Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

N
Nitalifanyia kazi ingawa kuna mtu aliniambia kuwa yawezekana ni kichuma kinachogonga kutoka kwenye starter kwenda kwenye flywheel kinachelewa kurudi ndio maana kinatoa huo mlio...

Hiyo nina uhakika wa karibu 90% kuwa huenda siyo kweli ingawaje inawezekana kuwa ni kweli kwa vile sijui aina ya mlio wenyewe unaopata. Ile bendix ya starter ikiharibika kufikia kiwango hicho cha kushindwa kurudi baada ya kustart, basi vile vile huwa inashindwa kusukuma wakati wa kustart, halafu hiyo haitokei kirahisi vile.
 
Ningependa kujua je kuna ulazima wa gari iliyotembea umbali mrefu kuachwa katika idle position kwa muda fulani kabla ya kuzimwa?

Na kama ulazima upo, gari iwe udle kwa mda gani, na baada ya kutembea kwa umbali kuanzia km ngapi/masaa mangapi?
Hakuna ulazima huo.
 
Naongezea kidogo....kwa magari haya ya siku hizi ya umeme zaidi...mfano EFI, VVTi n.k kama halina turbo..hakuna haja ya kuliacha idle baada ya safari ndefu hata kama umetoka Dar to Mwanza...magari ya kizamni kama yale ya Mfumo wa carburetor ndiyo yalihitaji kuachwa idle angalau dk 15 mpaka 30..

Ila kama gari lako lina turbo, ni lazima uliache idle kama dk 15 mpka 30 baada ya safari ili kuruhusu mfumo mzima wa turbo kupoa kidogo....joto kali huweza kuathiri mdumo huu...
 
Fuel Pump imechoka; ukibadilisha fuel pump, badilisha pia fuel pressure regulator na fuel filter kama gari yako inayo. Kuna magari ambayo hayana fuel filter bali imejengewa ndani ya fuel pressure regulator tu.
Ahsante sana mkuu. Nitafanya hivyo
 
Kosa kubwa ni kuchelewa kubadilisha timing belt. Je, ilipasua piston au ilivunja valve rods? Huenda pia hakukuwa na haja ya kubadilisha Cylinder head iwapo haikupasuka popote. Kama ilipasua piston kweli basi matatizo yalikuwa ni makubwa sana kwani hiyo itakuwa ni pamoja na connecting roads zote na pia crankshaft bearings. Ili kusuka upya injini yako, ondoa piston zote uweke mpya za aina moja, na Connecting rods zote pia uweke za aina moja, vile vile na crankshaft bearings zote uweke za aina moja. fanya hivyo hata kama kuna unavyoona kuwa havina madhara; usichange parts za zamani na mpya kwenye injini.
mzee baba hayo yote si zaidi ya bei ya Mswaki wa half injini???
 
Injini kuzimika wakati wa idling kunasababishwa na sababu nyingi sana ndogo ndogo ambazo hazina madhara kabisa kwenye injini yako. Ngoja nitaje ambazo ni za kawaida sana.

(1) Inawezekana air filter yako imeshajaa uchafu; iangalie na ukiweza uibadilishe.
(2) Inawezekan air flow sensor imeshachafuka au imekufa. Air flow sensor ni kiwaya chembamba sana kinachoweza kukatika hasa iwapo air filter ni chafu. Kama imechafuka, kuna mafuta ya kuisafishia, na kama imekufa unaweza kubadilisha na kuweka nyingine. Zinagharimu kati ya dola mbili hadi kumi na tano tu.

(3) Inawezekana injector zako zina uchafu, kwa hiyo hazipitishi mafuta wakati pressure ni ndogo. Kama tatizo ni hili, kuna injector cleaners ambazo unaweza kuongeza kichupa kimoja kwe tanki la mafuta likiwa full tank kukusafishia injector hizo.

