Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Mkuu kitunguu gari unabadilisha oil alafu unatembea km 160 then asubh ukichek oil unakuta oil imeliwa imebaki kidogo hapo mkuu tatizo nin gari ya mfano ni brevis
 
Mkuu kitunguu gari unabadilisha oil alafu unatembea km 160 then asubh ukichek oil unakuta oil imeliwa imebaki kidogo hapo mkuu tatizo nin gari ya mfano ni brevis
Jina langu siyo Kitunguu aisee, hebu badilisha; mimi ni Kichuguu, ".....huwezi kulinganisha Kichuguu na mlima Kilimanjaro"

Bila shaka gari yako huwa inatoa moshi mwingi sana, yaani kuna oil inavuja na kuingia kwenye combustion chamber na kuunguzwa pamoja na mafuta. Iwapo injini yako ina nguvu kama kawaida, basi kuna vipete fulani ambamo valve stem hupita (vinaitwa valve guides) huenda vimepanuka sana na kuacha mwanya wa oil kupenya ndani ya injini. Fundi wako akifungua cylinder head cover anaweza kuvikagua na kuona kama vimepanuka. Ni rahisi kuvibadilisha kwani viko kwenye cylinder head, ila utahitaji cylinder head gasket mpya.

Kama Injini haina nguvu kama zamani na vile vile inakula mafuta mengi sana basi huenda piston rings zako zimekwisha; hapo utahitaji kazi kubwa kidogo ya karibu na overhaul kwani itabidi ufungue injini yote kuweka piston rings mpya. Usifanye makosa ukabadilisha piston kwani unaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi. Kazi ya namna hiyo fundi anaweza kuifanya kikamilifu bila kuangusha injini kabisa; utahitaji cylinder head gasket mpya pia.

Piston rings hufa iwapo hubadilishi air filter yako mapema kwani huruhusu vumbi (ambalo ni silica na ni ngumu kama msasa) kuingia ndani ya cylinder na kusaga hizo piston rings na vile vile iwapo hubadilishi engine oil katika muda unaotakiwa.
 
Wengi wanakosea hapa wanaweka 20w50 mm mwenyewe kina kipindi niliambiwa na fundi wa mtaani niiweke gari ikabadilika ikawa inatoa vimlio wa ajabu ila nilivyoconsult manual na kuanza kutumia 5w30 aisee limetulia sometime unaweza hisi halijawaka..
Soma kwanza kitabu cha gari yako, kuna injini nyingi zinataka 5W-30 na 5W-20. Hata hivyo kwa Dar es Salaam ambayo ni sehemu yenye joto sana, unaweza kutumia 10W-30 au 10W-20.
 
Wengi wanakosea hapa wanaweka 20w50 mm mwenyewe kina kipindi niliambiwa na fundi wa mtaani niiweke gari ikabadilika ikawa inatoa vimlio wa ajabu ila nilivyoconsult manual na kuanza kutumia 5w30 aisee limetulia sometime unaweza hisi halijawaka..
20W-50 ni kwa ajili ya ajili ya magari makubwa na makuukuu kweli kweli; kama una gari lenye hali nzuri, oli nzuri ni 5W-20 mpaka 10W-30 ukihusisha grade zote za katikati, yaani 5W-30, na 10W-20. Kadri gari linavyochakaa na wakati wa joto sana ndipo unapandisha namba kidogo kidogo mpaka 10W-30 usizidi hapo kwa gari yoyote ndogo labda kwa basi na roli la mizigo.
 
Kwanini nikiwasha gari yangu inasumbua ila nikikanyaga mafuta inawaka pili inaweza ikawaka yenyewe ila ikakosa nguvu hadi nikanyage mafuta tena
 
Kwanini nikiwasha gari yangu inasumbua ila nikikanyaga mafuta inawaka pili inaweza ikawaka yenyewe ila ikakosa nguvu hadi nikanyage mafuta tena

Tatizo kama hilo nimekwisha lijibu kwenye post #75 hapa


Ngoja nikukopie jibu hilo:

Iwapo ukishaliwashalikisha likapata joto hutulia kabisa mpka akesho yake basi ina maana kuwa senor moja iitwayo Mass Air Flow (MAF) sensor ni chafu sana; kuna mafuta maalumu ya kuisafishia. MAF ikiwa chafu inasabababisha injini kupata hewa nyingi sana kuliko mafuta wakati wa kustart, hivyo inashindwa kuchoma mafuta mpaka ipate joto la kutosha.

