Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Niulize chochote kuhusu injini za magari madogo na pickup zinazotumia Petroli

Boeing 747, Nashukuru mkuu nitafanya kama ulivoshauri
Kwa upande wa tajiri bado ni mpya pia gari haidaiwi chochote hvo vingine itabid niviangalie kama hayo maji ...lakin pia nilisikia brek nikikanyaga zinapiga kelele itakua brek pads au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa unaongea vitu vya maana sana kwenye gari mkuu natamani watanzania wote hasa wanaomiliki magari wawe kama wewe huwa nachukia sana mmiliki kununua gari kwa pesa ndefu zaidi ya million 10 halafu anashindwa kuifanyia service inayotakiwa hasa kwa kuweka vitu genuine huwa nachukia sana maana gari ni kama mtoto unahangaika kulitafuta halafu likishafika duniani unashindwa kulipa matumizi yake stahili inakera sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukran mkuu..
Pamoja sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nashukuru mkuu nitafanya kama ulivoshauri
Kwa upande wa tajiri bado ni mpya pia gari haidaiwi chochote hvo vingine itabid niviangalie kama hayo maji ...lakin pia nilisikia brek nikikanyaga zinapiga kelele itakua brek pads au ?

Sent using Jamii Forums mobile app
Swala la break system ni swala nyeti sana linalobeba maisha ya mtumiaji wa gari..

Nikushauri tafundi fundi mzuri akague kama ni brake pads zimechoka ubadilishe ili zisisage vyuma vingine ambavyo utavibadilisha kwa gharama kubwa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nakuuliza kuhusu gear box kwa kuwa pia ni sehemu ya engine, engine ya gari yangu ni Mitsubishi 3G83, mfumo wa 4 wheel drive haufanyi kazi, baada ya kuiosha sana, nimefuatilia mfumo wa waya naona kama uko sawa, yaani unabonyeza button ndani ina engage 4wd, pia kuna gear lever ya manually ya 4wd unaivuta iwapo mfumo wa umeme haufanyi kazi, lakini zote hizi hazifanyi kazi, tatizo inaweza kuwa nini. Kichuguu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sinajinasasa,
Kuna actuator kwenye matairi ya mbele ambayo ndiyo inayounganisha hub za matairi ya mbele kwenye gear box; huenda actuator hiyo imekufa, au fuse yake imeungua. Kama si hivyo, inawezekana computer inayoongoza gearbox imelock; toa beteri iache kwa kama dakika kumi na tano au nusu saa hivi ndipo uunganishe beteri kusudi computer i-reset na kuanza upya .
 
Poa mkuu labda nijaribishe kutoa betri, lakini gari yangu ni full manual.
Kuna actuator kwenye matairi ya mbele ambayo ndiyo inayounganisha hub za matairi ya mbele kwenye gear box; huenda actuator hiyo imekufa, au fuse yake imeungua. Kama si hivyo, inawezekana computer inayoongoza gearbox imelock; toa beteri iache kwa kama dakika kumi na tano au nusu saa hivi ndipo uunganishe beteri kusudi computer i-reset na kuanza upya .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawasawa mkuu.. Huo ni ushauri (unaweza kuuchukua au kuuacha). Samahani kama nimekukwaza kingjohn255 na sidhani kama nimemwambia asiende kwa TOYOTA WORKSHOPS ila kwa expirience yangu mimi na hao TOYOTA WORKSHOPS ni wako OVERATED na hawakukata kiu yangu

Hebu nirekebishe nilipokosea nijifunze zaidi ndugu yangu.
Duh wewe mjamaa kweli unajitahid kupotosha yaani unamshauri mtu asiende kwenye maduka ya wenye magari yao kwamba hayana spare genuine Bali ni uzushi tu? Ndugu huu ni uongo uliokomaa kupita kiasi haiwezekani mwenye chombo akose spare genuine yake sema tu umempromote huyo mzungu kiaina tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lipi unashauri..kuchange head gasket na seals au kununua mswaki..Gari Ni Subaru
 
Mambo vp mkuu fund alifungua slota kwenye toyota alteza 3s yenyeengine ya yamaha kulikua na uchafu akasafisha kwa kutumia ile spray ya kusafishia


Kuja kurudishia gari sailensa yake inasomaa rpm ya 2000
.
Fund kajaribu kuadjust kacheza nayo imemshinda naomba msaada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mfobi,

IMG_20200130_092810.jpeg
IMG_20200130_091454.jpeg
IMG_20200131_172720.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lipi unashauri..kuchange head gasket na seals au kununua mswaki..Gari Ni Subaru
Kama cylinder head iko safi tu, ni bora kubadili cylinder head gasket tu kwani hata huo mswaki utakaonunua utakuta nao umeshachoka cylinder head gasket.
 
