Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
10,000kmHii unaimwaga baada ya km ngapi..??
Mkuu mimi nina Grand Escudo V6 H27A ilianza catalyst conveter kuwa inaziba baadae fundi akashauri tuitoe zile parts za ndani wavu fulani na unga matokeo mlio mbaya siupendi kabisa je kuna madhara na nitaurekebisha vipi?Ni sawa kuwa milage ni muhimu kuhusu ubora wa injini; lakini catalytic converter ndani yake mna madawa (catalyst) ambayo yana life span; baada ya muda yana-expire. Miaka minane nimechukulia umri wa chini, nyingine zinadumu mpaka miaka 15 kabla hayachoka
Nimesikitika sana nimekuwa natumia 20W 50 kwa suzuki grand 2730cc si nimeua?Sijasoma taarifa ulizoletwa kutoka Japan kwenye gari lako, kwa hiyo inawezekana sitakupa jibu kamili la swali lako. Kila gari lina grade ya oil yake kulingana na tolerance ya parts zinazotumika katika injini ya gari lile. Ndiyo maana mara kadhaa nimewaambia watu wasome vitabu vya magari yao, hakuna oil ya kutumika katika magari yote, kila gari lina optimal oil yake.
Iwapo una gari ambalo hujui oil yake, ndipo experience ya mafundi kama mimi inapokuja. Elewa kuwa oil zote za injini zina namba mbili, moja inayoishia na herufi W na nyingine haina herufi yoyote; kwa mfano 5W-20. Namba zile maana yake kwa watu wa Engineering na Physics zinaonyesha viscosity, au kwa lugha rahisi ya kiswahili ni utelezi wa oil hiyo. namba ya kwanza yenye W, ina maana ya utelezi wakati wa Winter au joto la chini sana, na namba ya pili ni utelezi wakati injini inafanya kazi zake sawsawa.
Kwa Tanzania ambako hakuna Winter, watu tunatakiwa kuwa tunatazama zaid ile namba ya pili ambayo nimesema ni kati ya 20 na 30 tu kwa gari la kawaida. Ile namba inayoishia W inakusaidia wakati wa baridi, na kwa Tanzania hatuna baridi kali kwa hiyo tunahitaji namba ya chini tu. ndiyo maana nashauri kati ya 5W na 10W tu.
Sijui sticker unazopata wewe kutoka kwa exporter wako wa Japan kwani iwapo anajuwa kuwa anauza magari hayo kwenye maeneo ya tropical, ninaamini kuwa oil recommendation yake haitakuwa ile namba inayoisha na W. Kwa gari amabayo ni reconditioned, inawezekana mafundi wakapandisha viscoscity kidogo ili kujaza mapengo ya ukuukuu wa injini. Iwapo namba ya pili ya oil ni 40 au 50 ina maana kuwa injini hiyo ni chakavu sana,
Inawezekana ikawa inakula mafuta sana sasa, lakini hakuna madhara makubwa kwenye injiniMkuu mimi nina Grand Escudo V6 H27A ilianza catalyst conveter kuwa inaziba baadae fundi akashauri tuitoe zile parts za ndani wavu fulani na unga matokeo mlio mbaya siupendi kabisa je kuna madhara na nitaurekebisha vipi?
Nimejaribu kweli kunaongezeko la ulaji mafuta. Nifanyeje? Jenaweza pata hata used huko?Inawezekana ikawa inakula mfuta sana sasa
Mbona ulishaiua tokea mda tu na ili isiendelee kufa zaidi ibadilishie sasa oil weka inayotakiwaNimesikitika sana nimekuwa natumia 20W 50 kwa suzuki grand 2730cc si nimeua?
Ok sawa mkuu...kwa town trips ni karibu mwaka mzima10,000km
Mkuu nakumbushia ombi langu hili, natanguliza shukraniMkuu Kichuguu naomba msaada wa User Manual ya Mitsubish Outlander 2006.
Either brake pad zinabana, kwa hiyo unakuwa umekanyaga accelerator wakati wote ili gari liende mbele, ukiachia tu linapunguza mwendo; au wheel bearing zimeanza kufa. Lakini nadhani sehemu kubwa ni breki kubana; jaribu kuachia steering kama hutaona gari linataka kuelekea upande unaopata joto.mkuu maoni yako gari kluger tairi ya mbele kushoto inapata moto sana nikitembea nini shida itakuwa?
shukrani mkuu kuna mtu nilimuuliza akaniambia brake caliper something like that ,ngoja nikawabane vzr mafundi warekebisheEither brake pad zinabana, kwa hiyo unakuwa umekanyaga accelerator wakati wote ili gari liende mbele, ukiachia tu linapunguza mwendo; au wheel bearing zimeanza kufa. Lakini nadhani sehemu kuwaba ni breki kubana; jaribu kuachia steering kama hutaona gari linataka kuelekea upande unaopata joto.
Mkuu, Ubarikiwe sana kwa ufafanuzi wako. Nimefanikiwa kupata aina mojawapo kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini
Asante sana.
Inategemea na kampuni unayoichagua lakini bei yake inaanzia 55000 kwa litre4Inauzwaje hii boss
Alikuwa anauza TZS 110,000.00 lakini tukapunguziana mpaka 100,000.00. Ni Mza pale Sinai. Kuna mwingine alikuwa ananitafutia aina ya TOTAL mjini kati, mwenye nayo alikuwa anauza TZS 20,000/L na mbaya zaidi akawa amefunga yuko mbali.Inauzwaje hii boss
Oil ya gear box ipo sawa? oil ya steering nayo ipo sawa? Tazama hayo wakati ukisubiri wataalam zaidi..Naolba kuuliza mkuu nna vits rs manual gear leaver yake inakua ngum unapoweka gia kama inakwama flan hv halaf na steering nayo ngumu...shida inaweza kua nn??