Toyota RAV4 2006 model DBA-ACA36W AWD engine inakula oil na hamna sehemu inavuja. Approximately 500-800km unakuta imepungua kiasi flani. Tatizo litakua nini na solution ni nini?
Pole mkuu...
Mwaenye uzi nadhani amepata dharura kidogo...ila naimani akija atajibu maswali yote vizur..
Lakini na mimi nijibu hivi..
Je, unapata moshi wa blue kwenye gari yako...?
Kama ndiyo, gari yako itakuwa inaunguza oil...
Je, rangi za Spark plugs zako zikoje..?
Kama zimejaa ukurutu mweusi( oily deposit.). ni wazi kwamba gari lako linaunguza oil...
Sababu kuu za gari kuunguza oil ni
1.Uchakavu wa piston rings...hapa gari litapoteza uwezo wa compression na kiasi cha oil kitapenya kwenye kuta za cylinders kupitia piston rings na kuunguzwa kwenye combustion chamber..
Suluhisho...tafuta fundi mzuri akague rings kama zimechoka uweke mpya, tatizo litakwisha.
2. Uchakavu wa valve guide na seals za intake valves...hivi kama vimechoka au seals kama zimekatika, oil itakuwa inafyonzwa kwenye combustion chamber wakati wa kitendo cha intake kinapofanyika...
Suluhisho ni kutafuta fundi mzuri akague na kubadili seals zilizochoka..
*3........Sababu ya tatu ambayo si rasmi inayozungumzwa mitaani ni aina ya oil unayotumia....inasemekana kuna oil fake ambazo zikipata joto kali sana zina evaporate hivyo kufanya kiasi cha oil kupungua....hii ni MYTHS lakini huenda ina ukweli....tuepuke cheap oils..
HITIMISHO....
Kama umejiridhisha vya kutosha kuwa hakuna sehemu yoyote oil inapovuja, ( make sure that no any external leakage of oil) , pia kama unatumia oil zenye viwango vizuri kutoka kampuni zinazoamika, basi wazi kuwa gari lako linakabiliwa na tatizo namba 1 au 2 au zote 1 na 2....
Tafuta fundi mzuri anayejua weledi wa kazi yake akukagulie kwa sababu hayo matatizo yanahusika na sehemu nyeti za injini yako....epukana na fundi mwenye papara kwenye ufunguaji wa engine.
Sent using
Jamii Forums mobile app