Labda nikueleze kidogo kwa nini matatizo ya namna hiyo hutokea. Injini ikiwa ya baridi huwa inataka mafuta mengi kuliko kawaida hadi ikishapata joto la kutosha. Kwa hiyo Computer husoma hiyo MAF na pamoja na sensor ya kupima joto la injini kuamua kiasi cha mafuta ya kupeleka kwenye injini. Sasa kama MAF haipeleki ujumbe mzuri kwenye computer ndipo unapokuta computer inaruhusu mafuta machache kuliko yanayotakiwa.

MAF huchafuka iwapo unatumia air cleaner ambayo ni chafu sana.

Kama kusafisha MAF hakusaidii kuoandoa tatizo basi huenda injector na valve zina masizi mengi; weka chupa moja ya mafuta ya kusafishia injector kwenye full tank ya mafuta, baada ya muda kama siku tatu hivi tatizo litatoweka lenyewe. Hata hivyo sababu kubwa ni hiyo ya MAF hapo juu.
 
Ok mkuu nitashukuru sana, unajua kuwa na gari bila kufuata proper service ilishanicost mafundi wetu wa bongo walishaniulia gear box ya corolla.
Sijapata Toyota Succeed version ya Marekani. Ila bado nipe muda kidogo watu wangu bado wananisaidia kuitafuta
 
Mkuu kichuguu nina gari Toyota Allex cc 1490. Mkoa ambao nipo mchana kunakuwa na jua kali sana na usiku kunakuwa na baridi. Unanishauri nitumie Oil yenye namba ipi.?
 
Mkuu kichuguu nina gari Toyota Allex cc 1490. Mkoa ambao nipo mchana kunakuwa na jua kali sana na usiku kunakuwa na baridi. Unanishauri nitumie Oil yenye namba ipi.?
Tunapozungumza baridi kwenye injini ya gari, Tanzania hakuna baridi, siyo hata lile la Makambako. Kulingana na mileage iliko unaweza kutumia oil yoyote kati ya 5W-20, 10W-20,5W-30, na 10W-30. Kama una zaidi ya km 180,000 tumia ama 5W-30 au 10W-30, na kama ni chini ya km 180,000 tumia 5W-20, 10W-20. Nakushauri zaidi utumie hizo nilizowekea msisitizo
 
Mkuu Kichuguu
Gari yangu ni Starlet Gt nikichomoa stick ya oil engine oil inaruka ruka kama gari nimeiwasha, je ni tatizo gani?
 
Mkuu Kichuguu
Gari yangu ni Starlet Gt nikichomoa stick ya oil engine oil inaruka ruka kama gari nimeiwasha, je ni tatizo gani?
Inawezekana umeweka oil nyingi sana. Vile vile kumbuka ile dip stick ndicho kifuniko imojawapo cha oil; kwa hiyo ukikitoa ina maana umefunua sufuria wakati oil inatokota, na iwapo sump imejaa kuliko kiasi ni lazima oil hiyo itaruka nje. Katika kucheck engine oil, inabidi injini iwe imezimwa. Dip stick ile ina alama mbili, ya asubuhi kabla hujawasha gari ni cold level, na ya wakati wowote mara baada ya kuzima gari ni hot level,
 
@kuchuguu, kuna gari ni Ford Focus ya 2003, CC 1,600. Gari inasumbua sana, sasa kuna advise ya kuchange engene na gear box ili system yote ibadilike.

Kuna fundi kanishauri kuweka injini ya Toyota:

Swali: Je ni injini ya gari gani Toyota inaweza kuwa compatible na iwe na CC between 1,300 - 1,600?
 
Back
Top Bottom