Mkuu na gari dogo la 1.5L, kwa kawaida likiwa idle mshale wa rpm unakua chini kidogo ya moja.
Leo nikiwa kwenye nimesimama kwenye foleni limenizimikia.
Nikaliwasha likawak na kuweza kuondoka bila shida yoyote.
Gari halikua lime overheat, sikua nimewasha AC, tank lilikua chini kidogo tu ya nusu.
Level ya coolant, oil zote zipo sahihi na sehemu liliponizimikia ni tambarare.
Tatizo linaweza kuwa nini? Maana kitu pekee nilichobadili hivi recently ni redio na nimenotice saa ya kwenye redio ilireset baada ya kutokea hivyo.
Injini kuzimika wakati wa idling kunasababishwa na sababu nyingi sana ndogo ndogo ambazo hazina madhara kabisa kwenye injini yako. Ngoja nitaje ambazo ni za kawaida sana.
(1) Inawezekana air filter yako imeshajaa uchafu; iangalie na ukiweza uibadilishe.
(2) Inawezekan air flow sensor imeshachafuka au imekufa. Air flow sensor ni kiwaya chembamba sana kinachoweza kukatika hasa iwapo air filter ni chafu. Kama imechafuka, kuna mafuta ya kuisafishia, na kama imekufa unaweza kubadilisha na kuweka nyingine. Zinagharimu kati ya dola mbili hadi kumi na tano tu.
(3) Inawezekana injector zako zina uchafu, kwa hiyo hazipitishi mafuta wakati pressure ni ndogo. Kama tatizo ni hili, kuna injector cleaners ambazo unaweza kuongeza kichupa kimoja kwe tanki la mafuta likiwa full tank kukusafishia injector hizo.
(4) Inawezekana throttle position sensors kwa upande wa chini haifanyi kazi, kwa hiyo ukiachia accelerator basi computer inakuwa haipati taarifa za position ya accelerator yako kwa hiyo inashindwa kujua ni kiasi gani cha mafuta kinahitajiwa na hivyo inaamua kukata mafuta kabisa. TPS zinazuwa kati ya dola tatu hadi 15 tu.
(5) Inawezekan fuel pressure regulator imeshachoka kwa hiyo inavujisha mafuta kurudi kwenye tank wakati pressure ni ndogo na kuiacha injini na ukame wa mafuta. Hii ikitokea, gari inaaza kupungukiwa na spidi hata ikiwa katika mwendo wa barabarani wa kawaida, kwa hiyo iwapo ukiwa barabarani hunaoni tatizo lolote basi ni wazi hili siyo tatizo ulilo nalo.
Sababu namba (2) hadi namba (4) zikitokea, ni lazima zitaregister kwenye computer ya gari na utapata checki engine light. Kama inakuonesha check engine light, ipeleke kwenye computer scan ujue ni sensor gani. Kama hakuna check engine light, basi kwa asilimia kubwa ni kwa air filter yako imechoka sana.