(4) Inawezekana throttle position sensors kwa upande wa chini haifanyi kazi, kwa hiyo ukiachia accelerator basi computer inakuwa haipati taarifa za position ya accelerator yako kwa hiyo inashindwa kujua ni kiasi gani cha mafuta kinahitajiwa na hivyo inaamua kukata mafuta kabisa. TPS zinazuwa kati ya dola tatu hadi 15 tu.

(5) Inawezekan fuel pressure regulator imeshachoka kwa hiyo inavujisha mafuta kurudi kwenye tank wakati pressure ni ndogo na kuiacha injini na ukame wa mafuta. Hii ikitokea, gari inaaza kupungukiwa na spidi hata ikiwa katika mwendo wa barabarani wa kawaida, kwa hiyo iwapo ukiwa barabarani hunaoni tatizo lolote basi ni wazi hili siyo tatizo ulilo nalo.

Sababu namba (2) hadi namba (4) zikitokea, ni lazima zitaregister kwenye computer ya gari na utapata checki engine light. Kama inakuonesha check engine light, ipeleke kwenye computer scan ujue ni sensor gani. Kama hakuna check engine light, basi kwa asilimia kubwa ni kwa air filter yako imechoka sana.

Mkuu nashukuru kwa majibu yako,
Jana Ilibidi tubadili Air-filter maana ni chafu sana.

Pia tuligundua ground terminal ya battery ilikua very loose kiasi kwamba ukivuta na mkono unaweza ukaitoa.
Leo mpaka sasa hilo tatizo halijajirudia na ukizingatia nimekaa sana kwenye foleni asubuhi.

Wiki ijayo nitalipeleka kwenye service kubwa ambapo watalicheck kwenye computer scan, nashukuru mkuu nitakujuza zaidi.
 
Nina gari Toyota premio likipoa nikiwa naliwasha mshale wa silencer hupanda alafu unashuka mpaka zero na huzimika sanasana wakati wa asubuh mpaka niliwashe tena na linaanza kumis mpaka litulie tatizo linaweza kuwa nini naomba msaada
 
mzee baba hayo yote si zaidi ya bei ya Mswaki wa half injini???
Sijui Mswaki ni kitu gani; lakini ni kweli kuwa tatizo ulilopata linaweza kuwa ni kati ya matatizo makubwa sana kwenye injini ya gari. Na gharama inaweza kuwa ni kubwa kulirudisha katika hali yake.
 
Sijui Mswaki ni kitu gani; lakini ni kweli kuwa tatizo ulilopata linaweza kuwa ni kati ya matatizo makubwa sana kwenye injini ya gari. Na gharama inaweza kuwa ni kubwa kulirudisha katika hali yake.
Kibongo bongo mswaki ni nusu injini....unawezq kukuta injini used ambayo haina vifaa vyote...unainunua kisha vifaa ilivyonavyo unahamishia kwenye injini uliyonayo
 
Sijui Mswaki ni kitu gani; lakini ni kweli kuwa tatizo ulilopata linaweza kuwa ni kati ya matatizo makubwa sana kwenye injini ya gari. Na gharama inaweza kuwa ni kubwa kulirudisha katika hali yake.
Nanunua used HALF ENGINE ILALA natumia cylinder head ya gari yangu maana nlibadilisha cylinder head pindi ilipopasua Pison na valves za head ya zamani.

nikabadilizha hio pison moja na head nyingine, sasaivi naona nitafute half engine tu
 
Hiyo ni sawa; ukinunua injini iliyotumika ikiwa na piston zake ukabadilisha cylinder head tu, ni vizuri zaidi kuliko kubadilisha piston moja tu kwenye injini. Kumbuka vitu vya muhimu kama idler pulley na Tensioner pulley kwa sababu bearings zake hufa, oil seals, water pump, timing belt na AC/clutch.
 
