rasulimohamed,
Fuel pump yako imekufa, badili fuel pump utaona gari litakavyochanganya tena.
Kutokana na ushauri uliopewa na fundi wako, ngoja nitoe maelezo ya kina kuhusu kufa kwa fuel pumps kama ifuatavyo. Fuel pump zote siku hizi zinaendeshwa kwa motor ya umeme, na huwa imefungiwa ndani ya tanki. Kuna vitu viwili, ile pump yenyewe inayosukuma mafuta, na motor inayoendesha pump hiyo. Sasa basi kufa kwa pump vile vile kunatokea kwa namna mbili; ile mota inaweza kufa au pump yenyewe inaweza kufa.
Mota ikifa, gari litazimika ghafla na litashindwa kustart kabisa, itabidi utafute breakdown wakuvute; hutaskia pump ikiunguruma. Matatizo ya motor kufa hutokea kwenye magari yenye milage kubwa hasa yale ambayo motor zake zina brush. Magari mengi ya kisasa yanatumia brushless motor, kwa hiyo hayo hayawezi kufa motor kirahisi.
Pump yenyewe ikifa, gari bado litastaart tu, ila litakuwa halina nguvu. Kufa kwa pump hutokea kwa kwa namna mbalimbali kulingana na muundo wa pump yenyewe kwani kuna miundo kadhaa ya pump; kikubwa ni kuwa wakati pump inafanya kazi vizuri hufungulia njia ya mafuta na kuyasukumua mbele huku ikiyazuia kurudi nyuma.
Sasa pump zote hufa baada ya kushindwa kuzuia mafuta kurudi nyuma, inaweza kuwa kuna seal imakufa au valve inayozuia mafuta yasiruid nyuma imekufa au njia ya mafuta imepanuka sana kiasi kuwa pressure inakuwa ndogo; zote hizo zinakuwa zinashababisha mafuta yesiende mbele kwa nguvu, bali mengine yarudi kwenye tanki. Kufa kwa namna hiyo ndiko utasikia motor inaunguruma sana kupeleka mafuta lakini hayaendi ya kutosha.
In fact ukishasikia motor ya pump inaunguruma sana, ina maana computer inaiambia isukume mafuta mengi kwa sababu hayafiki, kwa hiyo motor inajipinda kwa nguvu sana ndipo unasikia muungurumo huo wa pump; motor inakuwa overloaded.