ya pili ni utelezi wakati injini inafanya kazi zake sawsawa.

Kwa Tanzania ambako hakuna Winter, watu tunatakiwa kuwa tunatazama zaid ile namba ya pili ambayo nimesema ni kati ya 20 na 30 tu kwa gari la kawaida. Ile namba inayoishia W inakusaidia wakati wa baridi, na kwa Tanzania hatuna baridi kali kwa hiyo tunahitaji namba ya chini tu. ndiyo maana nashauri kati ya 5W na 10W tu.

Sijui sticker unazopata wewe kutoka kwa exporter wako wa Japan kwani iwapo anajuwa kuwa anauza magari hayo kwenye maeneo ya tropical, ninaamini kuwa oil recommendation yake haitakuwa ile namba inayoisha na W. Kwa gari amabayo ni reconditioned, inawezekana mafundi wakapandisha viscoscity kidogo ili kujaza mapengo ya ukuukuu wa injini. Iwapo namba ya pili ya oil ni 40 au 50 ina maana kuwa injini hiyo ni chakavu sana,
Nimesikitika sana nimekuwa natumia 20W 50 kwa suzuki grand 2730cc si nimeua?
 
Mkuu mimi nina Grand Escudo V6 H27A ilianza catalyst conveter kuwa inaziba baadae fundi akashauri tuitoe zile parts za ndani wavu fulani na unga matokeo mlio mbaya siupendi kabisa je kuna madhara na nitaurekebisha vipi?
Inawezekana ikawa inakula mafuta sana sasa, lakini hakuna madhara makubwa kwenye injini
 
Catalytic converter zinauzwa bei mbaya sana; huwa Kuna mafuta ya kuzisafisha yanaitwa Seafoam. Kwa vile umeshitoa, basi badilisha na muffler pia uweke kubwa
 
Nilichokigundua katika kipindi hiki cha kujihusisha na uuuzaji wa oil nimegundua vitu vifuatavyo?
1 wamiliki wengi wa magari hawanunui oil wenyewe wengi wao wanawapa mafundi gari na yeye fundi ndo atajua oil gani ya kuweka kulingana na pesa aliyomtajia boss na imekua kawaida kwa mafundi kuwadanganya wateja wao kwa kuwambia kiasi kikubwa cha pesa lkn kinachowekwa ni oil ya bei rahisi na nisisitize ukimpa fundi yeye haangalii ubora wa oil anaangalia masirahi
2 wamiliki wengi wa magari hawafuati manual za magari yao badala yake wanasikiliza kile ambacho anaambiwa na fundi "yaani mwenye chombo ambae ni mtengenezaji anakwambia weka kitu hiki lakini unashindwa kumuelewa badala yake unamsikiliza mrekebishaji" angejua sana si atengeneze gari yake huyo fundi wako na yenyewe itembee
3 wamiliki wengi wa magari hawahitaji ubora wa kitu ila wengi wanafuata unafuu wa bei na hapa ndo wengi wao utawasikia oil ni oil tu halafu gari si ya kwangu weka yyt tu ila baadae likibuma ndo hao hao wa kwanza kuja humu na kuanza kuomba ushauri" kama kweli umetoa pesa zako ukanunua gari ikawa yako mkononi plz ukiepuka hizo sababu tatu hapo juu hakika hiyo gari badala ya kukuchoka utaichoka wewe
 
Mkuu nakumbushia ombi langu hili, natanguliza shukrani
Samahani nilipitiwa; mambo mengi sana siku hizi. naomba unibipu Ijumaa kusudi nikutafutie wakati wa weekend
 
mkuu maoni yako gari kluger tairi ya mbele kushoto inapata moto sana nikitembea nini shida itakuwa?
 
mkuu maoni yako gari kluger tairi ya mbele kushoto inapata moto sana nikitembea nini shida itakuwa?
Either brake pad zinabana, kwa hiyo unakuwa umekanyaga accelerator wakati wote ili gari liende mbele, ukiachia tu linapunguza mwendo; au wheel bearing zimeanza kufa. Lakini nadhani sehemu kubwa ni breki kubana; jaribu kuachia steering kama hutaona gari linataka kuelekea upande unaopata joto.
 
Either brake pad zinabana, kwa hiyo unakuwa umekanyaga accelerator wakati wote ili gari liende mbele, ukiachia tu linapunguza mwendo; au wheel bearing zimeanza kufa. Lakini nadhani sehemu kuwaba ni breki kubana; jaribu kuachia steering kama hutaona gari linataka kuelekea upande unaopata joto.
shukrani mkuu kuna mtu nilimuuliza akaniambia brake caliper something like that ,ngoja nikawabane vzr mafundi warekebishe
 
Inauzwaje hii boss
Alikuwa anauza TZS 110,000.00 lakini tukapunguziana mpaka 100,000.00. Ni Mza pale Sinai. Kuna mwingine alikuwa ananitafutia aina ya TOTAL mjini kati, mwenye nayo alikuwa anauza TZS 20,000/L na mbaya zaidi akawa amefunga yuko mbali.
 
  • Thanks
Reactions: 365
Naolba kuuliza mkuu nna vits rs manual gear leaver yake inakua ngum unapoweka gia kama inakwama flan hv halaf na steering nayo ngumu...shida inaweza kua nn??
 
Back
Top Bottom