Nina gari Toyota premio likipoa nikiwa naliwasha mshale wa silencer hupanda alafu unashuka mpaka zero na huzimika sanasana wakati wa asubuh mpaka niliwashe tena na linaanza kumis mpaka litulie tatizo linaweza kuwa nini naomba msaada

Iwapo ukishaliwasha likapata joto hutulia kabisa mpaka akesho yake basi ina maana kuwa sensor moja iitwayo Mass Air Flow (MAF) sensor ni chafu sana; kuna mafuta maalumu ya kuisafishia. MAF ikiwa chafu inasabababisha injini kupata hewa nyingi sana kuliko mafuta wakati wa kustart, hivyo inashindwa kuchoma mafuta mpaka ipate joto la kutosha.

Labda nikueleze kidogo kwa nini matatizo ya namna hiyo hutokea. Injini ikiwa ya baridi huwa inataka mafuta mengi kuliko kawaida hadi ikishapata joto la kutosha. Kwa hiyo Computer husoma hiyo MAF na pamoja na sensor ya kupima joto la injini kuamua kiasi cha mafuta ya kupeleka kwenye injini. Sasa kama MAF haipeleki ujumbe mzuri kwenye computer ndipo unapokuta computer inaruhusu mafuta machache kuliko yanayotakiwa.

MAF huchafuka iwapo unatumia air cleaner ambayo ni chafu sana.

Kama kusafisha MAF hakusaidii kuoandoa tatizo basi huenda injector na valve zina masizi mengi; weka chupa moja ya mafuta ya kusafishia injector kwenye full tank ya mafuta, baada ya muda kama siku tatu hivi tatizo litatoweka lenyewe. Hata hivyo sababu kubwa ni hiyo ya MAF hapo juu.
 
Iwapo ukishaliwashalikisha likapata joto hutulia kabisa mpka akesho yake basi ina maana kuwa senor moja iitwayo Mass Air Flow (MAF) sensor ni chafu sana; kuna mafuta maalumu ya kuisafishia. MAF ikiwa chafu inasabababisha injini kupata hewa nyingi sana kuliko mafuta wakati wa kustart, hivyo inashindwa kuchoma mafuta mpaka ipate joto la kutosha.

Haya mafuta ya kusafishia injectors yanaitwaje..??
 
Nashukuru kwa ushauri ubarikiwe
 
Bw. Kichuguu umekuwa msaada mkubwa hapa..many thanks.
Nauliza, kuna Land Cruiser ( HZJ 75/78/79 ) zenye engine ya 1Hz baadhi kwenye Air Cleaner zimebandikwa sticker kwamba u change engine oil every 5,000 km na zingine zinaonyesha every 10,000 km inakuaje hapo ? Na zote zinatumia engines za 1Hz ?
 
Haya mafuta ya kusafishia injectors yanaitwaje..??
Haya hapa

1567185910891.png
 
Bw. Kichuguu umekuwa msaada mkubwa hapa..many thanks.
Nauliza, kuna Land Cruiser ( HZJ 75/78/79 ) zenye engine ya 1Hz baadhi kwenye Air Cleaner zimebandikwa sticker kwamba u change engine oil every 5,000 km na zingine zinaonyesha every 10,000 km inakuaje hapo ? Na zote zinatumia engines za 1Hz ?
Inawezekana kuwa magari mengine yalikuwa yametengezwa kwa ajili ya soko la nchi za baridi na mengine soko la nchi za joto. Kwenye nchi za joto unatakiwa ubadilishe oil mapema kuliko kwenye nchi za baridi. Dar es Salaam ni sehemu ya joto, kwa hiyo fuata hiyo km 5,000.

Halafu nikumbushe tena kuwa hizo km huwekwa kama guideline tu lakini kwa jumla wewe mtumiaji unatakiwa uwe unacheki level oil kwenye gari lako mara kwa mara, kwani wakati mwingi sana oil hupundua kabla ya kufikisha maili hizo. Hata kama njini haivuji, kadri gari llinapfsanya kazi kuna oil huwa inaungua kwenye vyuma polepole, ikishapungua na kuwa chini ya kiwango fulani, unatakiwa uibadilishe hata kama maili hizo hazijafika.
 
Back
Top Bottom