Kama cylinder head iko safi tu, ni bora kubadili cylinder head gasket tu kwani hata huo mswaki utakaonunua utakuta nao umeshachoka cylinder head gasket.
Thanks mkuu..naomba approximately figure
 
Mkuu naomba kuuliza, injin yangu ni 1nz, nikiqasha ikiwa imepoa kabisa inakuwa na nguvu, ila ikipata lilejoto lake lakawaida na tempreture gauge ikapanda mpaka pale inapotakiwa kuwa gari inakuwa nzito kuondoka, kubadili gear nahata kuchanganya, gari haichemshi ila nikitembea umbali mrefu sanaaa inawaka taa ya engin check baada ya muda ina potea japo sio mara kwa mara,

Pia nikiwa usawa wa tank huqa nasikia fuel pump inavuma, nilijaribu kumuuliza fundi akasema sio tatizo tena ndo inafanya kazi vizur japo mm ninawac wac na hilo, maana kwenye magari mengine mbona sijawah ckia fuel pump inavuma kama yanguu...
Kama cylinder head iko safi tu, ni bora kubadili cylinder head gasket tu kwani hata huo mswaki utakaonunua utakuta nao umeshachoka cylinder head gasket.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atakuja Kichuguu kukushauri zaidi...
Ila anza na hiyo fuel pump...mara nyingi ikianza kufa inavuma zaidi kuliko kawaida na gari linakosa nguvu. Kuvuma kwa sana kwa fuel pump ni dadalili za awali kuwa inaelekea kufa na siku si nyingi gari likiwa na mafuta kidogo litakuwa na tabia ya kuzima zima.

Fundi alikupeleka chaka kuwa ikivuma ndiyo inafanya kazi vizuri la hasha.
Hilo la check engine fanya diagnosis ya computer yawezekana ni MAF sensor au Oxygen sensor zimechafuka sana..au huenda ni loose connection ya waya wa kifaa nyeti kama MAF...pia kagua air filter yako huenda iko clogged
rasulimohamed,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
rasulimohamed,
Fuel pump yako imekufa, badili fuel pump utaona gari litakavyochanganya tena.

Kutokana na ushauri uliopewa na fundi wako, ngoja nitoe maelezo ya kina kuhusu kufa kwa fuel pumps kama ifuatavyo. Fuel pump zote siku hizi zinaendeshwa kwa motor ya umeme, na huwa imefungiwa ndani ya tanki. Kuna vitu viwili, ile pump yenyewe inayosukuma mafuta, na motor inayoendesha pump hiyo. Sasa basi kufa kwa pump vile vile kunatokea kwa namna mbili; ile mota inaweza kufa au pump yenyewe inaweza kufa.

Mota ikifa, gari litazimika ghafla na litashindwa kustart kabisa, itabidi utafute breakdown wakuvute; hutaskia pump ikiunguruma. Matatizo ya motor kufa hutokea kwenye magari yenye milage kubwa hasa yale ambayo motor zake zina brush. Magari mengi ya kisasa yanatumia brushless motor, kwa hiyo hayo hayawezi kufa motor kirahisi.

Pump yenyewe ikifa, gari bado litastaart tu, ila litakuwa halina nguvu. Kufa kwa pump hutokea kwa kwa namna mbalimbali kulingana na muundo wa pump yenyewe kwani kuna miundo kadhaa ya pump; kikubwa ni kuwa wakati pump inafanya kazi vizuri hufungulia njia ya mafuta na kuyasukumua mbele huku ikiyazuia kurudi nyuma.

Sasa pump zote hufa baada ya kushindwa kuzuia mafuta kurudi nyuma, inaweza kuwa kuna seal imakufa au valve inayozuia mafuta yasiruid nyuma imekufa au njia ya mafuta imepanuka sana kiasi kuwa pressure inakuwa ndogo; zote hizo zinakuwa zinashababisha mafuta yesiende mbele kwa nguvu, bali mengine yarudi kwenye tanki. Kufa kwa namna hiyo ndiko utasikia motor inaunguruma sana kupeleka mafuta lakini hayaendi ya kutosha.

In fact ukishasikia motor ya pump inaunguruma sana, ina maana computer inaiambia isukume mafuta mengi kwa sababu hayafiki, kwa hiyo motor inajipinda kwa nguvu sana ndipo unasikia muungurumo huo wa pump; motor inakuwa overloaded.
 
Back
Top Bottom